Filamu za Kikristo "Toka Nje ya Biblia" (2) - Je, Tunaweza Kupata Uzima wa Milele kwa Kushikilia Biblia?
Katika siku za mwisho Mwenyezi Mungu anafanya kazi yake ya hukumu na kuleta njia ya uzima wa milele, na ni kwa kukubali ukweli uliolezewa na Kristo siku zile za mwisho tunaweza kupata uzima wa milele. Hata hivyo wachungaji na wazee wa kanisa wa ulimwengu wa kidini wanasema kwamba uzima upo katika Biblia, na ilimradi tu tuzingatie Biblia basi tunaweza pata uzima wa milele. Je, ni Biblia iliyo na uzima wa milele, ama ni Kristo?
Wakati wakale ambapo Bwana Yesu alikuwa akifanya kazi Yake, Mafarisayo walikataa kukubali wokovu wa Bwana msingi wao ukiwa kisingizio kuwa uzima wa milele ulikuwa katika Biblia, kwa hivyo Bwana Yesu akawakemea Mafarisayo akisema, "Tafuteni katika maandiko; kwa kuwa ndani yake mnafikiri kuwa mnao uhai wa milele: na nashuhudiwa na hayo. Nanyi hamkuji kwangu, ili mpate uhai" (Yohana 5:39-40). Je, Biblia inaweza wakilisha Mungu akiweka uzima kwetu sisi? Kweli tunaweza kupata uzima wa milele kwa kushikilia Biblia? Katika Video hii tutajadiliana maswali haya pamoja.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni