Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Kushinda (1) | Umeme wa Mashariki |
Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Kushinda (1)|Umeme wa Mashariki
Mwenyezi Mungu alisema, Wanadamu kwa kupotoshwa sana na Shetani, hawajui kuwa kuna Mungu na wameacha kumwabudu Mungu. Adamu na Hawa walipoumbwa mwanzoni, utukufu wa Yehova na Ushuhuda wa Yehova daima vilikuwepo. Lakini baada ya kupotoshwa, mwanadamu alipoteza utukufu na ushuhuda kwa sababu kila mtu alimwasi Mungu na kuacha kumtukuza kabisa.
Kazi ya sasa ya kushinda ni kuupata ushuhuda na utukufu wote, na kuwafanya wanadamu wote wamwabudu Mungu, ili kuwepo na ushuhuda miongoni mwa viumbe wote. Hili ndilo linapaswa kufanywa katika hatua hii ya kazi. Wanadamu watashindwa vipi hasa? Watapata kushindwa kwa kutumia hii kazi ya maneno kumshawishi mwanadamu kwa dhati; kwa kutumia toba, hukumu, kuadibu, na laana isiyo na huruma kumhini kabisa; na kwa kuweka wazi uasi wa mwanadamu na kwa kuhukumu upinzani wake ili ajue udhalimu wa mwanadamu na uchafu wake, mambo ambayo yatatumiwa kuangazia tabia ya haki ya Mungu. Kwa kiwango kikubwa, ni matumizi ya maneno haya yatakayomshinda mwanadamu na kumshawishi kabisa. Maneno ndiyo njia ya kuwashinda wanadamu na wote wanaokubali ushindi lazima wakubali mapigo na hukumu ya maneno. Mchakato wa sasa wa kunena ni mchakato wa kushinda. Ni kwa njia gani watu wanapaswa hasa kushirikiana? Ni kwa kula na kunywa haya maneno ipasavyo na kuyafahamu. Watu hawawezi kujipatia ushindi wao wenyewe. Ni lazima, kwa kula na kunywa haya matamshi, wapate kufahamu uovu na uchafu wao, uasi na udhalimu wao, na waanguke chini mbele ya Mungu. Ikiwa waweze kufahamu mapenzi ya Mungu kisha uyatie katika vitendo, na zaidi, uwe na maono, na ikiwa waweza kuyatii maneno haya kabisa na usitende kulingana na mapenzi yako, basi utakuwa umeshindwa. Na itakuwa ni haya maneno yamekuwezesha kushindwa. Ni kwa nini wanadamu walipoteza ushuhuda? Ni kwa sababu hakuna aliye na imani kwa Mungu au anamshikilia Mungu rohoni mwake. Kuwashinda wanadamu kunamaanisha watu wairudie hii imani. Watu daima wanauegemea ulimwengu, wakiwa na matumaini mengi sana, wakitaka kujua mengi sana kwa ajili ya maisha yao ya usoni, na wakiwa na mahitaji mengi ya kupita kiasi mengi. Wanaifikiria na kuipangia miili yao kila mara wala hawatamani kutafuta njia ya kumwamini Mungu. Roho zao zimetekwa na Shetani, wameacha kumheshimu Mungu, na wanatoa mioyo yao kwa Shetani. Ila mwanadamu aliumbwa na Mungu. Hivyo, mwanadamu amepoteza ushuhuda, kumaanisha amepoteza utukufu wa Mungu. Kusudi la kumshinda mwanadamu ni kuurejesha utukufu wa mwanadamu wa kumheshimu Mungu. Inaweza kusemwa hivi: Kuna watu wengi wasiofuatilia uzima; hata kama kuna wengine, idadi hiyo inaweza kuhesabiwa kwa vidole vya mtu. Watu wanahangaishwa sana kuhusu siku zao za baadaye na hawatilii maanani uzima kwa vyovyote vile. Watu wengine huasi dhidi ya Mungu na kumpinga, humhukumu bila Yeye kufahamu na hawatendi ukweli . Siwajali watu hawa kwa sasa, na Najizuia kushughulikia tabaka hili la wana wa uasi kwa sasa. Katika siku za usoni utaishi gizani, ukilia na kusaga meno yako. Wewe huhisi thamani ya nuru unapoishi ndani yake, lakini utatambua thamani yake mara tu unapoishi katika usiku wa giza. Utasikitika wakati huo. Unahisi vizuri sasa, lakini itafika siku ambayo utasikitika. Siku hiyo itakapofika na giza lishuke na nuru isiweko tena, majuto yako yatakuwa yamechelewa. Ni kwa sababu bado huelewi kazi ya sasa ndio unakosa kutunza wakati wako sasa. Mara tu kazi ya ulimwengu mzima ianzapo, kumaanisha wakati ambapo kila kitu Nisemacho leo kimetimia, watu wengi watakuwa wakishikilia vichwa vyao kwa kilio cha uchungu. Je, huko sio kuingia katika giza na kulia na kusaga meno? Watu wote ambao hufuatilia uzima kweli na wamefanywa kuwa kamili watatumiwa, huku wana wote wa uasi ambao hawafai kutumiwa wataingia gizani, bila kupokea kazi yoyote ya Roho Mtakatifu kwa vyovyote vile na kubaki wasioweza kufahamu chochote. Hivyo wataingia katika adhabu kuomboleza na kutokwa na machozi. Kama umejiandaa vyema katika awamu hii ya kazi na maisha yako yamekomaa, basi wewe ni mtu unayefaa kutumiwa. Kama umejiandaa vibaya, basi hata kama umejitayarisha kwa awamu inayofuata ya kazi utakuwa hufai. Wakati huo, hata kama utataka kujiandaa mwenyewe, nafasi itakuwa imepita. Mungu atakuwa ameondoka; utaenda wapi basi kutafuta aina ya nafasi iliyo mbele yako sasa, na utaenda wapi basi kupokea zoezi linalotolewa na Mungu binafsi? Wakati huo, haitakuwa Mungu akinena binafsi au Mungu akitoa sauti Yake binafsi. Utaweza tu kusoma kinachosemwa leo; utawezaje kuelewa kwa urahisi? Ni vipi ambavyo maisha ya baadaye yataweza kulingana na ya leo? Wakati huo, kulia na kusaga meno kwako hakutakuwa kupitia kifo kilicho hai? Baraka inatolewa kwako sasa lakini hujui namna ya kuifurahia; unaishi katika baraka, lakini hutambui hilo. Hili linaonyesha kwamba umeandikiwa mateso! Wakati huu watu wengine hupinga, wengine huasi, wengine hufanya hili au lile. Mimi hukupuuza tu; usifikiri kwamba Sizifahamu shughuli hizo zenu. Je, Sifahamu kiini chenu? Mbona muendelee kwenda kinyume changu? Je, si kwa ajili yako mwenyewe ndio unafuatilia uzima na baraka? Je, si kwa ajili yako mwenyewe ndio una imani? Sasa hivi Nafanya tu kazi ya kushinda na maneno Yangu. Mara tu kazi hii ya kushinda ikihitimishwa, mwisho wako utakuwa dhahiri. Je, Nahitaji kujieleza wazi zaidi?
Kazi ya sasa ya kushinda ni kazi inayokusudiwa kuweka wazi hatima ya mwanadamu itakuwaje. Ni kwa nini Ninasema kuwa kuadibu na hukumu ni hukumu mbele ya kiti cha enzi kikubwa cheupe cha siku za mwisho? Hulioni hili? Ni kwa nini kazi ya kushinda ni hatua ya mwisho? Je, si kudhihirisha kwa usahihi hatima ya kila tabaka la wanadamu? Si kumruhusu kila mtu, katika harakati ya kazi ya kushinda ya kuadibu na hukumu, kuonyesha tabia zake halisi na kisha kuwekwa katika aina yake baadaye? Badala ya kusema kuwa huku ni kuwashinda wanadamu, inaweza bora kusema kuwa huku ni kuonyesha hatima ya kila aina ya mwanadamu. Yaani, huku ni kuhukumu dhambi zao halafu kuonyesha matabaka mbalimbali ya wanadamu, na kwa njia hiyo kubaini kama ni waovu au ni wenye haki. Baada ya kazi ya kushinda, kazi ya kutuza mazuri na kuadhibu maovu inafuata: watu wanaotii kabisa, yaani walioshindwa kabisa, watawekwa katika hatua nyingine ya kusambaza kazi ulimwenguni kote; wasioshindwa watawekwa gizani na watapatwa na majanga. Hivyo mwanadamu ataainishwa kulingana na aina yake, watenda maovu watawekwa pamoja na maovu, wasiuone mwangaza tena, na wenye haki watawekwa pamoja na mazuri, ili kupokea mwangaza na kuishi milele katika mwangaza. Mwisho wa vitu vyote u karibu, mwisho wa mwanadamu umebainishwa wazi machoni mwake, na vitu vyote vitaainishwa kulingana na aina yake. Ni vipi basi wanadamu wataepuka kuathiriwa na kuanisha huku? Kufichua mwisho kwa kila jamii ya mwanadamu kutafanywa hatima ya kila kitu ikikaribia, na kutafanywa wakati wa kazi ya kushinda ulimwengu mzima (ikiwemo kazi yote ya kushinda kuanzia kazi ya sasa). Huku kufichua mwisho wa wanadamu kunafanywa mbele ya kiti cha hukumu, katika harakati ya kuadibu, na harakati ya kazi ya kushinda ya siku za mwisho.
Kuwaainisha watu kwa kadri ya aina si kuwarudisha watu katika matabaka yao ya asili. Hii ni kwa sababu ulimwengu ulipoumbwa, kulikuwa tu na aina moja ya binadamu, kiume na wa kike. Hakukuwa na aina nyingi tofautitofauti. Ni baada tu ya miaka elfu kadhaa ya upotovu ndio matabaka mbalimbali ya binadamu yameibuka, mengine yakija chini ya miliki ya pepo wachafu, mengine chini ya miliki ya pepo waovu, na mengine, yanayofuatilia njia ya uzima, chini ya miliki ya Mwenyezi. Ni kwa njia hii tu ndio matabaka huibuka polepole miongoni mwa watu na ndio watu hujitenga katika matabaka ndani ya familia kubwa ya mwanadamu. Watu wote huja kuwa na "baba" tofauti; sio ukweli kwamba kila mtu yuko chini ya miliki ya Mwenyezi kabisa, kwa sababu uasi wa watu umezidi sana. Hukumu yenye haki hufichua nafsi ya kweli ya kila aina ya watu, bila kuacha chochote kikiwa kimefichika. Kila mtu huonyesha uso wake wa kweli katika nuru. Wakati huu, mwanadamu hayuko tena alivyokuwa mwanzoni na mfano wa asili wa mababu zake umepotea kitambo, kwa sababu vizazi visivyohesabika vya Adamu na Hawa vimenaswa na Shetani kwa muda mrefu, visijue tena jua la mbinguni, na kwa kuwa watu wamejazwa aina zote za sumu za Shetani. Hivyo, watu wana hatima zao za kufaa. Zaidi ya hayo, ni kwa msingi wa sumu zao zinazotofautiana ndio wanaainishwa kwa kadri ya aina, kumaanisha wanaainishwa kwa kiasi ambacho wanashindwa leo. Hatima ya mwanadamu si kitu kilichoamuliwa kabla tangu uumbaji wa dunia. Hii ni kwa sababu mwanzoni kulikuwa na jamii moja tu, ambayo kwa pamoja iliitwa “wanadamu,” na kwa sababu mwanadamu alikuwa bado hajapotoshwa na Shetani, na wanadamu wote waliishi katika mwangaza wa Mungu, bila giza kuwaandama. Lakini baada ya mwanadamu kupotoshwa na Shetani, kila jamii na aina ya watu walitapakaa ulimwenguni kote—kila jamii na aina ya watu waliotokana na ukoo mmoja ujulikanao kwa pamoja kama “wanadamu” uliojumuisha mwanamke na mwanamume. Wote walipotoshwa na mababu zao kutoka kwa nia za mababu zao wa kale sana—wanadamu waliojumuisha mwanamke na mwanamume (yaani, Adamu na Hawa wa asili, mababu zao wa kale sana). Wakati huo, watu wa pekee duniani walioongozwa na Yehova walikuwa Waisraeli. Watu wa aina mbalimbali walioibuka kutoka Israeli nzima (yaani kutoka ukoo wa asili) wakati ule walipoteza uongozi wa Mungu. Watu hawa wa mwanzo, wasiofahamu kabisa masuala ya ulimwengu wa wanadamu, walienda na mababu zao kuishi katika maeneo waliyodai kumiliki, mpaka wa leo. Hivyo hawatambui walipotoka vipi kutoka kwa Yehova na jinsi wamepotoshwa mpaka leo na aina yote ya pepo wachafu na roho waovu. Waliopotoshwa zaidi na kutiwa sumu mpaka leo hii, yaani ambao hatimaye hawawezi kukombolewa, hawatakuwa na budi ila tu kufuata mababu zao—pepo wachafu waliowapotosha. Wale wanaoweza kukombolewa hatimaye watakwenda hatima inayostahili wanadamu, yaani sehemu iliyotengwa kwa ajili ya waliokombolewa na walioshindwa. Kila kitu kitafanywa ili kukomboa wanaoweza kukombolewa, ila wale wasiosikia, watu wasioweza kutibika, chaguo lao pekee litakuwa kuwafuata mababu zao katika kuzimu ya kuadibu. Usidhani kuwa hatima yako iliamuliwa kabla tangu mwanzo na imefichuliwa tu sasa. Ikiwa unadhani hivyo, basi, umesahau kuwa katika uumbaji wa mwanzo wa wanadamu, hakukuumbwa jamii tofauti ya Shetani? Je, umesahau kuwa ni aina moja tu ya mwanadamu, yaani Adamu na Hawa, ndiyo iliumbwa (ikiwa na maana kwamba ni mwanamume na mwanamke tu ndio waliumbwa)? Ungalikuwa uzao wa Shetani kutoka mwanzo, je, hilo halingemaanisha kuwa Yehova alipomuumba mwanadamu Alijumuisha jamii ya Shetani? Je, Angefanya jambo kama hilo? Alimuumba mwanadamu kwa ajili ya ushuhuda Wake; Alimuumba mwanadamu kwa ajili ya utukufu Wake. Angeumbaje kwa makusudi jamii ya vizazi vya Shetani ili kumuasi kwa makusudi? Je, Yehova angeweza kufanya hili? Ikiwa hivyo, ni nani angeweza kusema kuwa Yeye ni Mungu Mwenye haki? Nikisema sasa kuwa baadhi yenu mwishowe mtaenda na Shetani, haimaanishi kuwa ulikuwa na Shetani toka mwanzo; ila, inamaanisha umejishusha chini sana hivi kwamba japo Mungu amejaribu kukukomboa, bado umekosa kuupata ukombozi huo. Hakuna budi ila kukuweka katika jamii moja na Shetani. Hii ni kwa sababu huwezi kukombolewa, si kwa sababu Mungu si mwenye haki kwako, yaani, si kwa sababu Mungu kimakusudi alipangia majaliwa yako kama mfano halisi wa Shetani na baadaye kukuweka katika jamii moja na Shetani na kutaka uteseke kwa makusudi. Huo si ukweli wa ndani wa kazi ya kushinda. Ikiwa unaamini hilo, basi ufahamu wako unaegemea upande mmoja sana! Hatua ya mwisho ya kushinda ni ya kukomboa watu na vilevile kufichua mwisho wa kila mtu. Inaweka wazi upotevu wa watu kupitia hukumu na kwa njia hiyo kuwafanya watubu, waamke, na kufuatilia uzima na njia ya haki ya maisha ya mwanadamu. Ni ya kuamsha mioyo ya waliolala na wapumbavu na kuonyesha, kwa njia ya hukumu, uasi wao wa ndani. Hata hivyo, ikiwa watu bado hawawezi kutubu, bado hawawezi kufuata njia ya haki ya maisha ya mwanadamu na hawawezi kuutupa upotovu huu, basi watakuwa vyombo visivyoweza kukombolewa vya kumezwa na Shetani. Hii ndiyo maana ya kushinda—kuwakomboa watu na vilevile kuwaonyesha mwisho wao. Mwisho mzuri, mwisho mbaya—yote yanafichuliwa na kazi ya kushinda. Kama watu watakombolewa au kulaaniwa yote yanafichuliwa wakati wa kazi ya kushinda.
Siku za mwisho ni wakati ambao vitu vyote vitaainishwa kulingana na aina zake kupitia kushinda. Kushinda ni kazi ya siku za mwisho; kwa maneno mengine, kuhukumu dhambi za kila mtu ni kazi ya siku za mwisho. La sivyo, watu wangeainishwa vipi? Kazi ya kuainisha inayofanywa miongoni mwenu ni mwanzo wa kazi ya aina hiyo ulimwenguni kote. Baada ya hii, watu wa kila mataifa vilevile watapitia kazi ya kushinda. Hii inamaanisha kuwa watu wote wataainishwa kimakundi na kufika mbele ya kiti cha hukumu kuhukumiwa. Hakuna mtu na hakuna kitu kitakachoepuka kupitia huku kuadibu na hukumu, na hakuna mtu au kitu kinaweza kukwepa uainishaji huu; kila mtu atawekwa katika jamii. Hii ni kwa sababu mwisho u karibu kwa vitu vyote na mbingu zote na dunia zimefikia hatima yake. Mwanadamu anawezaje kukwepa hatima ya maisha yake? Hivyo, mnaweza kuendelea na matendo yenu ya uasi kwa muda gani zaidi? Je, hamuoni kwamba siku zenu za mwisho ziko karibu sana? Ni vipi ambavyo wale wanaomcha Mungu na kutamani sana Aonekane watakosa kuona siku ya kuonekana kwa Mungu kwenye haki? Wanawezaje kukosa kupokea thawabu ya mwisho ya wema? Je, wewe ni yule atendaye mema, au yule atendaye maovu? Je, wewe ni yule akubaliye hukumu yenye haki na kisha kutii, au kisha hulaaniwa? Umekuwa ukiishi katika nuru mbele ya kiti cha hukumu, au katika giza jahanamu? Je, wewe mwenyewe si unayejua kwa dhahiri sana kama mwisho wako utakuwa wa thawabu au wa adhabu? Je, wewe si unayejua kwa dhahiri sana na kufahamu kwa kina sana kwamba Mungu ni mwenye haki? Kwa hiyo, kweli, mwenendo wako uko vipi na moyo wako uko wapi? Ninapoendelea kukushinda leo, unanihitaji Mimi kwa kweli kukueleza kinagaubaga kama mwenendo wako ni wa uovu au wa mema? Je, umeacha kiasi gani kwa ajili Yangu? Unaniabudu Mimi kwa kina gani? Wewe mwenyewe unajua kwa dhahiri sana ulivyo Kwangu—je, hiyo si kweli? Unapaswa kujua vizuri zaidi kuliko mtu yeyote jinsi utakavyokuwa hatimaye! Kweli Nakwambia, Niliwaumba tu wanadamu, na Nilikuumba wewe, lakini Sikuwakabidhi kwa Shetani; wala kuwafanya kwa makusudi muasi dhidi Yangu au kunipinga Mimi na kwa hivyo kuadhibiwa na Mimi. Hamjapata majanga haya kwa sababu mioyo yenu imekuwa migumu mno na mienendo yenu yenye kustahili dharau mno? Kwa hiyo si kweli kwamba mnaweza kuamua hatima yenu wenyewe? Je, si kweli kwamba mnajua ndani ya mioyo yenu, bora zaidi kuliko yeyote, vile mtaishia? Sababu ya Mimi kuwashinda watu ni kuwafichua, na pia kuhakikisha bora zaidi wokovu wako. Sio kukusababisha ufanye uovu au kwa makusudi kukusababisha uingie katika jahanamu ya uharibifu. Wakati utakapofika, mateso yako yote makuu, kulia kwako na kusaga meno—je, hayo yote hayatakuwa kwa ajili ya dhambi zako? Kwa hiyo, uzuri wako mwenyewe au uovu wako mwenyewe sio hukumu bora zaidi kukuhusu? Je, sio thibitisho bora zaidi ya kile ambacho mwisho wako utakuwa?
Sasa hivi Ninatumia kazi ya hawa watu walio Uchina kufichua tabia zao zote za uasi na kuufunua ubaya wao wote. Huu ndio usuli wa kusema kila Ninachotaka kusema. Baadaye Nitafanya hatua nyingine ya kazi ya kuushinda ulimwengu wote. Nitatumia hukumu Yangu kwenu kuhukumu udhalimu wa kila mtu duniani kote kwa sababu ninyi watu ndio wawakilishi wa waasi miongoni mwa wanadamu. Wasiojikakamua watakuwa foili[b] na vyombo vya kuhudumu tu, ila watakaojikakamua watatumika vizuri. Ni kwa nini Ninasema watakuwa foili[b] ? Ni kwa sababu maneno na kazi Yangu ya sasa vinalenga usuli wenu na kwa sababu mmekuwa wawakilishi na vielelezo vya uasi miongoni mwa wanadamu. Baadaye Nitapeleka maneno haya yanayowashinda kwa nchi za kigeni na kuyatumia kuwashinda watu wa huko, ila hutakuwa umeyafaidi. Je, hilo halitakufanya foili[b] ? Tabia potovu za wanadamu wote, matendo ya uasi ya mwanadamu, maumbile na sura mbaya za mwanadamu, zimeratibiwa zote katika maneno yanayotumiwa kuwashinda nyinyi. Baadaye Nitayatumia maneno haya kuwashinda watu wa kila taifa na kila dhehebu kwa sababu nyinyi ni mfano, kigezo. Hata hivyo, Sikupanga kuwaacha kwa makusudi; ukikosa kufanya vizuri katika utafutaji wako na kwa hivyo unathibitisha kuwa asiyeponyeka, hautakuwa tu chombo cha huduma na foili[b]? Wakati mmoja Nilisema kwamba hekima Yangu hutumiwa kutegemea njama za Shetani. Kwa nini Nilisema hilo? Je, huo si ukweli unaounga mkono Ninachosema na kufanya wakati huu? Kama huwezi kuchukua hatua, kama hujakamilishwa lakini badala yake unaadhibiwa, je, hutakuwa foili?[b] Labda umeteseka sana katika wakati wako, lakini sasa bado huelewi chochote; hujui kila kitu kuhusu uzima. Ingawa umeadhibiwa na kuhukumiwa, hujabadilika kamwe na ndani yako kabisa hujapata uzima. Wakati wa kutathmini kazi yako utakapofika, utapitia majaribio makali kama moto na hata majonzi makuu zaidi. Moto huu utageuza nafsi yako yote kuwa majivu. Kama mtu asiyekuwa na uzima, mtu asiye na aunsi ya dhahabu safi ndani yake, mtu ambaye bado amekatalia tabia potovu ya kale, na mtu asiyeweza hata kufanya kazi nzuri ya kuwa foili,[b] ni jinsi gani hutaweza kuondoshwa? Kazi ya kushinda ina faida gani kwa mtu aliye na thamani ya chini kuliko peni na asiyekuwa na uzima? Wakati huo ufikapo, siku zenu zitakuwa ngumu zaidi kuliko za Nuhu na Sodoma! Maombi yenu hayatawasaidia wakati huo. Mara tu kazi ya wokovu ikiisha, utaanzaje tena kutubu? Mara tu kazi ya wokovu itakuwa imefanywa, hakutakuwa tena na kazi ya wokovu. Kitakachokuwepo ni mwanzo wa kazi ya kuadhibu uovu. Wewe hupinga, huasi, na hufanya mambo unayojua ni maovu. Je, wewe sio shabaha ya adhabu kali? Ninakuelezea hili wazi leo. Ukichagua kutosikia, kisha maafa yakufike baadaye, je, hautakuwa umechelewa kama utaanza wakati huo tu kuhisi majuto na kuanza kuamini? Nakupa nafasi ya kutubu leo, lakini wewe hauko radhi kufanya hivyo. Unataka kungoja kwa muda gani? Mpaka siku ya kuadibu? Sikumbuki dhambi zako za zamani leo; Nakusamehe tena na tena, kugeuka kutoka upande wako mbaya kutazama tu upande wako mzuri, kwa sababu maneno na kazi Yangu yote ya sasa yanatakiwa kukuokoa wewe na sina nia mbaya kwako. Lakini unakataa kuingia; huwezi kutambua mema kutoka kwa mabaya na hujui namna ya kufurahia wema. Je, mtu wa aina hii hanuii tu kungoja ile adhabu na malipo yenye haki?
Musa alipougonga mwamba, na maji aliyokuwa Ameyatoa Yehova yakaruka, ilikuwa ni kwa sababu ya imani yake. Daudi alipocheza muziki wa sifa Kwangu, Yehova—moyo wake ukiwa umejaa furaha—ilikuwa ni kwa sababu ya imani yake. Ayubu alipowapoteza wanyama wake wote kote milimani, akapoteza mali yenye thamani kwa familia yake, na mwili wake kujawa na majipu, ilikuwa ni kwa sababu ya imani yake. Alipoweza kusikia sauti Yangu, Yehova, na kuuona utukufu Wangu, Yehova, ilikuwa ni kwa sababu ya imani yake. Kwamba Petro aliweza kumfuata Yesu Kristo, ilikuwa ni kwa imani yake. Kwamba Alitundikwa misumari msalabani kwa ajili Yangu na kutoa ushahidi mtukufu, pia ilikuwa kwa imani yake. Yohana alipoona mfano wa utukufu wa Mwana wa Adamu, ilikuwa kwa imani yake. Alipoona maono ya siku za mwisho, yote yalikuwa zaidi kwa sababu ya imani yake. Watu wanaojulikana kama wa taifa la Mataifa walipopokea ufunuo Wangu, wakijua kwamba Nimerudi katika mwili kufanya kazi Yangu miongoni mwa wanadamu, pia ni kwa sababu ya imani yao. Je, wale wote wanaogongwa na maneno Yangu makali na kuokolewa hawajafanya hivyo kwa sababu ya imani yao? Watu wamepokea vitu vingi sana kupitia imani. Kile ambacho wao hupokea sio baraka kila mara—kuhisi aina ya furaha na shangwe ambayo Daudi alihisi, au kuwa na maji yaliyotolewa na Yehova kama alivyofanya Musa. Kwa mfano, kuhusu Ayubu, alipokea baraka za Yehova na vilevile baa kupitia imani. Kama utapokea baraka au kupatwa na baa, yote ni matukio yaliyobarikiwa. Bila imani, hungeweza kupokea hii kazi ya kushinda, sembuse kuyaona matendo ya Yehova yanayoonyeshwa mbele ya macho yako leo. Hungeweza kuona, sembuse kuweza kupokea. Mabaa haya, maafa haya, na hukumu yote—kama haya hayangekufika, je, ungeweza kuona matendo ya Yehova leo? Leo hii ni imani inayokuruhusu kushindwa, na kushindwa ndiko kunakufanya uamini kila tendo la Yehova. Ni kwa sababu tu ya imani unapokea kuadibu na hukumu ya aina hii. Kupitia kuadibu na hukumu hizi, umeshindwa na kukamilishwa. Bila aina hii ya kuadibu na hukumu upokeayo leo hii, imani yako ingekuwa bure. Kwa sababu humtambui Mungu, haijalishi unamwamini kiasi gani, imani yako bado itakuwa maonyesho matupu yasiyokuwa na misingi katika uhalisi. Ni baada tu ya kupokea aina hii ya kazi ya kushinda inayokufanya mtiifu kabisa ndipo imani yako inakuwa kweli na inayotegemewa na roho yako kumrudia Mungu. Japo umehukumiwa na kulaaniwa sana kwa sababu ya hili neno “imani,” una imani ya kweli, na unapokea kitu cha kweli zaidi, halisi zaidi, na chenye thamani zaidi. Hii ni kwa sababu ni katika harakati ya hukumu tu ndipo unaona hatima ya viumbe wa Mungu; ni katika hukumu hii ndio unapata kuona kuwa Muumba anapaswa kupendwa; ni katika kazi kama hiyo ya kushinda ndio unapata kuona mkono wa Mungu; ni katika kushinda huku unapata kutambua kwa ukamilifu maisha ya mwanadamu; ni katika kushinda huku unapata kujua njia ya haki ya maisha ya mwanadamu na kufahamu maana ya kweli ya “mwanadamu”; ni kupitia tu huku kushinda ndiko unaweza kuona tabia ya haki ya mwenye Uweza na uso Wake mzuri na mtukufu. Ni katika kazi hii ya kushinda ndiko unaweza kujifunza kuhusu asili ya mwanadamu na kufahamu “historia isiyokufa” ya mwanadamu; ni katika kushinda huku ndiko unapata kufahamu mababu za wanadamu na asili ya upotovu wa mwanadamu; ni katika kushinda huku ndio unapokea furaha na starehe pamoja na kuadibu, nidhamu, na maneno ya kuonya kutoka kwa Muumba kwa wanadamu ambao Aliwaumba; katika kazi hii ya kushinda, ndipo unapokea baraka na majanga ambayo mwanadamu anapaswa kupokea… je, haya yote si kwa ajili ya hiyo imani yako ndogo? Je, baada ya kuvipata vitu hivi vyote imani yako haijakua? Hujapata kiwango kikubwa ajabu? Hujasikia tu maneno ya Mungu na kuona hekima ya Mungu, lakini wewe binafsi umepitia pia kila hatua ya kazi. Labda utasema kuwa usingekuwa na imani, basi usingepata aina hii ya kuadibu au aina hii ya hukumu. Ila unapaswa kufahamu kuwa bila imani, usingeweza tu kupokea aina hii ya kuadibu na ulinzi kutoka kwa mwenye Uweza, bali pia daima ungepoteza fursa ya kumwona Muumba. Usingejua asili ya wanadamu na kufahamu umuhimu wa maisha ya mwanadamu. Japo mwili wako utakufa na roho yako kuondoka, bado hutayafahamu matendo yote ya Muumba. Aidha hutafahamu kuwa Muumba alifanya kazi kubwa kiasi hicho duniani baada ya kuwaumba wanadamu. Kama mmojawapo wa hawa wanadamu Aliowaumba, je, uko tayari kutumbukia gizani kiasi hiki bila fahamu na kukumbana na adhabu ya milele? Ukijitenga na kuadibu na hukumu ya sasa, utapatana na kitu gani? Je, unafikiri ukishajitenga na hukumu ya sasa, utaweza kuepukana na haya maisha magumu? Je, si kweli kwamba ukiondoka “mahala hapa,” utakachokipata ni mateso machungu au majeraha kutoka kwa ibilisi? Je, waweza kukumbana na mchana na usiku zisizostahimilika? Je, unafikiri kwamba kwa kuepuka hukumu leo, unaweza kukwepa milele yale mateso ya siku zijazo? Ni kitu gani kitakukumba? Inaweza kuwa paradiso ya duniani unayoitarajia? Unafikiri unaweza kuepuka kuadibu kwa milele kwa baadaye kwa kuukimbia uhalisi kama ufanyavyo? Baada ya leo, je, utawahi kuweza kuipata fursa na baraka kama hii tena? Je, utapata fursa na baraka utakapokuwa umekumbwa na misukosuko? Je, utapata fursa na baraka wanadamu wote waingiapo katika pumziko? Maisha yako ya furaha ya sasa na hiyo familia yako ndogo yenye amani—vyaweza kuwa kibadala cha hatima yako? Iwapo una imani ya kweli, na iwapo unafaidi pakubwa kwa sababu ya imani yako, basi hayo yote ndiyo—wewe kiumbe—unapaswa kufaidi na vilevile kile ambacho ulipaswa kuwa nacho. Aina hii ya kushinda ndiyo ya faida zaidi kwa imani na maisha yako.
Kwa sasa unahitaji kufahamu kile anachotaka Mungu kwa wale wanaoshindwa, mtazamo Wake ni upi kwa wale wanaokamilishwa, na kile unachopaswa kuingia ndani mara moja. Mambo mengine unahitaji tu kuelewa kidogo. Mahubiri mengine kuhusu mafumbo huhitaji kujisumbua kuyaelewa. Si ya usaidizi sana kwa maisha, na inatosha tu kuyaangalia. Kwa mfano, mafumbo kama yale yanayohusu Adamu na Hawa unahitaji kuyaangalia. Kile ambacho Adamu na Hawa walikuwa wanalenga zama hizo na kazi gani inahitaji kufanywa leo—haya unahitaji kujua kuyahusu.[a] Unahitaji kuelewa kwamba katika kushinda na kumkamilisha mwanadamu, Mungu anataka kumrudisha mwanadamu vile Adamu na Hawa walikuwa. Jinsi gani mtu lazima awe mkamilifu ili kufikia kiwango cha Mungu—unapaswa kufahamu vizuri hilo na kutaka kulifikia kabisa. Hilo linahusu utendaji wako na ni jambo unalopaswa kuelewa. Unahitaji tu kutafuta kuingia kwa kadri ya maneno yanayohusu mambo haya. Unaposoma kwamba "historia ya maendeleo ya wanadamu inarudi nyuma makumi ya maelfu ya miaka, unadadisi, na kwa hiyo unajaribu kuielewa pamoja na ndugu. "Mungu asema maendeleo ya wanadamu yanarudi nyuma miaka elfu sita, sawa? Ni nini hiki kuhusu makumi ya maelfu ya miaka?" Kuna maana gani ya kujaribu kulielewa hili? Kama Mungu Mwenyewe amekuwa akifanya kazi kwa makumi ya maelfu ya miaka au mamia ya mamilioni ya miaka—je, Anakuhitaji uelewa hili? Hili si jambo ambalo wewe kama mtu aliyeumbwa anahitaji kujua kukihusu. Unaweza tu kuangalia aina hii ya mazungumzo; usijaribu kuyaelewa kama maono. Kile unachohitaji kujua kukihusu ni kile unachopaswa kuingia ndani na kupata uwazi sasa hivi. Tafakari na uelewe kuhusu haya. Ni wakati huo tu ndipo utapata kushindwa. Baada ya kusoma yaliyo hapo juu, huenda ukawa na athari ya kawaida: Mungu amejawa na hamu. Anataka kutushinda na kupata utukufu na ushuhuda. Tunapaswa kushirikiana vipi na Yeye? Lazima tufanye nini ili tuweze kushindwa kabisa na Yeye na kuwa ushuhuda Wake? Lazima tufanye nini kumwezesha Mungu kupata utukufu? Lazima tufanye nini ili kuturuhusu wenyewe kuishi chini ya miliki ya Mungu na si chini ya miliki ya Shetani? Hili ndilo watu wanapasa kufikiria kulihusu. Kila mmoja wenu anapaswa kuelewa umuhimu wa kushinda. Hilo ni jukumu lenu. Ni baada tu ya kupata uwazi huu ndio mtapata kuingia, mtajua hatua hii ya kazi, na mtakuwa watiifu kabisa. La sivyo, hamtatimiza utiifu wa kweli.
Tanbihi:
a. Maandishi ya asili yanaacha "haya unahitaji kujua kuyahusu."
b. Foili. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.
kutoka kwa Neno Laonekana katika Mwili
Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni