Jumatatu, 1 Julai 2019

Maneno ya Roho Mtakatifu | “Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Kumi na Nne”


Maneno ya Roho Mtakatifu | “Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima Tamko la Kumi na Nne”

Mwenyezi Mungu anasema, “Nasimama juu ya ulimwengu wote siku baada ya siku, nikichunguza, na kujificha Mimi Mwenyewe kwa unyenyekevu katika nyumba Yangu kupata uzoefu wa maisha ya binadamu, Nikichunguza kwa karibu matendo yote ya mwanadamu.
Hakuna aliyewahi kujitolea Kwangu kwa kweli. Hakuna aliyewahi kufuata ukweli. Hakuna aliyewahi kuwa mwangalifu Kwangu. Hakuna aliyewahi kufanya maazimio mbele Yangu na kufanya wajibu wake. Hakuna aliyewahi kuniruhusu kuishi ndani yake. Hakuna aliyewahi kunithamini kama afanyavyo maisha yake. Hakuna aliyewahi kuona kwa vitendo vya ukweli uzima wote wa uungu Wangu. Hakuna aliyewahi kutamani kuwasiliana na Mungu wa vitendo Mwenyewe.”Wakati maji yanameza wanadamu, Nawaokoa kutokana na maji yaliyotuama na kuwapa nafasi ya kuishi upya. Wanadamu wanapopoteza imani yao ya kuishi, Nawavuta juu kutoka ukingo wa kifo, na kuwapa ujasiri wa kuishi, ili kwamba wananichukua kama msingi wa kuwepo kwao. Wanadamu wanaponiasi, Nawafanya Kunijua kwa kuasi kwao. Kutokana na asili ya zamani ya binadamu na kutokana na huruma Yangu, badala ya kuwaua binadamu, Nawaruhusu kutubu na kuanza upya. Wakati wanadamu wanateseka na kiangazi, Nawatoa kifoni kama bado wamesalia na pumzi moja, kuwazuia kudanganywa na Shetani. Watu wameona mikono Yangu mara ngapi; watu wameona uso Wangu karimu mara ngapi, kuuona uso Wangu wa tabasamu; na wameona adhama Yangu mara ngapi, kuona ghadhabu Yangu. Ingawa binadamu haujawahi kunijua, Siwakamati juu ya udhaifu wao kufanya matata yasiyohitajika. Kupitia ugumu wa binadamu, Nina huruma na udhaifu wake. Ni kwa sababu ya kuasi kwa wanadamu, kutokuwa na shukrani kwao, ndiko Nawaadibu kwa viwango tofauti.

Tazama zaidi:
Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | "Ufalme wa Milenia Umewasili"  

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni