Maneno ya Roho Mtakatifu | "Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu" (Sehemu ya Pili)
Mwenyezi Mungu anasema, "Katika kila aina ya kazi ya Mungu kuna maono yanayofahamika na mwanadamu; maono yanayofuatwa na matarajio mwafaka ya Mungu kwa mwanadamu. Bila haya maono kama msingi, mwanadamu hawezi kuwa na uwezo wa utendaji na pia hangeweza kumfuata Mungu bila kuyumbayumba. Ikiwa mwanadamu hamjui Mungu au hayaelewi mapenzi ya Mungu, basi yote ayafanyayo ni bure na yasiyoweza kukubalika na Mungu.
Hata mwanadamu awe na vipawa vingi kiasi gani, bado hawezi kujitenga na kazi ya Mungu na uongozi wa Mungu. Bila kujali uzuri na wingi wa matendo ya mwanadamu, bado hayawezi kuchukua nafasi ya kazi ya Mungu. Kwa hivyo basi, utendaji wa mwanadamu hauwezi kutenganishwa na maono katika hali yoyote ile. Wale ambao hawakubali maono mapya hawana vitendo vipya. Vitendo vyao havina uhusiano na ukweli kwani wanajifunga katika mafundisho ya dini na kufuata sheria zilizokufa; hawana maono mapya kabisa na kwa sababu hiyo hawatendi kulingana na enzi mpya. Wamepoteza maono na kwa kufanya hivyo wamepoteza kazi ya Roho Mtakatifu, hivyo basi kupoteza ukweli pia."
Yaliyopendekezwa: Asili ya Kanisa la Mwenyezi Mungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni