Kwa sababu yeye alitoka katika familia iliyo masikini, tangu akiwa na umri mdogo Du Juan alikusudia kutengeneza pesa nyingi sana apate kuishi maisha mazuri. Ili kufikia lengo hili, aliacha shule mapema zaidi kwenda kufanya kazi ya mikono, chochote angeweza kufanya ili apate pesa. Yeye hakulalamika wakati kazi ilikuwa ngumu na ya kuchokesha.
27. Ni Nini Husababisha Uongo
Xiaojing Jijini Heze, Mkoani Shandong
Kila mara nilipoona neno la Mungu likituomba kuwa watu waaminifu na kuzungumza kwa usahihi, niliwaza, “Sina tatizo na kuzungumza kwa usahihi. Si ni kusema tu kitu jinsi kilivyo na kusema mambo jinsi yalivyo? Je, hiyo si rahisi? Kilichokuwa kimenikera zaidi daima katika dunia hii walikuwa watu waliotia chumvi walipozungumza.”