Jumapili, 28 Oktoba 2018

Maigizo Yaliyosimuliwa ya Hadithi za Kweli "Upendo wa Kweli wa Mungu" (Swahili Subtitles)

Maigizo Yaliyosimuliwa ya Hadithi za Kweli "Upendo wa Kweli wa Mungu" (Swahili Subtitles)

Ili kujitengenezea nafasi yake mwenyewe duniani, mhusika mkuu alilazimika kufuata mwenendo wa duniani humu, akihangaika na kufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya umaarufu na hadhi. Maisha yake yalilikuwa hasa matupu na yenye maumivu. Baada ya kumwamini Mwenyezi Mungu, alipata maana ya maisha ya binadamu ndani ya maneno ya Mwenyezi Mungu, na akiwa amejawa na furaha, akamfuata Mungu na kutimiza majukumu yake.

Jumamosi, 27 Oktoba 2018

Tamko la Themanini na Saba

Tamko la Themanini na Saba

Lazima uharakishe hatua na ufanye kile Nataka kufanya. Hii ni kusudi Langu lenye hamu kwenu. Inawezekana kuwa kwa wakati huu bado hamjaelewa maana ya maneno Yangu? Inawezekana kuwa bado hamjui kusudi Langu? Nimezungumza wazi zaidi na zaidi, na kusema mengi zaidi, lakini, je, ninyi hamjajitahidi kujaribu kuelewa maana ya maneno Yangu? Shetani, usifikiri kwamba unaweza kuharibu mpango Wangu! Wale wanaomtumikia Shetani, yaani, uzao wa Shetani (hii inahusu wale ambao wanamilikiwa na Shetani.

Maonyesho ya Mungu "Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili" (Official video)


Maonyesho ya Mungu "Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili" (Official video)

Mwenyezi Mungu anasema, "Hiyo ni kwa sababu Roho tayari amekwishaanza kazi Yake, na maneno sasa yameelekezwa kwa watu wa ulimwengu mzima. Hii tayari ni nusu ya kazi. Roho wa Mungu amefanya kazi kubwa hiyo tangu dunia ilipoumbwa; Amefanya kazi tofauti katika enzi tofautitofauti, na katika mataifa tofauti. Watu wa kila enzi wanaiona tabia Yake tofauti, ambayo kwa asili inafichuliwa kupitia kazi tofauti Anazozifanya. Yeye ni Mungu, mwingi wa rehema na wema;

Ijumaa, 26 Oktoba 2018

Tamko la Themanini na Nne

Tamko la Themanini na Nne

Kwa sababu ya ukosefu wao wa ujuzi kunihusu Mimi, mwanadamu amekatiza usimamizi Wangu na kudhoofisha mipango Yangu mara zisizo na idadi, lakini hawajawahi kuweza kuzuia hatua Zangu zinazoendelea mbele. Hii ni kwa sababu Mimi ni Mungu wa hekima. Pamoja na Mimi kuna hekima isiyo na mipaka; pamoja na Mimi kuna siri isiyo na mipaka na isiyoweza kueleweka. Mwanadamu hajawahi kuweza kuielewa na kuifahamu kabisa tangu zamani za kale hadi milele. Je, hilo haliko hivyo?

Neno la Mungu | "Ni Jinsi Gani Mwanadamu Aliyemfafanua Mungu katika Dhana Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?"

Neno la Mungu | "Ni Jinsi Gani Mwanadamu Aliyemfafanua Mungu katika Dhana Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?"

Mwenyezi Mungu anasema, "Historia inaendelea mbele, na pia kazi ya Mungu, na matakwa ya Mungu yanaendelea kubadilika. Haingewezekana kwa Mungu kudumisha hatua moja ya kazi kwa miaka elfu sita, kwani kila mwanadamu anajua kwamba Yeye daima ni mpya na kamwe si mzee. Hangeweza kuendelea kuendeleza kazi sawa na kusulubiwa, na mara moja, mara mbili, mara tatu…. kupigwa misumari kwa msalaba.

Alhamisi, 25 Oktoba 2018

Tamko la Sabini na Saba

Tamko la Sabini na Saba

Kutokuwa na hakika ya maneno Yangu ni sawa na kushikilia mtazamo wa kukanusha kuelekea matendo Yangu. Yaani, maneno Yangu yamebubujika kutoka ndani ya Mwanangu, lakini hamyatilii maanani. Ninyi hamko makini! Maneno mengi yamebubujika kutoka ndani ya Mwanangu, lakini ninyi ni wenye mashaka, hamyajui sana. Ninyi ni vipofu! Hamwelewi madhumuni ya kila kitu ambacho Nimefanya. Je, maneno Ninayoyaeleza kupitia kwa Mwanangu si maneno Yangu?

Gospel Music | "Yule Anayeshikilia Ukuu Juu ya Kila Kitu" | Musical Documentary (Swahili Subtitles)

Gospel Music | "Yule Anayeshikilia Ukuu Juu ya Kila Kitu" | Musical Documentary (Swahili Subtitles)

Kote katika ulimwengu mkubwa mno, sayari zote ya mbingu husogea kwa usahihi katika mizunguko yazo zenyewe. Chini ya mbingu, milima, mito, na maziwa vyote vina mipaka yavyo, na viumbe vyote huishi na kuzaana wakati wa misimu yote minne kulingana na sheria za maisha…. Hili lote limepangwa vizuri sana—je, kuna Mwenye Uwezo Mmoja anayepanga na kutawala yote haya? Tangu tuje katika ulimwengu huu tukilia tumeanza kutekeleza majukumu tofauti katika maisha.