47. Siri Zilizofichwa Nyuma ya Ukimbizaji
Li Li Mji wa Dezhou, Mkoa wa Shandong
Sio muda mrefu uliopita, nilitiwa moyo na Mungu na kupandiswa cheo kuwa mfanyakazi wa eneo. Siku moja, nilipokuwa nimekusanyika na wafanyakazi wenzangu, sikuweza kujizuia kufikiria mwenyewe: ni lazima nifanye vyema. Ningetimiza wajibu wangu vibaya, viongozi wangu na wafanyakazi wenzangu wangenionaje?