Jumatano, 24 Oktoba 2018

Tamko la Sabini

Tamko la Sabini

Kwamba siri Yangu imefichuliwa na kuonyeshwa bayana, pasi kufichwa tena, ni kwa njia ya neema Yangu na huruma kabisa. Kwamba neno Langu linaonekana miongoni mwa wanadamu, pasi kufichwa tena, hata zaidi ni kwa neema na huruma Zangu. Ninawapenda wote wanaotumia rasilmali kwa moyo safi kwa ajili Yangu na kujitolea Kwangu. Ninawachukia wale wote waliozaliwa na Mimi ilhali ambao hawanijui, hata hunipinga Mimi. Sitamtelekeza mtu yeyote ambaye kwa kweli yu upande Wangu, ila Nitafanya baraka zake ziwe maradufu.

Wimbo wa Injili | "Kusudi la Kazi ya Usimamizi ya Mungu ni Kumwokoa Binadamu" | Wema wa Mungu

Wimbo wa Injili | "Kusudi la Kazi ya Usimamizi ya Mungu ni Kumwokoa Binadamu" | Wema wa Mungu


Upendo na huruma za Mungu
hupenyeza kazi Yake
ya usimamizi kwa utondoti.

I
Ikiwa mwanadamu ahisi mapenzi Yake ya huruma au la,
Yeye hachoki kufuatilia kazi Anayohitaji kufanya.
Ikiwa mwanadamu aelewa usimamizi Wake au la,
kazi Yake huleta usaidizi na utoaji unaoweza kuhisiwa na wote.

Jumanne, 23 Oktoba 2018

Tamko la Themanini

Tamko la Themanini

Kila kitu kinahitaji mawasiliano halisi na Mimi ili kupata nuru na kuangazwa; aidha, ni kwa njia hii tu ndio roho inaweza kuwa na amani. La sivyo, haitakuwa na amani. Sasa ugonjwa mbaya zaidi kati yenu ni kutenganisha ubinadamu Wangu wa kawaida kutoka kwa uungu Wangu kamili; aidha, wengi wenu huweka mkazo kwa ubinadamu Wangu wa kawaida, kama kwamba kamwe hawajui kuwa Mimi nina uungu kamili pia. Hii inanikufuru Mimi! Je, mnajua? Ugonjwa wenu ni mbaya sana kiasi kwamba msipoharakisha kuurekebisha mtauawa kwa mikono Yangu.

Wimbo wa Injili "Kiini cha Kristo Ni Mungu" | Differences Between the True Christ and False Christs

Wimbo wa Injili "Kiini cha Kristo Ni Mungu" | Differences Between the True Christ and False Christs


Mungu anayekuwa mwili anaitwa Kristo,
na hivyo Kristo anayeweza kuwapa watu ukweli anaitwa Mungu.
Si kupita kiasi kusema hivyo,
kwani Ana kiini cha Mungu, Ana tabia ya Mungu na hekima katika kazi Yake,
ambayo haifikiwi na mwanadamu.
Wale wanaojiita Kristo wenyewe ilhali hawawezi kufanya kazi ya Mungu ni wadanganyifu.

Jumatatu, 22 Oktoba 2018

Swahili Praise Song "Upendo wa Mungu Unauzingira Moyo Wangu" Thank and Praise the Lord for His Grace

Swahili Praise Song "Upendo wa Mungu Unauzingira Moyo Wangu" Thank and Praise the Lord for His Grace


Jua la haki linainuka Mashariki.
Ee Mungu! Utukufu Wako unajaza mbingu na dunia.
Mpendwa wangu, upendo Wako unauzunguka moyo wangu.
Wale wanaotafuta ukweli—wanampenda Mungu, kila mmoja.
Asubuhi na mapema, ingawa naamka peke yangu,
furaha iko moyoni mwangu ninavyoyatafakari maneno ya Mungu.

Tamko La Thelathini Na Tano

Tamko La Thelathini Na Tano

Ngurumo saba zinatoka kwenye kiti cha enzi, zinautikisa ulimwengu, zinageuza mbingu na ardhi, na zinavuma angani! Sauti hiyo inapenya sana kiasi kwamba watu hawawezi kuepuka wala kujificha. Nuru ya ghafla ya umeme na sauti ya radi zinatumwa mbele, zikiiangusha chini mbingu na ardhi papo hapo, na watu wamekaribia kufa. Kisha, dhoruba ya mvua kali inafagia ulimwengu wote kwa kasi ya umeme, ikianguka kutoka angani!

Jumapili, 21 Oktoba 2018

Tamko la Thelathini na Sita


Tamko la Thelathini na Sita

Mwenyezi Mungu wa kweli, Mfalme katika kiti cha enzi, hutawala ulimwengu mzima, Anakabiliana na mataifa yote na watu wote, kila kitu chini ya mbingu hung’aa kwa utukufu wa Mungu. Viumbe vyote hai katika miisho ya ulimwengu vitaona. Milima, mito, maziwa, ardhi, bahari na viumbe vyote viishivyo, katika nuru ya uso wa Mungu wa kweli wamefungua mapazia yao, kuhuishwa, kama kuamka kutoka kwa ndoto, kuchipuka kwa kuvunja uchafu!