Jumamosi, 17 Machi 2018

Umeme wa Mashariki | Njia… (3)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki
Umeme wa Mashariki | Njia… (3)

Umeme wa Mashariki | Njia… (3)


Mwenyezi Mungu alisema, Katika maisha Yangu, Niko radhi kila mara kujitolea Mwenyewe kwa Mungu kabisa, mwili na fikra. Kwa njia hii, hakuna lawama kwa dhamiri Yangu na Naweza kupata kiasi kidogo cha amani. Mtu anayeandama uzima ni lazima kwanza aukabidhi moyo wake wote kwa Mungu kabisa. Hili ni sharti la mwanzo. Ningependa ndugu na dada Zangu wamwombe Mungu pamoja na Mimi: “Ee Mungu! Roho Wako aliye mbinguni awape neema watu walio duniani ili moyo Wangu uweze kukugeukia Wewe kikamilifu, kwamba Roho Yangu iweze kusisimuliwa Nawe, na kwamba Niweze kuona kupendeza Kwako ndani ya moyo Wangu na Roho Yangu, ili wale walio duniani wabarikiwe kuuona uzuri Wako. Mungu! Roho Wako mara tena asisimue roho zetu ili upendo wetu uwe wa kudumu na usibadilike kamwe!” Kile ambacho Mungu hufanya ndani yetu sote ni kuijaribu mioyo yetu kwanza, na tunapomimina mioyo yetu ndani Yake, ni wakati huo ndipo Yeye huanza kusisimua roho zetu. Ni katika roho tu ndipo mtu anaweza kuona kupendeza, uwezo wa juu kabisa, na ukuu wa Mungu. Hii ni njia ya Roho Mtakatifu ndani ya wanadamu. Je, una maisha ya aina hii? Umepitia maisha ya Roho Mtakatifu? Roho yako imesisimuliwa na Mungu? Umeona jinsi Roho Mtakatifu hufanya kazi ndani ya watu? Umeukabidhi moyo wako kwa Mungu kabisa? Ukiukabidhi moyo wako kwa Mungu kikamilifu, unaweza kupitia moja kwa moja maisha ya Roho Mtakatifu, na kazi Yake inaweza kufichuliwa daima kwako. Wakati huo, unaweza kuwa mtu anayetumiwa na Roho Mtakatifu. Je, uko radhi kuwa mtu wa aina hiyo? Katika kumbukumbu Yangu, Niliposisimuliwa na Roho Mtakatifu na kumpa Mungu moyo Wangu mara ya kwanza, Nilianguka chini mbele Yake na kupaza sauti: “Ee Mungu! Ni Wewe uliyeyafungua macho Yangu ili Niweze kutambua wokovu Wako. Niko radhi kukupa Wewe moyo Wangu kabisa, na kile Ninachoomba ni kwamba mapenzi Yako yafanyike. Kile Ninachotamani ni kwamba moyo Wangu upate kibali Chako machoni Pako, na kutekeleza mapenzi Yako.” Ombi hilo ndilo lisilosahaulika kamwe Kwangu; Nilisisimuliwa sana, na Nikalia kwa uchungu mbele ya Mungu.Hilo lilikuwa ombi Langu lililofanikiwa la kwanza mbele ya Mungu kama mtu ambaye ameokolewa, na ilikuwa hamu Yangu ya kwanza. Nilisisimuliwa mara kwa mara na Roho Mtakatifu baada ya hilo. Umekuwa na aina hii ya tukio? Ni jinsi gani Roho Mtakatifu amefanyaje kazi ndani yako? Nafikiri kwamba watu wanaotafuta kumpenda Mungu wote watakuwa na aina hii ya tukio, kwa viwango vikubwa zaidi au vidogo zaidi, lakini watu huyasahau. Mtu akisema hajakuwa na aina hii ya tukio, hii inathibitisha kwamba bado hajaokolewa na bado yuko chini ya miliki ya Shetani. Kazi ambayo Roho Mtakatifu hutekelza ndani ya kila mtu ni njia ya Roho Mtakatifu, na pia ni njia ya mtu anayemwamini na kumtafuta Mungu. Hatua ya kwanza ya kazi ambayo Roho Mtakatifu hutenda juu ya watu ni ile ya kusisimua roho zao. Baada ya hiyo, wataanza kumpenda Mungu na kuandama maisha; wale wote walio katika njia hii wako ndani ya mkondo wa Roho Mtakatifu. Huu sio uwezo tu wa kazi ya Mungu katika China bara, lakini pia katika ulimwengu mzima. Yeye hufanya hili juu ya wanadamu wote. Ikiwa mtu hajasisimuliwa hata mara moja tu, hii inaonyesha kwamba yeye yuko nje ya mkondo huu wa kupata tena. Mimi humwomba Mungu bila kukoma katika moyo Wangu kwamba Atawasisimua watu wote, kwamba kila mtu chini ya jua asisimuliwe Naye na kutembea njia hii. Labda hili ni ombi ndogo sana Ninalomwomba Mungu, lakini Naamini kwamba Atatenda hili. Natarajia kwamba ndugu na dada Zangu wote wataliombea hili, kwamba mapenzi ya Mungu yatendeke, na kwamba kazi Yake ihitimishwe hivi punde ili Roho Wake aliye mbinguni aweze kuwa na raha. Hili ni tarajio Langu dogo.
Naamini kwamba kwa vile Mungu anaweza kutekeleza kazi Yake katika mji mmoja wa pepo wabaya, basi Anaweza bila shaka kutekeleza kazi Yake katika miji mingi ya pepo wabaya kutoka upande mmoja hadi mwingine wa ulimwenguni. Sisi ambao ni wa enzi ya mwisho tutaona bila shaka siku ya utukufu wa Mungu. Hii inaitwa “kufuata hadi mwisho kutasababisha wokovu.” Hakuna anayeweza kubadilisha hatua hii ya kazi ya Mungu—ni Mungu Mwenyewe tu anaweza kufanya hivyo. Hii ni kwa sababu ni ya ajabu; ni hatua ya kazi ya ushindi, na wanadamu hawawezi kuwashinda wanadamu wengine. Ni maneno tu ya kutoka kinywani mwa Mungu na mambo Ayafanyayo binafsi ndiyo yanaweza kuwashinda wanadamu. Kutoka kwa ulimwengu mzima, Mungu anatumia nchi ya joka kuu jekundu kama uwanja wa majaribio. Baada ya hili, Ataanza kazi hii mahali pengine pote. Hiyo inamaanisha kwamba Mungu atatekeleza hata kazi kubwa zaidi ulimwenguni kote, na watu wote wa ulimwengu watapokea kazi ya Mungu ya ushindi. Watu wa kila madhehebu na kila kikundi lazima wakubali hatua hii ya kazi. Hii ni njia ambayo ni lazima ifuatwe—hakuna anayeweza kuiepuka. Je, uko radhi kukubali hiki ulichoaminiwa na Mungu? Mimi huhisi kila mara kwamba kukubali kitu unachoaminiwa na Roho Mtakatifu ni jambo la utukufu. Vile Ninavyoona, hii ndiyo amana kuu sana ambayo Mungu huweka katika wanadamu. Natarajia kuwa na ndugu na dada Zangu wakifanya kazi kwa bidii ubavuni Mwangu na kukubali hili kutoka kwa Mungu, ili Mungu atukuzwe kotekote katika ulimwengu mzima, na maisha yetu hayatakuwa bure. Tunapaswa kumfanyia Mungu kitu, au tunapaswa kula kiapo. Ikiwa mtu anaamini katika Mungu lakini hana kusudi la kufuatilia, basi maisha yake huwa kazi bure, na wakati ufikapo wa yeye kufa, wao wana anga la samawati na ardhi ya vumbi tu ya kutazama. Je, hayo ni maisha ya maana? Ikiwa unaweza kutimiza masharti ya Mungu ukiwa bado hai, hili si jambo zuri? Mbona kila mara unatafuta tatizo, na mwenye huzuni? Kwa njia hiyo unapata chochote kutoka kwa Mungu? Mungu anaweza kupata chochote kutoka kwako? Katika ahadi Niliyofanya na Mungu, Mimi nampa tu moyo Wangu na Simpumbazi kwa maneno Yangu. Singefanya kitu kama hicho—Mimi niko radhi tu kumfariji Mungu Nimpendaye kwa moyo Wangu, ili Roho Wake aliye mbinguni afarijiwe. Moyo unaweza kuwa na thamani lakini upendo una thamani kuu zaidi. Niko radhi kumtolea Mungu upendo wa thamani kubwa zaidi moyoni Mwangu ili kile Anachofurahia kiwe ni kitu kizuri zaidi Nilichonacho, ili Atimizwe na upendo Ninaomtolea Yeye. Je, uko radhi kumpa Mungu upendo wako ili Afurahie? Je, uko radhi kuifanya hii kuwa kanuni yako wewe ya kuendelea kuishi? Ninachoona kutokana na uzoefu Wangu ni kwamba kadri Ninavyompa Mungu upendo mwingi, ndivyo Ninavyohisi kwamba Ninaishi kwa furaha, na Nina nguvu zisizo na mipaka, Niko radhi kutoa mwili na mawazo Yangu yote kama dhabihu, na kuhisi kila mara kwamba Siwezi kabisa kumpenda Mungu vya kutosha. Kwa hiyo je, upendo wako ni upendo usio muhimu, au ni usio na kikomo, wa kupita kiasi? Ikiwa kweli unataka kumpenda Mungu, utakuwa kila mara na upendo zaidi wa kumrudishia Yeye. Ikiwa hali ni hiyo, ni mtu gani na ni kitu gani kina uwezo wa kuzuia upendo wako kwa Mungu?
Mungu huona upendo wa wanadamu wote kuwa wa thamani; Yeye hulimbikiza baraka Zake nyingi zaidi juu ya wote wanaompenda Yeye. Hii ni kwa sababu upendo wa mwanadamu ni mgumu sana kupatikana, kunao kidogo sana, na nusura usiweze kupatikana. Kotekote ulimwenguni, Mungu amejaribu kudai kwamba watu warudishe upendo Kwake, lakini katika enzi zote mpaka sasa, wale ambao wametoa upendo halisi kwa Mungu ni wachache—ni wachache katika idadi. Kadri Ninavyokumbuka, Petro alikuwa mmoja, lakini aliongozwa binafsi na Yesu na ni wakati tu wa kifo chake ndipo alipompa Mungu upendo wake wote, kumaliza hayo maisha yake. Kwa hivyo, ni katika aina hizi za hali zisizofaa ndipo Mungu amefanya eneo la kazi Yake kuwa dogo katika ulimwengu, kwa kutumia nchi ya joka kuu jekundu kama maonyesho. Anaelekeza nguvu Zake zote na juhudi Zake zote mahali pamoja. Hii itakuwa na matokeo yenye kufaa zaidi na itakuwa ya faida zaidi kwa ushahidi Wake. Ni katika hali hizi mbili ndipo Mungu alisongeza kazi Yake ya ulimwengu mzima kwa watu hawa wenye uhodari duni katika China bara na kuanza kazi Yake yenye upendo ya ushindi ili baada ya watu hawa kuweza kumpenda Yeye, Aweze kutekeleza hatua inayofuata ya kazi Yake. Huu ni mpango wa Mungu. Matunda ya kazi Yake yatakuwa makubwa zaidi kwa njia hii. Eneo la kazi Yake liko katikati na limedhibitiwa. Ni wazi kuhusu namna ya kiasi kukubwa cha gharama ambayo Mungu amelipa na kiasi cha juhudi ambazo Ametumia kwa kutekeleza kazi Yake ndani yetu, kwamba siku yetu imefika. Hii ni baraka yetu. Kwa hivyo, kile ambacho hakilingani na fikira za wanadamu ni kwamba wenyeji wa Magharibi hutuonea wivu kwa kuzaliwa mahali pazuri, lakini sisi wote hujiona kuwa duni na wanyonge. Je, huyu si Mungu anayetuinua? Uzao wa joka kuu jekundu ambao wamekuwa wakikandamizwa kila mara wanategemewa na wenyeji wa Magharibi—hii ni baraka yetu kweli. Ninapofikiria juu ya hili, ninajawa na wema wa Mungu, na upendo na ukaribu Wake. Kutokana na hili inaweza kuonekana kwamba lile afanyalo Mungu ni kinyume cha fikira za wanadamu, na ingawa watu hawa wote wamelaaniwa, Hashurutishwi na shutuma za sheria na Amelenga kwa kudhamiria kazi Yake pande zote za kuzunguka sehemu hii ya dunia. Hii ndio maana nafurahi, ndio maana nahisi furaha ya kupita kiasi. Kama mtu anayechukua wajibu wa kuongoza katika kazi hii, kama vile makuhani wakuu miongoni mwa Waisraeli, Ninaweza kutekeleza moja kwa moja kazi ya Roho na kuhudumia moja kwa moja Roho wa Mungu; hiii ni baraka Yangu. Nani angethubutu kufikiria juu ya jambo kama hili? Lakini leo, hili limetujia sisi bila kutazamiwa. Ni furaha kuu kweli inayostahili sherehe yetu. Natarajia kwamba Mungu ataendelea kutubariki na kutuinua ili sisi tulio katika lundo la samadi tutumiwe kwa kiwango kikubwa na Mungu, hivyo kuturuhusu kulipa upendo Wake.
Kulipa upendo wa Mungu ni njia ambayo Ninafuata sasa, lakini Nahisi kwamba haya si mapenzi ya Mungu, wala si njia Ninayopaswa kutembea. Mapenzi ya Mungu ni kuwa Mimi nitumiwe kwa kiwango kikubwa na Yeye—hii ni njia ya Roho Mtakatifu. Labda Nimekosea. Nafikiri hii ni njia Ninayofuata tangu Nilipoanzisha azimio Langu na Mungu kitambo sana. Niko radhi kumwacha Mungu aniongoze ili Niingie katika njia Ninayopaswa kuifuata mapema iwezekanavyo, na kuridhisha mapenzi ya Mungu mapema iwezekanavyo. Bila kujali kile ambacho wengine watafikiria, Naamini kwamba kutekeleza mapenzi ya Mungu ni la muhimu zaidi na ni jambo muhimu zaidi la maisha Yangu. Hakuna yeyote anayeweza kuninyang’anya Mimi haki hii—huu ni mtazamo Wangu binafsi, na labda kuna wengine ambao hawawezi kuufahamu, lakini naamini kwamba Sihitaji kuthibitisha uhalali wa hili kwa yeyote. Nitafuata njia Ninayopaswa kufuata—mara tu Nikitambua njia Ninayopaswa kuifuata Nitaifuata na Sitarudi nyuma. Hivyo Narudi kwa maneno haya: Nasababisha moyo Wangu kutekeleza mapenzi ya Mungu. Natazamia kwamba ndugu na dada Zangu hawatanikosoa! Kwa jumla, Ninavyoona binafsi, watu wengine wanaweza kusema wanachopenda, lakini Nahisi kwamba kutekeleza mapenzi ya Mungu ni muhimu sana na Sipaswi kutii vizuizi kuhusu hili. Siwezi kukosea Ninapotekeleza mapenzi Yake, na kufanya hili hakuwezi kupangwa kulingana na upendeleo Wangu mimi! Naamini kwamba Mungu ameona ndani ya moyo Wangu! Kwa hivyo ni jinsi gani unapaswa kufahamu hili? Uko radhi kujitolea mwenyewe kwa ajili ya Mungu? Uko radhi kutumiwa na Mungu? Azimio lako wewe ni kutekeleza mapenzi ya Mungu? Natarajia kwamba ndugu na dada Zangu wote wanaweza kupata msaada wa kiwango fulani kutoka kwa maneno Yangu. Ingawa maoni Yangu mimi ni ya juujuu, bado Ninasema Ninachoweza kusema ili sote tuweze kuwa na mazungumzo ya wazi yasiyo na vizuizi, ili Mungu abaki miongoni mwetu milele. Haya ni maneno kutoka moyoni Mwangu. Sawa! Hayo ni yote kuhusu maneno Yangu ya dhati kwa leo. Natarajia kwamba ndugu na dada Zangu wataendelea kufanya kazi kwa bidii, na Natarajia kwamba Roho wa Mungu atatutunza kila wakati!

kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni