Jumanne, 19 Februari 2019

Maonyesho ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV Utakatifu wa Mungu (I)” Sehemu ya Kwanza

Maonyesho ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV Utakatifu wa Mungu (I)” Sehemu ya Kwanza

Maneno ya Mungu katika video hii ni kutoka kitabu “Neno Laonekana katika Mwili”.
Maudhui ya video hii:
Amri ya Yehova Mungu kwa Mwanadamu
Nyoka Anamshawishi Mwanamke

Kwanza wacha tufafanue neno “takatifu.” Mkitumia utambuzi wenu na kutoka kwa maarifa yenu mmefunzwa, mnaelewa ufafanuzi wa “takatifu” kuwa nini? Nifafanulieni. (“Takatifu” inamaanisha bila doa, bila upotovu au dosari yoyote ya binadamu. Kila kitu inachonururisha—kiwe kwa mawazo, matamshi ama vitendo, kila kitu inafanya—ni chema kabisa.) Vizuri kabisa. (“Takatifu” ni ya Mungu, haijanajisiwa, isiyokosewa na mtu. Ni ya kipekee, ni ishara ya tabia ya Mungu.) (“Takatifu” haina doa na ni kipengele cha Mungu, tabia isiyokosewa.) Huu ni ufafanuzi wako. Katika moyo wa kila mtu, neno hili “takatifu” lina wigo, ufafanuzi na fasiri. Kwa kiwango cha chini kabisa, mnapoona neno “takatifu” akili zenu si tupu. Mna wigo fulani uliofafanuliwa wa neno hili, na ufafanuzi huu wa watu wengine uko karibu kutumia neno hili kufafanua kiini cha tabia ya Mungu. Hii ni vizuri sana. Watu wengi zaidi wanaamini neno “takatifu” ni neno njema, na hii inaweza kuthibitishwa. Lakini utakatifu wa Mungu Ninaotaka kushiriki leo hautafafanuliwa tu, ama kuelezwa tu. Badala yake, Nitatumia baadhi ya ukweli kudhihirisha ili kukuruhusu kuona kwa nini Nasema Mungu ni mtakatifu, na mbona Natumia neno “takatifu” kuelezea kiini cha Mungu. Kabla ya ushirika wetu kuisha, utahisi kwamba matumizi ya neno “takatifu” kuelezea kiini cha Mungu na matumizi ya neno hili kumrejelea Mungu yanastahili sana na yanafaa. Kwa kiwango cha chini zaidi, kuhusiana na lugha za sasa za binadamu, kutumia neno hili kumrejelea Mungu kunafaa hasa—ni neno pekee kwa lugha ya binadamu linalofaa kabisa kumrejelea Mungu. Si neno tupu linapotumika kumrejelea Mungu, wala si sifa bila sababu au pongezi tupu. Madhumuni ya ushirika wetu ni kumruhusu kila mtu kuutambua ukweli wa kipengele hiki cha kiini cha Mungu. Mungu haogopi uelewa wa watu, bali kutoelewa kwao tu. Mungu anataka kila mtu ajue kiini Chake na kile Anacho na alicho. Hivyo kila wakati tunapotaja kipengele cha kiini Cha Mungu, tunaweza kutumia ukweli mwingi kuwaruhusu watu kuona kwamba kipengele hiki cha kiini cha Mungu kweli kipo.

kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Yaliyopendekezwa: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni