Jumanne, 7 Novemba 2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mungu, ukweli

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II

Kwenye mkutano wetu wa mwisho tuliweza kuzungumzia mada muhimu sana. Je, wakumbuka mada hiyo ilikuwa kuhusu nini? Hebu Niirudie. Mada ya ushirika wetu wa mwisho ilikuwa: Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe. Je, mada hii ni muhimu kwako? Ni sehemu gani katika mada hii ni muhimu kwako?
Kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, au Mungu Mwenyewe? Ni sehemu ipi inakuvutia zaidi? Ni sehemu ipi unayotaka kusikiliza kuhusu zaidi? Najua ni vigumu kwako wewe kulijibu swali hilo, kwa sababu tabia ya Mungu inaweza kuonekana katika kila kipengele cha kazi Yake, na tabia Yake inafichuliwa katika kazi Yake siku zote na pahali pote, na, kutokana na hayo, inawakilisha Mungu Mwenyewe; kwenye mpango wa usimamizi wa ujumla wa Mungu, kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe vyote hivi haviwezi kutenganishwa.
Maudhui ya ushirika wetu wa mwisho kuhusu kazi ya Mungu yaliweza kuangazia mambo yaliyofanyika kitambo kwenye Biblia. Maudhui hayo yote yalikuwa hadithi kuhusu binadamu na Mungu, na yalimfanyikia binadamu na wakati huohuo yakahusisha kushiriki na maonyesho ya Mungu, hivyo basi hadithi hizi zinashikilia thamani na umuhimu mkubwa katika kujua Mungu. Baada tu ya kuumba ubinadamu, Mungu Alianza kujihusisha na binadamu na kuzungumza na binadamu, na tabia yake ikaanza kuonyeshwa kwa binadamu. Kwa maneno mengine, tangu Mungu alipojihusisha kwanza na mwanadamu, Alianza kuujuza umma kuhusu binadamu, bila kusita, kiini Chake halisi na kile Anacho na alicho. Licha ya kama watu wa awali au watu wa leo wanaweza kuona au kuelewa kiini hicho, kwa ufupi Mungu anamzungumzia mwanadamu na kufanya kazi miongoni mwa binadamu, Akifichua tabia Yake na Akionyesha kiini Chake —jambo ambalo ni ukweli, na lisilopingika na mtu yeyote. Hii inamaanisha pia kwamba tabia ya Mungu, kiini cha Mungu, na kile Anacho na alicho vyote vinatolewa daima na kufichuliwa huku naye Akifanya kazi na kujihusisha na binadamu. Hajawahi kusetiri au kumfichia binadamu chochote, lakini badala yake anatangaza kwa umma na kuachilia tabia Yake binafsi bila ya kuficha chochote. Hivyo basi, Mungu anatumai kwamba binadamu anaweza kumjua Yeye na kuielewa tabia Yake na kiini chake. Hapendi binadamu kuchukulia tabia Yake na kiini Chake kuwa mafumbo ya milele, wala Hataki mwanadamu kumchukulia Mungu kama fumbo lisiloweza kutatuliwa. Mpaka tu pale ambapo mwanadamu atakapomjua Mungu ndipo binadamu atakapojua njia ya kufuata na kuweza kuukubali mwongozo wa Mungu, na mwanadamu tu kama huyu ndiye anayeweza kuishi kwa kweli katika utawala wa Mungu, na kuishi katika mwangaza, na kuishi katikati ya baraka za Mungu.
Maneno na tabia iliyowasilishwa mbele na kufichuliwa na Mungu inawakilisha mapenzi Yake, na pia inawakilisha kiini Chake halisi. Wakati Mungu anapojihusisha na binadamu, haijalishi ni nini Anachosema au kufanya, au tabia gani Anayofichua, na haijalishi ni nini binadamu anaona kuhusu kiini cha Mungu na kile Anacho na alicho, vyote vinawasilisha mapenzi ya Mungu kwa binadamu. Licha ya kiwango ambacho binadamu anaweza kutambua, kufahamu, au kuelewa, vyote hivi vinawakilisha mapenzi ya Mungu—mapenzi ya Mungu kwa binadamu. Hii ni zaidi ya shaka! Mapenzi ya Mungu kwa binadamu ni vile Anavyohitaji watu kuwa, kile Anachohitaji wao kufanya, namna Anavyohitaji wao kuishi, na vile Anavyowahitaji kuweza kukamilisha kutimia kwa mapenzi ya Mungu. Je, mambo haya hayawezi kutenganishwa na kiini cha Mungu? Kwa maneno mengine, Mungu huwasilisha mbele tabia Yake na vyote Alivyo navyo na kile ambacho Mungu ni wakati huohuo Akimtolea madai binadamu. Hakuna uongo, hakuna kusingizia, hakuna ufichaji, na wala hakuna kupiga chuku. Ilhali kwa nini binadamu hawezi kujua na kwa nini hajawahi kuweza kutambua waziwazi tabia ya Mungu? Na kwa nini hajawahi kutambua mapenzi ya Mungu? Kile ambacho kimefichuliwa na kuwasilishwa mbele na Mungu ndicho kile Mungu anacho Mwenyewe na maana yake , na kinaonyesha kila kipengele cha tabia Yake ya kweli—hivyo kwa nini binadamu hawezi kuona? Kwa nini binadamu hana uwezo wa kuwa na maarifa ya kina? Kunayo sababu muhimu ya haya. Na sababu yenyewe ni ipi? Tangu wakati wa uumbaji, binadamu hajawahi kumchukulia Mungu kama Mungu. Kwenye nyakati zile za mwanzo kabisa, haikujalisha ni nini Mungu alifanya kuhusiana na binadamu, yule binadamu ambaye ndiye tu alikuwa ameumbwa, binadamu alimchukulia yeye kuwa mwandani wake tu na wala si zaidi ya hapo, kama mtu wa kutegemewa, na hakuwa na maarifa yoyote wala uelewa wa Mungu. Hivi ni kusema, hakujua kwamba kile kilichowasilishwa mbele na Kiumbe huyu—Kiumbe huyu ambaye yeye alitegemea na kumwona kuwa mwandani wake—alikuwa kiini cha Mungu, na wala hakujua kwamba Kiumbe huyu ndiye anayetawala viumbe wote. Nikisema kwa urahisi, watu wa wakati huo hawakuwa na maarifa hata kidogo kumhusu Mungu. Hawakujua kwamba mbingu na nchi na mambo yote yalikuwa yameumbwa na Yeye na wala hawakujua ni wapi Alipotokea, na, zaidi hawakujua Yeye Alikuwa nani. Bila shaka, wakati huo Mungu hakumhitaji binadamu kumjua Yeye au kumfahamu Yeye au kuelewa kila kitu Alichofanya, au kufahamishwa kuhusu mapenzi Yake, kwani hizi zilikuwa nyakati za mapema zaidi baada ya uumbwaji wa mwanadamu. Wakati Mungu alipoanza matayarisho ya kazi ya Enzi ya Sheria, Mungu alifanya mambo fulani kwa binadamu na pia Akaanza kutolea binadamu madai fulani, Akimwambia namna ya kutolea Mungu sadaka na namna ya kumwabudu. Ni wakati huo ndipo binadamu alipopata mawazo machache mepesi kuhusu Mungu, ni hapo tu ndipo alipojua tofauti kati ya binadamu na Mungu na kwamba Mungu Ndiye aliyewaumba wanadamu. Wakati binadamu alipojua kwamba Mungu alikuwa Mungu na binadamu alikuwa binadamu kukawa umbali fulani kati ya Yeye na Mungu , bado Mungu hakuhitaji kwamba binadamu awe na maarifa makuu au uelewa wa kina kumhusu Yeye. Hivyo basi, Mungu anayatoa mahitaji tofauti kwa binadamu kutokana na awamu na hali za kazi Yake. Unaona nini katika haya? Ni kipengele kipi cha tabia ya Mungu unayoitambua? Je, Mungu ni wa kweli? Yale mahitaji ambayo Mungu anampa binadamu yanastahili? Kwenye nyakati za mapema kabisa kufuatia uumbaji wa wanadamu na Mungu, wakati ambao Mungu alikuwa bado hajatekeleza kazi ya ushindi na utimilifu wa binadamu, na Alikuwa hata bado hajaongea yale maneno mengi sana kwake, Alihitaji kidogo sana kutoka kwa binadamu. Licha ya kile ambacho binadamu alifanya na namna alivyotenda—hata kama alifanya mambo fulani yaliyomkosea Mungu—Mungu alimsamehe hayo yote, na akayapuuza. Kwa sababu Mungu Alijua kile Alichokuwa Amempa binadamu, na Alijua kile kilichokuwa ndani ya binadamu, basi Alijua kiwango cha mahitaji ambayo anafaa kudai kutoka kwa binadamu. Ingawaje kiwango cha mahitaji Yake kilikuwa cha chini sana wakati huo, hii haimaanishi kwamba tabia Yake haikuwa kuu, au kwamba hekima na uweza Wake yalikuwa si yoyote ila maneno matupu. Kwa binadamu, kunayo njia moja tu ya kujua tabia ya Mungu na Mungu Mwenyewe: kwa kufuata hatua za kazi ya usimamizi ya Mungu na wokovu wa mwanadamu, na kuyakubali maneno ambayo Mungu anaongea akiyaelekeza kwa mwanadamu. Kujua kile Mungu anacho na alicho, na kujua tabia ya Mungu, bado binadamu angemuuliza Mungu kumwonyesha ubinafsi Wake halisi? Binadamu hatafanya hivyo, na hathubutu kufanya hivyo, kwa kuweza kuifahamu tabia ya Mungu na kile Anacho na alicho, tayari binadamu atakuwa amemwona Mungu Mwenyewe wa kweli, na atakuwa tayari ameona ubinafsi Wake halisi. Haya ndiyo matokeo yasiyoepukika.
Kazi na mpango wa Mungu ulipokuwa ukiendelea mbele bila kusia, na baada ya Mungu kuanzisha agano la upinde wa mvua na binadamu kama ishara kwamba Hangewahi tena kuuangamiza ulimwengu kwa kutumia gharika, Mungu alikuwa na tamanio lililokuwa likiongezeka na kumsukuma kuwapata wale ambao wangeweza kuwa katika akili moja na Yeye. Hivyo, pia, Alikuwa na tamanio lenye udharura zaidi wa kupata wale waliokuwa na uwezo wa kutekeleza mapenzi Yake duniani, na, isitoshe, kupata kundi la watu ambao wangeweza kuwa huru dhidi ya nguvu za giza, na kutoweza kuwa watumwa wa Shetani, na kuweza kuwa na ushuhuda kwake Yeye duniani. Kupata kundi la watu kama hawa kulikuwa ni tamanio la Mungu kwa muda mrefu, Alichokuwa akisubiria tangu wakati wa uumbaji. Hivyo basi, licha ya matumizi ya gharika na Mungu ili kuuangamiza ulimwengu, au agano Lake na binadamu, mapenzi ya Mungu, hali yake ya akili, mpango, na matumaini yote yalibakia yaleyale. Kile Alichotaka kufanya, ambacho Alikuwa ametamani kwa muda mrefu kabla ya uumbaji, kilikuwa kupata wale walio miongoni mwa wanadamu ambao Alitamani kuwapata—Kupata watu wa kundi hili ambao walioweza kufahamu na kujua tabia Yake, na kuyaelewa mapenzi Yake, kundi ambalo lingeweza kumwabudu Yeye. Watu kwenye kundi kama hili wanaweza kweli kuwa na ushuhuda kwake, na wao ndio, yaweza kusemekana, wasiri Wake.
Leo, hebu tuendelee kuzifuata nyayo za Mungu na kufuata nyayo za kazi Yake, ili tuweze kufichua fikira na mawazo ya Mungu, na kila kitu kinachomhusu Mungu, vyote ambavyo “vimehifadhiwa kwenye ghala” kwa muda mrefu. Kupitia mambo haya tutajua hatimaye tabia ya Mungu, kukielewa kiini cha Mungu, tutamruhusu Mungu kuingia kwenye mioyo yetu, na kila mmoja wetu ataweza kukaribia Mungu kwa utaratibu, na kupunguza umbali wetu na Mungu.
Sehemu ya kile tulichozungumzia wakati wa mwisho ilihusiana na kwa nini Mungu alianzisha agano na binadamu. Wakati huu, tutakuwa na ushirika kuhusu vifungo vya maandiko zilizo hapa chini. Hebu tuanze kwa kuyasoma maandiko.
Ibrahimu
1. Mungu Amwahidi Ibrahimu Mwana
(Mwa 17:15-17) Mungu akamwambia Abrahamu, na Sarai mkeo, hutamwita jina lake Sarai, kwa kuwa jina lake litakuwa Sara. Nami nitambariki, na pia nitakupa mwana kutoka kwake: naam, Nitambariki, na yeye atakuwa mama wa mataifa; na wafalme wa za watu watatoka kwake. Kisha Abrahamu akaanguka kifudifudi, akacheka, akasema moyoni, Je, mtoto atazaliwa kwa mtu wa umri aliye na miaka mia moja? Na Sara, aliye na umri wa miaka tisini, atazaa?
(Mwa 17:21-22) Lakini agano langu Nitalifanya imara na Isaka, ambaye Sara atakuzalia wakati kama huu mwaka ujao. Na akaacha kuzungumza naye, na Mungu akapanda kutoka kwa Ibrahimu.
2. Ibrahimu Amtoa Isaka
(Mwa 22:2-3) Naye akasema, Umchukue mwanao, mwanao wa pekee, umpendaye, Isaka, uende mpaka nchi ya Moria; na huko umtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo Nitakaokuambia. Abrahamu akaondoka alfajiri, akatandika punda wake, akachukua vijana wawili pamoja naye, na Isaka mwanawe, akachanja kuni kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa, akaondoka, akaenda hadi mahali alipoambiwa na Mungu.
(Mwa 22:9-10) Wakafika mahali pale alipoambiwa na Mungu; Abrahamu akajenga madhabahu huko, akazipanga kuni tayari, na akamfunga Isaka mwanawe, na akamweka juu ya madhabahu juu ya zile kuni. Abrahamu akanyosha mkono wake, akakichukua kisu ili amchinje mwanawe.

Hakuna Awezaye Kuzuia Kazi Ambayo Mungu Anaamua Kufanya

Hivyo, nyote muda mfupi uliopita mmesikia hadithi ya Ibrahimu. Alichaguliwa na Mungu baada ya gharika kuuangamiza ulimwengu, jina lake lilikuwa Ibrahimu, na alipokuwa na miaka mia moja, na mke wake Sara akiwa na umri wa miaka tisini, ahadi ya Mungu ilimjia. Mungu alimwahidi nini? Mungu alimwahidi kile ambacho kinarejelewa katika Maandiko: “Nami Nitambariki, na pia nitakupa mwana kutoka kwake.” Ni maelezo yapi yalitangulia ahadi ya Mungu ya kumpa mtoto? Maandiko yanaelezea yafuatayo: “Kisha Abrahamu akaanguka kifudifudi, akacheka, akasema moyoni, Je, mtoto atazaliwa kwa mtu wa umri aliye na miaka mia moja? Na Sara, aliye na umri wa miaka tisini, atazaa?” Kwa maneno mengine wanandoa hawa wazee walikuwa na umri mwingi sana wa kupata watoto. Naye Ibrahimu alifanya nini baada ya Mungu Kumwahidi? Aliuangukia uso wake akicheka, na kujiambia, “Je, mtoto atazaliwa kwa mtu wa umri aliye na miaka mia moja?” Ibrahimu aliamini kwamba haikuwezekana—hivi alimaanisha kwamba alisadiki ahadi ya Mungu kwake haikuwa chochote ila mzaha. Kutoka mtazamo wa binadamu, ahadi isingeweza kutimizika na binadamu, na vilevile isingeweza kutimizika na Mungu na ilikuwa haiwezekani kwa Mungu. Pengine, kwa Ibrahimu, ahadi hii ilikuwa ya kuchekesha. Mungu alimuumba binadamu, lakini yaonekana kwamba hajui kwamba mtu aliyezeeka sana hawezi kupata watoto; Anafikiria kwamba Anaweza kuniruhusu kupata mtoto, Anasema kwamba atanipa mtoto—kwa kweli hilo haliwezekani!. Na hivyo, Ibrahimu akaangukia uso wake na kucheka, akijifikiria yeye mwenyewe: Haiwezekani—Mungu anafanya mzaha na mimi, hili haliwezi kuwa kweli. Hakutilia maanani maneno yake Mungu. Hivyo, katika macho ya Mungu, Ibrahimu alikuwa binadamu wa aina gani? (Mwenye haki) Ni wapi ulipojifunza kwamba alikuwa mwenye haki? Wewe unafikiria kwamba wale wote ambao Mungu anawaita ni wenye haki, na watimilifu, na watu wanaotembea na Mungu. Wewe unashikilia mafundisho ya dini! Lazima uone waziwazi kwamba wakati Mungu anapomfasili mtu, Hafanyi hivyo kiholela. Hapa, Mungu hakusema kwamba Ibrahimu alikuwa mwenye haki. Katika moyo Wake, Mungu anavyo viwango vya kupima kila mtu. Ingawaje Mungu hakusema ni mtu wa aina gani ambaye Ibrahamu alikuwa, kwa mujibu wa mwenendo wake, Ibrahimu alikuwa na imani ya aina gani kwake Mungu? Ilikuwa ya kidhahania kidogo? Au alikuwa mwenye imani kuu? La, hakuwa! Kicheko na fikira zake zilionyesha yeye alikuwa nani, hivyo imani yako kwamba alikuwa mwenye haki ni ndoto ya kufikiria kwako, ni matumizi yasiyo na mwelekeo ya mafundisho ya dini, usiopaswa. Je, Mungu alikiona kicheko cha Ibrahimu na maonyesho yake madogo, [a] Alijua kuyahusu? Mungu alijua. Lakini Mungu angebadilisha kile Alichokuwa ameamua kufanya? La! Wakati Mungu alipopangilia na kuamua kwamba Angemchagua binadamu huyu, suala hilo lilikuwa tayari limekamilishwa. Si fikira za binadamu wala mwenendo wake ungemshawishi au kuhitilafiana na Mungu hata chembe; Mungu Asingebadilisha kiholela mpango Wake, wala Asingebadilisha au kuharibu mpango Wake kwa sababu ya mwenendo wa binadamu, hali ambayo ingekuwa ujinga. Nini, basi, kimeandikwa katika Mwanzo 17:21-22? “Lakini agano langu Nitalifanya imara na Isaka, ambaye Sara atakuzalia wakati kama huu mwaka ujao. Na akaacha kuzungumza naye, na Mungu akapanda kutoka kwa Ibrahimu.” Mungu hakutilia maanani hata chembe kile Ibrahimu alichofikiria au kusema. Na sababu ya kutotilia maanani Kwake ni gani? Kutotilia maanani kwake kulikuwa kwa sababu, wakati huo Mungu hakuhitaji kwamba mwanadamu awe mwenye imani kuu au kwamba aweze kuwa na maarifa kuu kuhusu Mungu, au, vilevile, aweze kuelewa kile kilichofanywa na kusemwa na Mungu. Hivyo, hakuhitaji kwamba binadamu aelewe kabisa kile Alichoamua kufanya, au watu Alioamua kuchagua, au kanuni za vitendo Vyake, kwani kimo cha binadamu hakikutosha tu. Wakati huo, Mungu alichukulia kile ambacho Ibrahimu alifanya na vyovyote alivyojiendesha yeye mwenyewe kuwa kawaida. Hakushutumu, au kukemea, lakini alisema tu: “Sara atakuzalia Isaka wakati huu uliopangwa mwaka ujao.” Kwa Mungu, baada Yake kuyatangaza maneno haya, suala hili hatimaye lilikuwa kweli hatua kwa hatua; katika macho ya Mungu, kile ambacho kilikuwa kikamilishwe na mpango Wake kilikuwa tayari kimetimizwa. Baada ya kuikamilisha mipangilio ya hayo, Mungu aliondoka. Kile binadamu hufanya au kufikiria, kile binadamu huelewa, mipango ya binadamu—hakuna chochote kati ya hivi vyote kinacho uhusiano wowote na Mungu. Kila kitu hufanyika kulingana na mpango wa Mungu, kikiendana na nyakati na awamu zilizowekwa na Mungu. Hivyo ndivyo kanuni ya kazi ya Mungu inavyoenda. Mungu haingilii kati chochote kile binadamu anafikiria au kujua, ilhali Haachi mpango Wake, wala kuacha kazi Yake kwa sababu binadamu hasadiki wala kuelewa. Kweli hizi hivyo basi zinakamilishwa kulingana na mpango na fikira za Mungu. Hivi ndivyo hasa tunavyoona kwenye Biblia: Mungu Alisababisha Isaka kuzaliwa wakati ule Aliokuwa amepanga. Je, kweli zinathibitisha kwamba tabia na mwenendo wa binadamu vilizuia kazi ya Mungu? Havikuzuia kazi ya Mungu! Je, imani ndogo ya binadamu kwa Mungu, na dhana zake na fikira kumhusu Mungu viliweza kuathiri kazi ya Mungu? La, havikuathiri! Hata kidogo! Mpango wa usimamizi wa Mungu hauathiriwi na binadamu, suala, au mazingira yoyote. Kila kitu Anachoamua kufanya kitakamilika na kukamilishwa kwa wakati na kulingana na mpango Wake, na kazi Yake haiwezi kutatizwa na binadamu yeyote. Mungu hatilii maanani baadhi ya ujinga na kutojua kwa binadamu, na hata Hupuuza upinzani na dhana fulani za binadamu Kwake; badala yake, Anafanya kazi ambayo lazima Afanye bila ya kusita. Hii ni tabia ya Mungu na ni onyesho la kudura Yake.

Kazi ya Usimamizi wa Mungu na Wokovu wa Mwanadamu Yaanza kwa Sadaka ya Isaka ilivyotolewa na Ibrahimu

Baada ya kumpa mtoto Ibrahimu, maneno ambayo Mungu alikuwa ametamka kwa Ibrahimu yakawa yametimizwa. Hii haimaanishi kwamba mpango wa Mungu ulifikia mwisho hapa; kinyume cha mambo ni kwamba, mpango wa ajabu wa Mungu wa usimamizi na wokovu wa mwanadamu ndipo ulikuwa tu umeanza, na baraka Yake ya mwana kwa Ibrahimu ilikuwa tu ni utangulizi wa mpango wa usimamizi Wake kwa ujumla. Wakati huo, ni nani aliyejua kwamba vita vya Mungu na Shetani vilikuwa vimeanza kimya kimya wakati Ibrahimu alipomtoa Isaka?

Mungu Hajali Kama Binadamu Ni Mjinga—Anahitaji Tu Binadamu Awe Mkweli

Kisha, hebu tuangalie kile Mungu alimfanyia Ibrahimu. Ukiangalia Mwanzo 22:2, Mungu alimtolea Ibrahimu amri ifuatayo: “Naye akasema, Umchukue mwanao, mwanao wa pekee, umpendaye, Isaka, uende mpaka nchi ya Moria; na huko umtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo Nitakaokuambia.” Maana ya Mungu ilikuwa wazi: Alikuwa akimwambia Ibrahimu amtoe mtoto wake wa pekee Isaka, ambaye alimpenda, kwa minajili ya sadaka ya kuteketezwa. Tukiiangalia amri ya Mungu leo, je ingali inakinzana na dhana za binadamu? Ndiyo! Kile alichokifanya Mungu wakati huo ni kinyume sana na dhana za binadamu na hakieleweki kwa binadamu. Katika dhana zao, watu husadiki yafuatayo: Wakati binadamu hakusadiki, na akafikiria ni jambo lisilowezekana, Mungu Alimpa mwana, na baada ya kupata mtoto, Mungu alimwomba amtoe mwana wake—haiwezekani! Mungu kwa hakika alinuia kufanya nini? Kusudio halisi la Mungu lilikuwa nini? Alimpa Ibrahimu mtoto bila masharti yoyote, ilhali pia Alimwomba Ibrahimu aweze kutoa bila masharti. Maji yalikuwa yamezidi unga? Katika mtazamo wa mtu wa pembeni, hapa maji hayakuwa tu yamezidi unga lakini pia ilikuwa kwa kiasi fulani hali ya “kuunda tatizo pasipo na tatizo” Lakini Ibrahimu mwenyewe hakusadiki kwamba Mungu alikuwa akihitaji mengi sana. Ingawaje alikuwa na wasiwasi fulani, na alimshuku kidogo Mungu, alikuwa tayari bado kumtoa mtoto wake. Wakati huu, ni nini unachoona ambacho kinathibitisha kuwa Ibrahimu alikuwa radhi kumtoa mtoto wake? Ni nini kinazungumzwa kwenye sentensi hizi? Maandishi asilia yanaelezea yafuatayo: “Abrahamu akaondoka alfajiri, akatandika punda wake, akachukua vijana wawili pamoja naye, na Isaka mwanawe, akachanja kuni kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa, akaondoka, akaenda hadi mahali alipoambiwa na Mungu.” (Mwa 22:3). “Wakafika mahali pale alipoambiwa na Mungu; Abrahamu akajenga madhabahu huko, akazipanga kuni tayari, na akamfunga Isaka mwanawe, na akamweka juu ya madhabahu juu ya zile kuni. Abrahamu akanyosha mkono wake, akakichukua kisu ili amchinje mwanawe.” (Mwa 22:9-10). Wakati Ibrahimu alipounyosha mkono wake, na kukichukua kisu ili kumwua mtoto wake, Mungu aliviona vitendo vyake? Naam aliviona. Mchakato wote—kuanzia mwanzo, wakati Mungu alipomwomba Ibrahimu kumtoa Isaka, hadi pale ambapo Ibrahimu alikiinua kisu chake ili kumwua mtoto wake—hilo lilionyesha Mungu moyo wa Ibrahimu, na haijalishi kuhusu ujinga wake wa awali, kutojua kwake, na kutomwelewa Mungu kwake, wakati huo moyo wa Ibrahimu kwa Mungu ulikuwa kweli, na wenye uaminifu, na kwa kweli alikuwa akienda kumrudisha Isaka, mtoto aliyepewa yeye na Mungu, ili arudi kwa Mungu. Ndani yake, Mungu aliuona utiifu—utiifu uleule ambao Yeye Alitamani.
Kwa binadamu, Mungu hufanya mengi yasiyoeleweka na yaliyo ya ajabu. Wakati Mungu anapotaka kupangilia mtu, mpango huu mara nyingi unakinzana na dhana za binadamu, na huwa haueleweki kwa binadamu huyo, ilhali ni ukosefu wa mwafaka huu na kutofahamu ndiyo majaribio ya Mungu na mtihani wake kwa binadamu. Ibrahimu, huku haya yakiendelea, aliweza kuonyesha utiifu kwa Mungu uliokuwa ndani yake, jambo ambalo ndilo lililokuwa sharti muhimu zaidi la yeye kuweza kushibisha mahitaji ya Mungu. Hapo tu, wakati Ibrahimu alipoweza kutii mahitaji ya Mungu, alipomtoa Isaka ndipo Mungu Alipohisi kwa kweli utulivu na kukubaliwa na Mungu—kwa Ibrahimu, ambaye Alikuwa amemchagua. Hapo tu ndipo Mungu alipokuwa na hakika kwamba mtu huyu Aliyekuwa amemchagua Yeye alikuwa kiongozi muhimu ambaye angetekeleza ahadi Yake na mpango Wake wa usimamizi wa baadaye. Ingawaje lilikuwa tu jaribio na mtihani, Mungu alihisi furaha, Alihisi upendo wa binadamu kwake Yeye, na Alihisi akiwa ametulizwa na binadamu kwa mara ya kwanza. Wakati huu ambao Ibrahimu alipokiinua kisu chake ili kumwua Isaka, Mungu alimsimamisha? Mungu hakumruhusu Ibrahimu kumpa Isaka, kwani Mungu hakuwa na nia yoyote ya kumtoa uhai Isaka. Hivyo, Mungu alimsimamisha Ibrahimu kwa wakati mwafaka. Kwake Mungu, utiifu wa Ibrahimu ulikuwa tayari umepita mtihani, kile alichofanya kilitosha, naye Mungu tayari alikuwa ameona matokeo ya kile Alichokuwa amenuia kufanya. Je, matokeo haya yalimtosheleza Mungu? Yaweza kusemekana kwamba matokeo haya yalimtosheleza Mungu na kwamba ndiyo ambayo Mungu alitaka, na ndiyo ambayo Mungu alikuwa ametamani kuyaona. Je, hili ni kweli? Ingawaje, katika miktadha tofauti, Mungu anatumia njia tofauti za kupima kila mtu. Kwa Ibrahimu Mungu aliona kile Alichotaka, Aliona kwamba moyo wa Ibrahimu ulikuwa wa kweli, na kwamba utiifu wake haukuwa na masharti na ilikuwa hali hii hasa ya “kutokuwa na masharti” ambayo Mungu alitamani. Watu mara nyingi husema, tayari nimetoa hii, tayari nimeachana na ile—kwa nini bado Mungu hajatosheka na mimi? Kwa nini Anaendelea kuniweka katika majaribio? Kwa nini Anaendelea kunijaribu? Hii yaonyesha ukweli mmoja: Mungu bado hajauona moyo wako, na bado hajapata moyo wako. Hivi ni kusema, Hajauona uaminifu kama wakati ule ambao Ibrahimu aliweza kukiinua kisu chake ili kumuua mtoto wake kwa mkono wake mwenyewe na kumtoa kwa Mungu. Bado Hajauona utiifu wako usio na masharti, na hajatulizwa na wewe. Ni jambo la kiasili, hivyo basi, kwamba Mungu anaendelea kukujaribu. Je, haya si kweli? Tutaachia hapa kwa mada hii. Halafu, tutasoma “Ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu.”
3. Ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu
(Mwa 22:16-18) … Nimeapa kwa nafsi yangu, akasema BWANA, kwa kuwa umetenda jambo hili, wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee: Kwamba katika kubariki Nitakubariki, na katika kuzidisha Nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulio kwenye ukanda wa pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao; na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watabarikiwa; kwa sababu umeitii sauti yangu.
Huu ni ukamilifu wa maelezo ya baraka za Mungu kwa Ibrahimu. Ingawaje ni fupi, maudhui yake ni mengi: Yanajumuisha sababu ya, na usuli wa, zawadi ya Mungu kwa Ibrahimu, na kile ambacho Alimpa Ibrahimu. Unao pia mhemko wa furaha na msisimko Aliotumia Mungu kutamka maneno haya, , pamoja na udharura wa tamanio Lake la kupata wale wanaoweza kusikiliza maneno Yake. Katika haya, tunaona upendo wa Mungu kwa, na wema Wake kwa, wale wanaotii maneno Yake na kufuata amri Zake. Hivyo, pia, tunaiona gharama Anayolipia ili kupata watu, na utunzaji na fikira Anazotumia kuweza kuwapata. Zaidi ya hayo, kifungu hicho, kilicho na maneno “Nimeapa kwa nafsi yangu,” kinatupa hali ya nguvu ya machungu na maumivu Aliyoyapitia Mungu, na Mungu pekee, usiri wa kazi hii ya mpango wa usimamizi. Ni kifungu cha kuchokonoa fikira, na kile ambacho kilikuwa na umuhimu maalum kwa, na ilikuwa na athari nyingi ajabu kwa wale waliokuja baadaye.

Binadamu Anapata Baraka za Mungu kwa Sababu ya Uaminifu na Utii Wake

Je, baraka aliyopewa Ibrahimu na Mungu tuliyoisoma hapa ni kubwa? Ilikuwa kubwa vipi? Kunayo sentensi moja muhimu hapa: “na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watabarikiwa,” ambayo inaonyesha kwamba Ibrahimu alizipokea baraka ambazo hazikupewa tena kwa mwingine aliyekuja kabla au baadaye. Wakati, alipoulizwa na Mungu, Ibrahimu alimrudisha mwana wake wa pekee—mtoto wake pekee wa kiume na mpendwa Isaka—kwa Mungu (dokezo: Hapa hatuwezi kutumia neno “tolewa sadaka”; tunafaa kusema alimrudisha mtoto wake kwa Mungu), Mungu naye hakumruhusu tu Ibrahimu kutoa Isaka, lakini pia Alimbariki. Ni kwa ahadi gani Alimbariki Ibrahimu? Ahadi ya kuzidisha watoto wake. Na walizidishwa mara ngapi? Maandiko yanatuelezea rekodi hii: “kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulio kwenye ukanda wa pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao; na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watabarikiwa.” Mungu Aliyatamka maneno haya katika muktadha upi? Hivi ni kusema, ni vipi ambavyo Ibrahimu alipokea baraka za Mungu? Alizipokea kama vile tu Mungu anavyosema kwenye maandiko: “kwa sababu umeitii sauti yangu.” Yaani, kwa sababu Ibrahimu alikuwa amefuata amri ya Mungu, kwa sababu alikuwa amefanya kila kitu ambacho Mungu alikuwa amesema, kuomba na kuamuru bila ya malalamiko hata kidogo, hivyo Mungu akatoa ahadi hiyo kwake. Kunayo sentensi moja muhimu katika ahadi hii ambayo inagusia fikira za Mungu wakati huo. Je, umeiona? Huenda hukutilia maanani sana maneno ya Mungu kwamba “Nimeapa kwa nafsi Yangu.” Yale yanamaanisha ni kwamba, wakati Mungu alipoyatamka maneno haya, Alikuwa anajiapisha Mwenyewe. Watu huapa kwa yapi wakati wanapokula kiapo? Wanaapa kwa Mbingu, hivi ni kusema, wanakula kiapo na jina la Mungu na kuapa kwa jina la Mungu. Huenda watu wasiwe na uelewa mwingi wa hali hiyo ambayo Mungu Alijiapisha mwenyewe, lakini mtaweza kuelewa Nitakapowapatia maelezo sahihi. Kukabiliwa na mtu ambaye aliweza tu kuyasikia maneno Yake lakini kutoelewa moyo Wake kwa mara nyingine kulimfanya Mungu kuhisi mpweke na mwenye upungufu. Katika hali ya kukata tamaa—na, yaweza kusemekana, kwa nadhari—Mungu alifanya kitu cha kiasili sana: Mungu aliuweka mkono Wake kwenye moyo wake na kutamka ahadi ya zawadi kwa Ibrahimu kwake Yeye Mwenyewe, na kutokana na haya binadamu akamsikia Mungu akisema “Nimeapa kwa nafsi Yangu.” Kupitia vitendo vya Mungu, unaweza kujifikiria wewe mwenyewe. Unapoweka mkono wako juu ya moyo wako, na kujizungumzia, unalo wazo wazi kuhusu kile unachosema? Je, mwelekeo wako ni wa uaminifu? Unaongea waziwazi, kwa kutumia moyo wako? Hivyo, tunaona hapa kwamba wakati Mungu alipomzungumzia Ibrahimu, Alikuwa mwenye bidii na wa ukweli. Wakati huohuo alipokuwa Akiongea naye Ibrahimu na Akimbariki, Mungu alikuwa pia Akijizungumzia Mwenyewe. Alikuwa Akijiambia: Nitambariki Ibrahimu na kuuzidisha uzao wake kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani, kwa sababu alitii maneno Yangu na ndiye Niliyemchagua. Wakati Mungu aliposema “Nimeapa kwa nafsi Yangu,” Mungu Aliamua kwamba ndani ya Ibrahimu Angezalisha wateule wa Israeli , na baadaye Angewaongoza watu hawa kusonga mbele sambamba na kazi Yake. Yaani, Mungu angekifanya kizazi cha Ibrahimu kufanya kazi ya usimamizi wa Mungu, na kazi ya Mungu na ile iliyoonyeshwa na Mungu ingeanza na Ibrahimu, na kuendelea katika vizazi vya Ibrahimu, na hivyo kuthamini tamanio la Mungu la kuokoa binadamu. Unasemaje, hiki si kitu kilichobarikiwa? Kwa binadamu, hakuna baraka kubwa zaidi kuliko hii; hii, inaweza kusemekana, ndiyo baraka kubwa zaidi. Baraka aliyopata Ibrahimu haikuwa kuzidishwa kwa uzao wake, lakini ilikuwa Mungu kutimiza usimamizi Wake, agizo Lake na kazi Yake kwa vizazi vya Ibrahimu. Hii inamaanisha kwamba baraka alizopata Ibrahimu hazikuwa za muda, lakini ziliendelea kwa kadri mpango wa usimamizi wa Mungu ulipoendelea. Wakati Mungu alipoongea, wakati Mungu alipoapa kwa nafsi Yake Mwenyewe, tayari Alikuwa ameamua. Je, mchakato wa uamuzi huu ulikuwa kweli? Ulikuwa halisi? Mungu aliamua kwamba, kuanzia hapo kuendelea, jitihada Zake, gharama Aliyolipia, kile Anacho na alicho, kila kitu Chake, na hata maisha Yake yangekabidhiwa Ibrahimu na vizazi vya Ibrahimu. Na ndivyo pia Mungu alivyoamua kwamba, kuanzia kwenye kundi hili la watu, Angeonyesha vitendo Vyake, na kumruhusu binadamu kuiona hekima, mamlaka na nguvu Yake.

Kuwapata Wale Wanaomjua Mungu na Wanaweza Kumtolea Ushuhuda Ndilo Tamanio la Mungu Lisilobadilika

Wakati huohuo Alipokuwa akijizungumzia Mwenyewe, Mungu alizungumza pia na Ibrahimu, lakini mbali na kusikiliza baraka ambazo Mungu alimpa, Ibrahimu aliweza kuyaelewa matamanio ya kweli ya Mungu katika maneno Yake yote wakati huo? Hakuweza! Na hivyo, kwa wakati huo, wakati Mungu alipoapa kwa nafsi Yake Mwenyewe, moyo Wake ulikuwa bado pweke na wenye huzuni. Hakukuwepo hata na mtu mmoja wa kuweza kuelewa au kufahamu kile Alichonuia na Alichopangilia. Wakati huo, hakuna—akiwemo Ibrahimu—aliyeweza kuongea na Yeye kwa ujasiri, isitoshe hakuna yule aliyeweza kushirikiana na Yeye katika kufanya kazi ambayo lazima Angefanya. Juujuu, Mungu alikuwa Amempata Ibrahimu na Alipata mtu ambaye angetii maneno Yake. Lakini kwa hakika, maarifa ya mtu huyu kuhusu Mungu yalikuwa kidogo mno. Hata ingawaje Mungu alikuwa amembariki Ibrahimu, moyo wa Mungu ulikuwa bado hujatosheka. Inamaanisha nini kwamba Mungu hakuwa ametosheka? Inamaanisha kwamba usimamizi Wake ulikuwa tu umeanza, inamaanisha kwamba watu Aliotaka kupata, watu Aliotamani kuona, watu Aliopenda, walikuwa bado mbali na Yeye; Alihitaji muda, Alihitaji kusubiri, Alihitaji kuwa na subira. Kwani kwa wakati huo, mbali na Mungu Mwenyewe, hakuna yeyote yule aliyejua kile Alichohitaji au kile Alichotaka kupata, au kile Alichotamani. Na hivyo basi, Kwa wakati uohuo aliokuwa akihisi sana furaha Mungu pia alihisi kuwa mwenye uzito wa moyo. Bado Hakusitisha hatua Zake, na Aliendelea kupanga hatua inayofuata ya kile ambacho lazima Afanye.
Unaona nini katika ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu? Mungu alimpa baraka kuu Ibrahimu kwa sababu tu ya yeye kusikiliza maneno ya Mungu. Ingawaje, juujuu, hali hii yaonekana ya kawaida na suala ambalo bila shaka, ndani yake tunauona moyo wa Mungu: Mungu hasa anathamini utiifu wa binadamu kwake Yeye, na hutunzwa mno na uelewa wa binadamu kuhusu Yeye na uaminifu wake Kwake. Mungu anathamini kiasi kipi uaminifu huu? Huenda usielewe ni kiasi kipi ambacho Yeye Anauthamini, na huenda hata kusiwe na yeyote anayeutambua. Mungu alimpa Ibrahimu mwana, na wakati mwana huyo alipokua, Mungu alimwomba Ibrahimu kumkabidhi mtoto wake Kwake. Ibrahimu alifuata amri ya Mungu kwa umakinifu, alitii neno la Mungu na uaminifu wake ulimpendeza Mungu na ukathaminiwa sana na Mungu. Mungu aliuthamini kiasi kipi? Na kwa nini Akauthamini sana? Kwa wakati ambao hakuna aliyefahamu maneno ya Mungu au kuuelewa moyo Wake, Ibrahimu alifanya kitu kilichotikisa mbingu na kutetemesha ardhi, na kikafanya Mungu kuhisi hali fulani ya kutosheka kwa mara ya kwanza, kikamletea Mungu furaha ya kumpata mtu ambaye aliweza kutii maneno Yake. Uradhi na furaha hii ilitoka kwa kiumbe aliyeumbwa kwa mkono ya Mungu, na ndiyo iliyokuwa “sadaka” ya kwanza ambayo binadamu aliwahi kumpa Mungu na ambayo ilithaminiwa sana na Mungu, tangu binadamu kuumbwa. Mungu alikuwa na wakati mgumu kusubiria sadaka hii, na Aliichukulia kama zawadi ya kwanza muhimu zaidi kutoka kwa binadamu, ambaye Alikuwa amemuumba. Hii ilionyesha Mungu tunda la kwanza la jitihada Zake, na gharama ambayo Alikuwa amelipia na ikamruhusu Yeye kuliona tumaini kwa wanadamu. Baadaye, Mungu alikuwa na hata tamanio kubwa zaidi la kundi la watu kama hao wa kushinda na Yeye kumchukulia Yeye kwa uaminifu, kumtunza Yeye kwa uaminifu. Mungu alitamani hata kwamba Ibrahimu angeendelea kuishi, kwani Alipenda kuwa na moyo kama huo ukiandamana na Yeye na kuwa na Yeye Alipoendelea na usimamizi Wake. Haijalishi ni nini alichotaka Mungu, yalikuwa tu ni matakwa, wazo tu—kwani Ibrahimu alikuwa tu binadamu aliyeweza kumtii Yeye, na wala hakuwa na uelewa au maarifa hata madogo zaidi kuhusu Mungu. Yeye alikuwa mtu aliyepungukiwa pakubwa na viwango vya mahitaji ya Mungu kwa binadamu: kumjua Mungu, kuweza kushuhudia Mungu, na kuwa na akili sawa na Mungu. Na hivyo, hangeweza kutembea na Mungu. Katika sadaka ya Ibrahimu ya Isaka, Mungu aliuona uaminifu na utiifu huu wa Ibrahimu, na Akaona kwamba alikuwa amestahimili jaribio la Mungu kwake yeye. Hata ingawaje Mungu aliukubali uaminifu na utiifu wake, bado hakustahili kuwa mwandani wa Mungu, wa kuwa mtu aliyemjua Mungu, na kumwelewa Mungu, na alifahamishwa kuhusu tabia ya Mungu; alikuwa mbali sana na kuwa na akili sawa na Mungu na vilevile kuweza kutekeleza mapenzi ya Mungu. Hivyo basi, katika moyo Wake, Mungu alikuwa bado mpweke na mwenye wasiwasi. Kwa kadri Mungu alipokuwa mpweke na mwenye wasiwasi zaidi, ndipo Yeye alipohitaji zaidi kuendelea na usimamizi Wake haraka iwezekanavyo, na kuweza kuchagua na kulipata kundi la watu wa kukamilisha mpango Wake wa usimamizi na kutimiza mapenzi Yake haraka iwezekanavyo. Hili ndilo lilikuwa tamanio lenye hamu kubwa la Mungu, na limebakia vilevile kuanzia mwanzo kabisa hadi leo. Tangu Alipomuumba binadamu hapo mwanzo, Mungu ametamani kuwa na kundi la washindi, kundi ambalo litatembea na Yeye na linaweza kuelewa, kufahamu na kujua tabia Yake. Mapenzi haya ya Mungu hayajawahi kubadilika. Haijalishi ni muda gani bado Atasubiria, haijalishi barabara iliyo mbele ni ngumu kiasi gani, hata malengo Anayoyatamani yawe mbali kiasi kipi, Mungu hajawahi kubadilisha au kukata tamaa katika matarajio Yake kuhusu binadamu. Kwa vile nimeyasema haya, unatambua chochote kuhusu mapenzi ya Mungu? Pengine kile ulichotambua hakina uzito sana—lakini kitajitokeza kwa utaratibu!
Kwenye kipindi sawa na kile cha Ibrahimu, Mungu pia aliliangamiza jiji. Jiji hili liliitwa Sodoma. Bila shaka, watu wengi wanaijua hadithi ya Sodoma, lakini hakuna yeyote aliyejua fikira za Mungu zilikuwa usuli wa kuangamiza Kwake jiji hili.
Na hivyo leo, kupitia mazungumzo yake Mungu na Ibrahimu hapa chini, tutajifunza fikira Zake wakati huo, huku pia tukijifunza kuhusu tabia Yake. Kinachofuata, hebu tusome vifungu vya maandiko.
B. Mungu Lazima Aangamize Sodoma.
(Mwa 18:26) Kisha BWANA akasema, Nikipata katika Sodoma wenye haki hamsini mjini, basi Nitapaacha mahali pote kwa ajili yao.
(Mwa 18:29) Na akazungumza tena naye, akasema, Huenda wakapatikana humo arobaini. Akasema, Sitafanya hivyo.
(Mwa 18:30) Akamwambia, labda watapatikana huko thelathini. Naye akasema, Sitafanya hivyo.
(Mwa 18:31) Kisha akasema, huenda wakaonekana huko ishirini. Naye akasema, Sitauharibu.
(Mwa 18:32) Naye akasema, huenda wakaonekana huko kumi. Naye akasema, Sitauharibu.
Hizi ni dondoo chache Nilizochagua kutoka kwenye Biblia. Dondoo hizi si kamilifu, za matoleo ya awali. Kama mngependa kuziona hizo, mnaweza kuzitafuta kwenye Biblia nyinyi wenyewe; ili kuokoa muda, Nimeiacha sehemu ya maudhui asilia. Hapa Nimechagua tu vifungu na sentensi mbalimbali kuu, huku nikiziacha sentensi mbalimbali ambazo hazina umuhimu katika ushirika wetu wa leo. Katika vifungu na maudhui yote tunayotumia katika ushirika, zingatio letu haliyaendei maelezo ya hadithi na mwenendo wa binadamu katika hadithi hizi; badala yake, tunazungumzia tu fikira za Mungu na mawazo Yake wakati huo. Katika fikira na mawazo ya Mungu, tutaiona tabia ya Mungu, na kutoka katika kila kitu alichofanya Mungu, tutaweza kumuona Mungu Mwenyewe wa kweli—na katika haya tutaweza kutimiza malengo yetu.

Mungu Anawajali tu Wale Wanaoweza Kutii Maneno Yake Na Kufuata Amri Zake

Vifungu hivi vilivyotajwa hapo juu vinayo maneno msingi mbalimbali: nambari. Kwanza, Yehova alisema kwamba kama Angewapata wenye haki hamsini ndani ya Jiji, basi Angepanusurisha mahali hapo, hii ni kusema, Asingeangamiza jiji hilo. Hivyo walikuwepo, kwa hakika, watakatifu hamsini ndani ya Sodoma? Hawakuwemo. Muda mfupi baadaye, Ibrahimu alimwambia nini Mungu? Alisema, labda kutakuwemo arubaini waliopatikana humo? Naye Mungu akasema, Sitafanya hivyo. Kisha, Ibrahimu akasema huenda wakawepo thelathini watakaopatikana hapo? Naye Mungu akasema, Sitafanya hivyo. Na labda ishirini? Sitafanya hivyo. Kumi? Sitafanya hivyo. Kulikuwemo, kwa hakika, wenye haki kumi ndani ya jiji? Hapakuwa kumi—lakini kulikuwemo na mmoja. Na huyu mmoja alikuwa nani? Alikuwa Loti. Wakati huo, kulikuwepo tu na mwenye haki mmoja kwenye eneo la Sodoma, lakini Mungu alikuwa mmakinifu sana au mkali kuhusiana na nambari hii? La, hakuwa hivyo! Na wakati binadamu aliendelea kuulizia, “Na je wale arubaini?”“Na je wale thelathini?” mpaka pale alipofika katika sehemu ile ya “Na je wale kumi?” Mungu alisema, “Hata kama wangalikuwemo kumi, Singeangamiza jiji hilo; Ningelinusurisha, na kuwasamehe wale watu wengine mbali na wale kumi.” Idadi ya watu kumi ingekuwa ya kuhurumiwa vya kutosha, lakini ilitokea kwamba, kwa hakika, hakukuwemo na hata ile idadi inayohitajika ya watu wenye haki kule Sodoma. Unaona, basi, kwamba katika macho ya Mungu dhambi na maovu ya watu wa jiji ilikuwa kwa kiasi kwamba Mungu hakuwa na chaguo lolote ila kuwaangamiza. Mungu alimaanisha nini Aliposema kwamba Asingeliharibu jiji kama kungekuwemo na wenye haki hamsini? Nambari hizi hazikuwa muhimu kwa Mungu. Kile kilichokuwa muhimu kilikuwa kama jiji lilikuwa na wenye haki Aliotaka au la. Kama jiji lisingekuwa na mwenye haki yeyote isipokuwa mmoja, Mungu asingewaruhusu madhara kuwepo kutokana na Yeye kuangamiza jiji hilo. Kile ambacho haya yote yanamaanisha ni kwamba, haijalishi kama Mungu angeliangamiza jiji au la, na haijalishi idadi ya wenye haki waliokuwa ndani ya jiji hilo, kwake Mungu jiji hili lenye dhambi lilikuwa limelaaniwa na lilikuwa limejaa maovu, na hivyo lilifaa kuangamizwa, na kutoweka kwenye macho ya Mungu huku nao wenye haki wakisali. Haikulijalisha enzi husika, haikujalisha awamu ya maendeleo ya mwanadamu, mwelekeo wa Mungu haubadiliki: Anachukia maovu, na Anawajali wenye haki mbele ya macho Yake. Mwelekeo huu wazi wa Mungu ndiyo pia ufunuo wa kweli wa kiini cha Mungu. Kwa sababu hakukuwepo na mwenye haki yeyote isipokuwa mmoja ndani ya jiji, Mungu hakusita tena. Matokeo yake ni kwamba Sodoma ingeangamizwa bila kusita. Unaona nini katika haya? Katika enzi hiyo, Mungu asingeangamiza jiji kama wamo wenye haki hamsini ndani yake, wala kama kulikuwemo kumi, kumaanisha kwamba Mungu angeamua kusamehe na kumvumilia mwanadamu, au angefanya kazi ya kuongoza, kwa sababu ya watu wachache ambao waliweza kumstahi na kumwabudu Yeye. Mungu hutilia maanani haki ya binadamu, Hutilia maanani sana kwa wale wanaoweza kumwabudu Yeye, na Anatilia maanani sana wale wanaoweza kufanya matendo mema mbele yake.
Kutoka nyakati za mapema sana hadi leo, umewahi kusoma ndani ya Biblia kuhusu Mungu kuuwasilisha ukweli, au kuzungumzia kuhusu njia ya Mungu, kwa mtu yeyote? La, hujawahi. Maneno ya Mungu kwa binadamu tunayoyasoma yaliwaambia watu tu cha kufanya. Baadhi walienda na wakayafanya, baadhi hawakuyafanya; baadhi walisadiki, na baadhi hawakusadiki. Hivyo ndivyo ilivyokuwa tu. Hivyo, wenye haki wa enzi hiyo—wale waliokuwa wenye haki mbele ya macho ya Mungu—walikuwa wale tu ambao wangeweza kuyasikia maneno ya Mungu na kufuata amri za Mungu. Walikuwa watumishi waliotekeleza maneno ya Mungu miongoni mwa binadamu. Je, watu kama hao wangeweza kuitwa wale wanaomjua Mungu? Wangeweza kuitwa watu waliofanywa kuwa watimilifu na Mungu? La, wasingeweza kuitwa hivyo. Na hivyo, licha ya idadi yao, kwenye macho ya Mungu hawa wenye haki walistahili kuitwa wandani wa Mungu? Wangeweza kuitwa mashahidi wa Mungu? Bila shaka la! Hawakustahili kamwe kuitwa wandani na mashahidi wa Mungu. Na hivyo Mungu aliwaita watu kama hawa vipi? Kwenye Biblia, hadi kufikia kwenye vifungu vya maandiko ambavyo tumetoka kusoma hivi punde, kulikuwa na matukio mengi ya Mungu kuwaita “Mtumishi wangu.” Hivi ni kusema, kwa wakati huo kwenye macho ya Mungu watu hawa wenye haki walikuwa watumishi wa Mungu, walikuwa watu waliomhudumia Yeye duniani. Naye Mungu alifikiria vipi kuhusu jina hilo? Kwa nini Akawaita hivyo? Je, Mungu anavyo viwango ambavyo Anatumia katika Kuwaita watu ndani ya moyo Wake? Bila shaka anavyo. Mungu anavyo viwango, haijalishi kama Anawaita watu wenye haki, watimilifu, wanyofu, au watumishi. Anapomwita mtu mtumishi Wake, Anayo imani thabiti kwamba mtu huyu anaweza kuwapokea wajumbe Wake, na anaweza kufuata amri Zake, na anaweza kutekeleza kile ambacho ameamrishwa kufanya na wale wajumbe. Na mtu huyu anatekeleza nini? Kile ambacho Mungu anamwamuru binadamu kufanya na kutekeleza duniani. Wakati huo, kile ambacho Mungu alimwomba binadamu kufanya na kutekeleza duniani kingeweza kuitwa njia ya Mungu? La, kisingeweza. Kwani wakati huo, Mungu alimwomba tu binadamu kufanya mambo machache rahisi; Alitamka amri chache rahisi, Akimwambia binadamu kufanya hiki au kile, na si zaidi ya hayo. Mungu alikuwa akifanya kazi kulingana na mpango Wake. Kwa sababu, wakati huo, masharti mengi hayakuwepo, muda ulikuwa haujatimia, na ilikuwa vigumu kwake mwanadamu kuvumilia njia ya Mungu, hivyo basi njia ya Mungu ilikuwa bado haijaanza kuwasilishwa mbele kutoka kwenye moyo wa Mungu. Katika haya, tunaona kwamba haijalishi kama kulikuwa thelathini au ishirini ya wale wenye haki aliozungumzia Mungu, mbele ya macho Yake wote walikuwa watumishi Wake. Wakati wajumbe wa Mungu walipowajia watumishi hawa, wangeweza kuwapokea, na kufuata amri zao, na kutenda kulingana na maneno yao. Haya ndiyo hasa yaliyofaa kufanywa, na kutimizwa, na watumishi mbele ya macho ya Mungu. Mungu ni mwenye busara katika majina Yake kwa watu. Hakuwaita watumishi Wake kwa sababu walikuwa vile mlivyo sasa—kwa sababu walikuwa wamesikia mahubiri mengi, walijua kile ambacho Mungu alifaa kufanya, walielewa mengi kuhusu mapenzi ya Mungu na walifahamu mpango Wake wa usimamizi—lakini kwa sababu ubinadamu wao ulikuwa wenye uaminifu na waliweza kutii maneno ya Mungu; wakati Mungu alipowaamuru, waliweza kuweka pembeni kile walichokuwa wakifanya na kutekeleza kile ambacho Mungu aliwaamuru kufanya. Na hivyo, kwake Mungu safu ile nyingine ya maana kwenye cheo cha[b] mtumishi ni kwamba walishirikiana na kazi Yake duniani na ingawaje hawakuwa wajumbe wa Mungu, hao ndio waliokuwa watekelezaji na wafuatiliaji wa maneno ya Mungu duniani. Unaona, basi, watumishi hawa au wenye haki hawa walikuwa na umuhimu mkubwa katika moyo wa Mungu. Kazi ile ambayo Mungu alifaa kuishughulikia duniani isingeweza kufanyika bila ya watu wa kushirikiana na Yeye, na wajibu uliotekelezwa na watumishi wa Mungu usingeweza kufanywa na wajumbe wa Mungu. Kila kazi ambayo Mungu alitoa amri kwa watumishi hawa ilikuwa yenye umuhimu mkubwa Kwake, na hivyo basi Asingeweza kuwapoteza. Bila ya ushirikiano wa watumishi hawa na Mungu, kazi Yake miongoni mwa wanadamu ingefikia kikomo, na matokeo yake ni kwamba mpango wa usimamizi wa Mungu na matumaini ya Mungu vyote visingewezekana.

Mungu ni Mwenye Wingi wa Rehema Kwa Wale Anaowajali, na Mwenye Hasira Kali kwa Wale Anaochukia na Kukataa

Kwenye simulizi za Biblia, kulikuwepo na watumishi kumi wa Mungu kule Sodoma? La, hakukuwepo! Kulikuwepo na jiji lililostahili kusamehewa na Mungu? Mtu mmoja tu kwenye jiji hilo—Loti—ndiye aliye wapokea wajumbe wa Mungu. Matokeo ya haya ni kwamba kulikuwa na mtumishi mmoja tu wa Mungu kwenye jiji, na hivyo basi Mungu hakuwa na chaguo ila kumwokoa Loti na kuliangamiza jiji la Sodoma. Mabadilishano haya kati ya Ibrahimu na Mungu yanaweza kuonekana kuwa rahisi tu, lakini yanaonyesha kitu fulani kikuu: Kuna kanuni za vitendo vya Mungu, na kabla ya kufanya uamuzi Atachukua muda mrefu akiangalia na kutafakari; kabla ya wakati kuwa sawa, bila shaka Hatafanya au kukimbilia hitimisho zozote. Mabadilishano kati ya Ibrahimu na Mungu yanatuonyesha kwamba uamuzi wa Mungu wa kuangamiza Sodoma haukuwa mbaya hata kidogo, kwani Mungu alijua tayari kwamba kwenye jiji hakukuwa na watu arubaini wenye haki, na wala thelathini wenye haki, wala ishirini. Hawakuwa hata kumi. Mtu mwenye haki pekee kwenye jiji alikuwa Loti. Yote yaliyofanyika ndani ya Sodoma na hali zake ziliangaliwa na Mungu, na zilizoeleka kwa Mungu kama sehemu ya nyuma ya mkono Wake. Hivyo, uamuzi Wake usingekosa kuwa sahihi. Kinyume na haya, tukilinganisha uweza wa Mungu, binadamu hajali katu, ni mjinga na asiyejua neno, asiyeona-mbele katu. Haya ndiyo tunayoona katika mabadilishano kati ya Ibrahimu na Mungu. Mungu amekuwa akiwasilisha mbele tabia Yake kuanzia mwanzo hadi leo. Hapa, vilevile, kuna pia tabia ya Mungu tunayofaa kuona. Nambari ni rahisi, na hazionyeshi chochote, lakini hapa kuna maonyesho muhimu sana ya tabia ya Mungu. Mungu asingeangamiza jiji kwa sababu ya watu hamsini wenye haki. Je, haya ni kutokana na rehema ya Mungu? Ni kwa sababu ya upendo na uvumilivu Wake? Je umeuona upande huu wa tabia ya Mungu? Hata kama kungekuwa na wenye haki kumi pekee, Mungu asingeangamiza jiji hili kwa sababu ya watu hawa kumi wenye haki. Je, haya yanaonyesha uvumilivu na upendo wa Mungu au la? Kwa sababu ya rehema, uvumilivu, na kujali kwa Mungu kwa wale watu wenye haki, Asingeliangamiza jiji hili. Huu ndio uvumilivu wa Mungu. Na hatimaye, ni matokeo gani tunayoyaona? Wakati Ibrahimu aliposema, “huenda wakaonekana huko kumi,” Mungu akasema, “Sitauharibu .” Baada ya hapo, Ibrahimu hakusema tena—kwani ndani ya Sodoma hakukuwa na wenye haki kumi aliowarejelea, na hakuwa na chochote ziada cha kusema, na kwa wakati huo alielewa ni kwa nini Mungu alikuwa ameamua kuangamiza Sodoma. Katika haya, ni tabia gani ya Mungu unayoiona? Ni aina gani ya utatuzi ambayo Mungu alifanya? Yaani, kama jiji hili lisingekuwa na wenye haki kumi, Mungu asingeruhusu uwepo wake, na bila shaka Angeliangamiza. Je hii si hasira ya Mungu? Je, hasira hii inawakilisha tabia ya Mungu? Je, hii tabia ni ufunuo wa kiini cha haki cha Mungu? Je, huu ni ufunuo wa kiini cha haki ya Mungu, ambacho binadamu hafai kukosea? Baada ya kuthibitisha kwamba hakukuwa na wenye haki kumi kule Sodoma, Mungu alikuwa na hakika ya kuliangamiza jiji, na angewaadhibu vikali watu walio ndani ya hilo jiji, kwani walimpinga Mungu, na kwa sababu walikuwa wachafu na waliopotoka.
Kwa nini tumechambua vifungu hivi kwa njia hii? Kwa sababu sentensi hizi chache rahisi zinatupa maonyesho kamili ya tabia ya Mungu ya wingi wa rehema na hasira kali. Wakati sawa na kuthamini sana wale wenye haki na kuwa na rehema juu yao, kuwavumilia, na kuwajali, ndani ya moyo wa Mungu kulikuwa na chukizo kuu kwa wale waliokuwa ndani ya Sodoma ambao walikuwa wamepotoshwa. Je, hii ilikuwa, au haikuwa rehema nyingi na hasira kali? Ni kwa mbinu zipi Mungu aliliangamiza jiji? Kwa moto. Na kwa nini Aliliangamiza kwa kutumia moto? Unapoona kitu kikiungua kwa moto, au wakati uko karibu kuchoma kitu, ni nini hisia zako juu ya kitu hicho? Kwa nini unataka kukichoma? Unahisi kwamba hukihitaji tena, kwamba hutaki tena kukiangalia? Unataka kukiacha? Matumizi ya moto na Mungu yanamaanisha uwachaji, na chuki, na kwamba hakutaka tena kuiona Sodoma. Hii ilikuwa ni hisia iliyomfanya Mungu kuteketeza Sodoma kwa moto. Matumizi ya moto yanawakilisha namna ambavyo Mungu alikuwa amekasirika. Rehema na uvumilivu wa Mungu kwa kweli vipo, lakini utakatifu na uhaki wa Mungu Anapoachilia hasira Yake pia inaonyesha binadamu upande wa Mungu usiyovumilia kosa lolote. Wakati binadamu anaweza kabisa kutii amri za Mungu na kutenda kulingana na mahitaji ya Mungu, Mungu anakuwa mwingi katika huruma Yake kwa binadamu; wakati binadamu amejawa na upotoshaji, chuki na uadui kwake Yeye, Mungu anakuwa mwenye ghadhabu nyingi. Na anakuwa na ghadhabu nyingi hadi kiwango kipi? Hadi kiwango kipi ndipo anapokuwa na ghadhabu nyingi? Hasira yake itaendelea kuwepo mpaka pale ambapo Mungu hataona tena upinzani wa binadamu na matendo maovu, mpaka vyote hivi havipo tena mbele ya macho Yake. Hapo tu ndipo ghadhabu ya Mungu itakapotoweka. Kwa maneno mengine, haijalishi mtu husika ni yupi, kama moyo wake umekuwa mbali na Mungu, na yeye amemgeukia Mungu, asirudi tena, basi haijalishi ni vipi, kwa mionekano yote au kuhusiana na matamanio yake ya kibinafsi, atapenda kuabudu na kufuata na kutii Mungu katika mwili wake au katika kufikiria kwake pindi tu moyo wake utakapokuwa mbali na ule wa Mungu, hasira ya Mungu itaachiliwa bila kikomo. Itakuwa kwamba wakati Mungu anapoiachilia kabisa ghadhabu Yake, akiwa amempa binadamu fursa za kutosha, pindi inapoachiliwa hakutakuwepo na njia yoyote ya kuirudisha, na hatawahi tena kuwa mwenye huruma na mvumilivu kwa mtu kama huyo. Huu ni upande mmoja wa tabia ya Mungu isiyovumilia kosa. Hapa, yaonekana kawaida kwa watu kwamba Mungu angeliangamiza jiji, kwani ndani ya macho ya Mungu, jiji lililojaa dhambi lisingeweza kuwepo na kuendelea kubakia pale, na ilikuwa jambo ya kueleweka kwamba jiji hilo liangamizwe na Mungu. Lakini katika kile kilichofanyika kabla ya na kufuatia uangamizi Wake wa Sodoma, tunaiona tabia nzima ya Mungu. Yeye ni mvumilivu na mwenye huruma kwa viumbe walio na upole, na wenye wema; kwa vitu viovu, na vyenye dhambi, na vilivyojaa maovu, Yeye anayo hasira kali , kiasi cha kwamba Hawachi kuendeleza hasira Yake. Hivi ndivyo vipengele viwili vikuu na vinavyojitokeza zaidi kuhusu tabia ya Mungu, na, zaidi, vimefichuliwa na Mungu kutoka mwanzo hadi mwisho: wingi wa huruma na ghadhabu nyingi. Wengi wenu hapa mmepitia huruma ya Mungu, lakini wachache sana wameweza kutambua hasira ya Mungu. Huruma na upole wa upendo wa Mungu unaweza kuonekana kwa kila mmoja; yaani, Mungu Amekuwa mwingi wa huruma kwa kila mmoja. Ilhali ni nadra sana—au, inaweza kusemekana, kwamba—Mungu amekuwa na ghadhabu nyingi kwa watu binafsi au sehemu yoyote ya watu miongoni mwenu hapa leo. Tulia! Hivi karibuni au baadaye, hasira ya Mungu itaonekana na kupitiwa na kila mmoja, lakini kwa sasa bado muda haujawadia. Na kwa nini hivi? Kwa sababu wakati Mungu anakuwa na ghadhabu kila mara kwa mtu, yaani, wakati Anapoiachilia hasira Yake kuu kwao, inamaanisha kwamba Amekuwa akichukia na Akikataa kwa muda mrefu mtu huyu, kwamba Anadharau uwepo wake na kwamba Hawezi kuvumilia uwepo wake; pindi tu ghadhabu Yake inapomjia, watatoweka. Leo, kazi ya Mungu bado haijafikia hapo. Hakuna yeyote kati yenu ambaye ataweza kuivumilia pindi tu Mungu anapoghadhabika kupindukia. Unaona, kisha, kwamba kwa wakati huu Mungu anayo huruma nyingi tu kwa watu wote, na ungali hujaona ghadhabu yake nyingi. Kama wapo wale wanaobakia wakiwa hawajashawishika, mnaweza kuuliza kuwa hasira ya Mungu ije kwenu e, ili mweze kuipitia na kujua kama ghadhabu ya Mungu na tabia Yake isiyokosewa kwa binadamu ipo kwa kweli au la. Mtathubutu kufanya hivyo?

Watu Wa Siku Za Mwisho Wanaiona tu Hasira Ya Mungu Katika Maneno Yake, na Hawaipitii kwa Kweli Hasira Ya Mungu

Je, pande mbili za tabia ya Mungu zinazoonekana kwenye vifungu hivi vya maandiko zinastahili ushirika? Baada ya kuisikia hadithi hii, je, unao uelewa mpya kuhusu Mungu? Ni uelewa aina gani? Inaweza kusemekana kwamba kuanzia wakati wa uumbaji mpaka leo, hakuna kikundi ambacho kimefurahia neema au huruma nyingi za Mungu pamoja na upole wa upendo kama kikundi hiki cha mwisho. Ingawaje, kwenye awamu ya mwisho, Mungu amefanya kazi Yake ya hukumu na kuadibu, na Amefanya kazi Yake kwa adhama na hasira, wakati mwingi Mungu anatumia tu maneno kukamilisha kazi Yake; Anatumia maneno ili kufunza, kunyunyiza na kutosheleza, na kulisha. Hasira ya Mungu, wakati haya yakiendelea, siku zote imefichwa, na mbali na kuipitia tabia ya Mungu yenye hasira kwa maneno Yake, watu wachache sana wamepitia ghadhabu Yake ana kwa ana. Hivi ni kusema, kwamba wakati wa kazi ya hukumu na kuadibu kwa Mungu, ingawaje hasira iliyofichuliwa katika maneno ya Mungu inawaruhusu watu kupitia adhama na kutovumilia kosa kwa Mungu, hasira hii haizidi maneno Yake. Kwa maneno mengine, Mungu hutumia maneno ili kukemea binadamu, kumfichua binadamu, kuhukumu binadamu, kumwadhibu binadamu na hata kumshutumu binadamu—lakini Mungu angali hajawa mwenye wingi wa ghadhabu kwa binadamu, na hata hajaachilia hasira Yake kwa binadamu nje ya maneno yake. Hivyo, rehema na upole wa upendo wa Mungu uliopitiwa na binadamu kwenye enzi hii ni ufunuo wa tabia ya kweli ya Mungu, huku hasira ya Mungu iliyoipitiwa na binadamu ikiwa tu ni athari ya sauti na hisia za matamko Yake. Watu wengi wanachukulia athari hii kimakosa na kuiona kuwa njia ya kweli ya kupitia na maarifa ya kweli ya hasira ya Mungu. Hivyo basi, watu wengi wanasadiki kwamba wameiona huruma ya Mungu na upole wa upendo ndani ya maneno Yake, kwamba wameweza pia kushuhudia kutovumilia Kwake kwa kosa la binadamu, na wengi wao wamekuja hata kutambua huruma na uvumilivu wa Mungu kwake binadamu. Haijalishi tabia ya binadamu ni mbaya kiasi kipi, au upotovu wa tabia yake, Mungu siku zote anavumiliwa. Katika kuvumiliwa, nia Yake ni kusubiria maneno Aliyokuwa Ametamka, jitihada Alizofanya na gharama Aliyolipia ili kutimiza athari iliyo ndani ya wale Anaotaka kupata. Kusubiria matokeo kama haya yanachukua muda, na yanahitaji uumbaji wa mazingira tofauti ya binadamu, kwa njia sawa ambayo watu hawawi watu wazima pindi tu wanapozaliwa; huchukua miaka kumi na minane au kumi na tisa na baadhi ya watu hata huhitaji miaka ishirini au thelathini kabla hawajakomaa na kuwa mtu mzima halisi. Mungu husubiria kukamilika kwa mchakato huu, Yeye husubiria kuwadia kwa muda huo, na Yeye husubiria kufika kwa matokeo haya. Na kwa muda wote Anaousubiria, Mungu huwa mwenye wingi wa huruma. Kwenye kipindi cha kazi ya Mungu, hata hivyo, kiwango kidogo sana cha watu kinaangamizwa, na baadhi wanaadhibiwa kwa sababu ya upinzani wao mkuu kwa Mungu. Mifano kama hiyo ni ithibati kubwa zaidi ya tabia ya Mungu ambayo haivumilii kosa la binadamu, na inathibitisha kabisa uwepo wa kweli wa uvumilivu na ustahimilivu wa Mungu kwa wale wateule. Bila shaka, katika mifano hii halisi, ufunuo wa sehemu ya tabia ya Mungu kwa watu hawa hauathiri jumla ya mpango wa usimamizi wa Mungu. Kwa hakika, kwenye awamu hii ya mwisho ya kazi ya Mungu, Mungu amevumilia kwenye kipindi hiki chote ambacho Amekuwa akisubiria na Amebadilisha uvumilivu Wake na maisha Yake kwa wokovu wa wale wanaomfuata Yeye. Unayaona haya yote? Mungu haharibu mpango Wake bila sababu. Anaweza kuiachilia hasira Yake na Anaweza pia kuwa mwenye huruma; huu ndio ufunuo wa sehemu mbili kuu za tabia ya Mungu. Je, hii iko au haiko wazi kabisa? Kwa maneno mengine, tunapokuja kwa Mungu, sahihi na isiyokuwa sahihi, yenye haki na dhalimu, nzuri na mbaya—hivi vyote vimeonyeshwa waziwazi kwa binadamu. Kile Atakachofanya, kile Anachopenda, kile Anachochukia—yote haya yanaweza kuonyeshwa moja kwa moja katika tabia Yake. Mambo kama hayo yanaweza pia kuwa ya waziwazi sana na ya kuonekana katika kazi ya Mungu na hayako juujuu au kwa jumla; badala yake, yanaruhusu watu wote kutazama tabia ya Mungu na kile Anacho na alicho hasa kwa njia thabiti, ya kweli na ya kimatendo. Huyu ndiye Mungu Mwenyewe wa kweli.

Tabia ya Mungu Haijawahi Kufichwa Kutoka Kwa Binadamu—Moyo wa Binadamu Umepotoka kwa Mungu

Kama Sikushiriki kuhusu mambo haya, hakuna yeyote kati yenu ambaye angeweza kutazama tabia ya kweli ya Mungu katika hadithi za Biblia. Hii ni ukweli. Hiyo ni kwa sababu, ingawaje hadithi hizi za kibiblia zilirekodi baadhi ya mambo ambayo Mungu alifanya, Mungu aliongea mambo machache na hakuitambulisha tabia Yake kwa njia ya moja kwa moja au kuwasilisha mbele waziwazi mapenzi Yake kwa binadamu. Vizazi vya baadaye vimechukulia rekodi hizi kama tu hadithi, na hivyo yaonekana kwa watu kwamba Mungu anajificha kutoka kwa binadamu na kwamba si mwili wa Mungu ambao umefichwa kutoka kwa binadamu, lakini tabia na mapenzi Yake. Baada ya ushirika wangu leo, bado unahisi kwamba Mungu amefichwa kabisa kutoka kwa binadamu? Bado unasadiki kwamba tabia ya Mungu imefichwa kutoka kwa binadamu?
Tangu wakati wa uumbaji, tabia ya Mungu imeenda sako kwa bako na kazi Yake. Haijawahi kufichwa kutoka kwa binadamu, lakini imewekwa kadamnasi na kwa dhahiri kabisa kwa binadamu. Ilhali, kwa kadri muda unavyopita, moyo wa binadamu umekua hata mbali zaidi na Mungu, na kwa kuwa upotovu wa mwanadamu umekuwa wa kina zaidi, binadamu na Mungu wamekuwa mbali na mbali zaidi kati yao. Kwa utaratibu lakini kwa uhakika, binadamu ametoweka kutoka kwa macho ya Mungu. Binadamu ameshindwa kuweza “kuona” Mungu, jambo ambalo limemwacha yeye bila “habari” zozote kuhusu Mungu; hivyo, hajui kama Mungu yupo, na hata anaenda mbali mno kiasi cha kukataa kabisa kuwepo kwa Mungu. Kwa hivyo, kutofahamu kwa binadamu kuhusu tabia ya Mungu na kile Anacho na alicho si kwa sababu Mungu amefichwa kutoka kwa binadamu, lakini kwa sababu moyo wake umemgeukia Mungu. Ingawaje binadamu anamsadiki Mungu, moyo wa binadamu haupo na Mungu, na hajui chochote kuhusu namna ya kumpenda Mungu, wala hataki kumpenda Mungu, kwani moyo wake haujawahi kusonga karibu na Mungu na siku zote anamuepuka Mungu. Kutokana na haya, moyo wa binadamu umekuwa mbali sana na Mungu. Kwa hivyo moyo wake uko wapi? Kwa hakika, moyo wa binadamu haujaenda popote: Badala ya kuupatia moyo huo Mungu, au kuufichua kwa Mungu ili Aweze kuuona, amejiekea yeye mwenyewe. Hiyo ni licha ya ukweli kwamba baadhi mara nyingi wanamwomba Mungu na kusema, “Ee Bwana, utazame moyo wangu—unajua yote ninayofikiria,” na baadhi hata huapa kumruhusu Mungu kuwafikiria, kwamba waweze kuadhibiwa kama watavunja kiapo chao. Ingawaje binadamu anamruhusu Mungu kuangalia ndani ya moyo wake, hii haimanishi kwamba anaweza kutii mipango na mipangilio ya Mungu, wala kwamba ameacha hatima na matarajio yake na mambo yake yote katika udhibiti wa Mungu. Hivyo, licha ya viapo unavyotoa kwa Mungu au mwelekeo kwake Yeye, kwa macho ya Mungu moyo wako ungali umefungwa kwake Yeye, kwani unamruhusu Mungu tu kuangalia kwenye moyo wako lakini humruhusu Yeye kuudhibiti. Kwa maneno mengine, hujampa Mungu moyo wako kamwe, na unazungumza tu maneno yanayosikika kuwa matamu ili Mungu asikie; nia zako mbalimbali za kijanja, huku, unajificha kutoka kwa Mungu, unajificha usionekane na Mungu, pamoja na maajabu, njama, na mipango yako, na unashikilia matarajio na hatima yako mikononi mwako, ukiwa na hofu kubwa kwamba huenda yakachukuliwa na Mungu. Hivyo, Mungu hatazamii uaminifu wa binadamu kwake Yeye. Ingawaje Mungu anaangalia kina cha moyo wa binadamu, na Anaweza kuona kile ambacho binadamu anafikiria na anataka kufanya moyoni mwake, na Anaweza kuona ni mambo yapi yamewekwa ndani ya moyo wake, moyo wa binadamu haumilikiwi na Mungu, hajautoa ili udhibitiwe na Mungu. Hivi ni kusema, Mungu anayo haki ya kuangalia, lakini Hana haki ya kuudhibiti moyo huo. Kwenye nadharia za kibinafsi za binadamu, binadamu hataki wala hanuii kujiacha kwenye huruma za Mwenyezi Mungu. Binadamu hajajifungia tu kutoka kwa Mungu, bali kunao hata watu wanaofikiria njia za kusetiri mioyo yao, kwa kutumia mazungumzo matamu na sifa za kinafiki ili kuunda hali ya uongo na kupata uaminifu wa Mungu, na kuficha uso wao wa kweli dhidi ya kuonekana na Mungu. Nia yao ya kutomruhusu Mungu kuona ni kutoruhusu Mungu kuelewa namna walivyo kwa kweli. Hawataki kuitoa mioyo yao kwa Mungu lakini wanajihifadhia wao wenyewe. Maandishi madogo ya haya ni kwamba kile ambacho binadamu anafanya na kile ambacho anataka kimepangiliwa chote, kikapigiwa hesabu, na kuamuliwa na binadamu mwenyewe; haihitaji kushiriki au kuingilia kati kwa Mungu, na isitoshe hahitaji mipango na mipangilio ya Mungu. Hivyo, iwapo ni kuhusiana na amri za Mungu, agizo Lake, au mahitaji ambayo Mungu anamwekea binadamu, uamuzi wa binadamu unatokana na nia na maslahi yake mwenyewe, katika mazingira na hali yake mwenyewe ya wakati huo. Siku zote binadamu anatumia maarifa na maono ambayo amezoeana nayo, na akili zake binafsi ili kuamua na kuchagua njia anayofaa kutembelea na haruhusu uingiliaji kati au udhibiti wa Mungu. Huu ndio moyo wa binadamu ambao Mungu anaona.
Kuanzia mwanzo hadi leo, ni binadamu tu ambaye ameweza kuzungumza na Mungu. Yaani, miongoni mwa viumbe wote walio hai na viumbe wa Mungu, hakuna yeyote isipokuwa binadamu ameweza kuzungumza na Mungu. Binadamu anayo masikio yanayomwezesha kusikia, na macho yanayomwezesha kuona, anayo lugha na fikira zake binafsi, na pia anao uhuru wa kuamua chochote. Anamiliki kila kitu kinachohitajika kusikia Mungu akiongea, na kuelewa mapenzi ya Mungu, na kukubali agizo la Mungu, na hivyo basi Mungu anayaweka matamanio yake yote kwake binadamu, Akitaka kumfanya binadamu kuwa mwandani Wake ambaye anayo akili sawa na Yeye na ambaye anaweza kutembea na Yeye. Tangu Alipoanza kusimamia, Mungu amekuwa akisubiria binadamu kumpa moyo wake, kumwacha Mungu kuutakasa na kuufaa ipaswavyo, kumfanya yeye kumtosheleza Mungu na kupendwa na Mungu, kumfanya yeye kumstahi Mungu na kujiepusha na maovu. Mungu amewahi kutazamia mbele na kusubiria matokeo haya. Kunao watu kama hawa miongoni mwa rekodi za Biblia? Yaani, kunao wowote kwenye Biblia wanaoweza kutoa mioyo yao kwa Mungu? Kunaye yeyote anayetangulia kabla ya enzi hii? Leo, hebu tuendelee kusoma simulizi za Biblia na kuangalia kama kile kilichofanywa na mhusika huyu—Ayubu—kina muunganisho wowote na mada ya “kumpa Mungu moyo wako” ambalo tunazungumzia kuhusu leo. Hebu tuone kama Ayubu alimtosheleza Mungu na kupendwa na Mungu.
Maoni yako ni yapi kuhusu Ayubu? Wakitolea mifano ya maandiko asilia, baadhi ya watu husema kwamba Ayubu “alimcha Mungu na kujiepusha na maovu.” “Alimcha Mungu na kujiepusha na maovu: Huo ndio ukadiriaji mojawapo asilia wa Ayubu uliorekodiwa kwenye Biblia. Kama uliyatumia maneno yako binafsi, unawezaje kumzungumzia Ayubu? Baadhi ya watu wanasema kwamba Ayubu alikuwa binadamu mzuri mwenye busara, baadhi wanasema kwamba alikuwa na imani ya kweli kwa Mungu; baadhi wanasema kwamba Ayubu alikuwa binadamu mwenye haki na utu. Mmeiona imani ya Ayubu, hivi ni kusema, katika mioyo yenu mnaambatisha umuhimu mkubwa kwa na mnaionea wivu imani ya Ayubu. Leo, basi, hebu tuzungumzie kile kilichomilikiwa na Ayubu ambacho Mungu anafurahishwa sana naye. Kisha, hebu tusome maandiko yaliyo hapa chini.
C. Ayubu
1. Ukadiriaji wa Ayubu na Mungu na kwenye Biblia
(Ayubu 1:1) Palikuwa na mtu katika nchi ya Uzi, jina lake aliitwa Ayubu; mtu huyo alikuwa mkamilifu na mnyoofu, na mmoja aliyemcha Mungu, na kuepukana na uovu .
(Ayubu 1:5) Na ilikuwa hivyo, hizo siku za karamu zao zilipokuwa zimetimia, Ayubu aliwatuma na kuwatakasa, kisha akaamka asubuhi na mapema, na kutoa sadaka za kuteketezwa kulingana na hesabu yao wote ilivyokuwa; kwani Ayubu alisema, Inaweza kuwa kwamba wanangu wamefanya dhambi, na kumkufuru Mungu mioyoni mwao. Hivyo ndivyo Ayubu alivyofanya siku zote.
(Ayubu 1:8) Kisha BWANA akamwuliza Shetani, Je, umemwangalia mtumishi wangu Ayubu, kwa kuwa hakuna hata mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mnyofu, mwenye kumcha Mungu, na kuuepuka uovu?
Ni nini hoja kuu unayoiona kwenye vifungu hivi? Vifungu hivi vitatu vifupi vya maandiko vyote vinahusu Ayubu. Ingawaje ni vifupi, vinaelezea waziwazi alikuwa mtu wa aina gani. Kupitia kwa ufafanuzi wake kuhusu tabia ya kila siku ya Ayubu na mwenendo wake, vinaelezea kila mmoja kwamba, badala ya kukosa msingi, ukadiriaji wa Mungu ya Ayubu ulikuwa na msingi wake na ulikuwa umekita mizizi. Vinatuambia kwamba iwapo ni utathmini wa binadamu kuhusu Ayubu (Ayubu 1:1), au utathmini wa Mungu kuhusu yeye (Ayubu 1:8), tathmini zote zinatokana na matendo ya Ayubu mbele ya Mungu na binadamu (Ayubu 1:5)
Kwanza, hebu tukisome kifungu nambari moja: “Palikuwa na mtu katika nchi ya Uzi, jina lake aliitwa Ayubu; mtu huyo alikuwa mkamilifu na mnyoofu, na mmoja aliyemcha Mungu, na kuepukana na uovu.” Ukadiriaji wa kwanza wa Ayubu kwenye Biblia, sentensi hii ndiyo utathmini wa mwandishi kuhusu Ayubu Kiasili, unawakilisha pia ukadiriaji wa binadamu kuhusu Ayubu, ambayo ni “mtu huyo alikuwa mkamilifu na mnyoofu, na mmoja aliyemcha Mungu, na kuepukana na uovu” Kisha, hebu tuusome utathmini wa Mungu kuhusu Ayubu: “kwa kuwa hakuna hata mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mnyofu, mwenye kumcha Mungu, na kuuepuka uovu” (Ayubu 1:8). Kati ya tathmini hizi mbili, moja ilitoka kwa binadamu, na nyingine ikatoka kwa Mungu; ni ukadiriaji aina mbili ulio na maudhui moja. Inaweza kuonekana, basi, kwamba tabia na mwenendo wa Ayubu ulijulikana kwa binadamu, na pia ulisifiwa na Mungu. Kwa maneno mengine, mwenendo wa Ayubu mbele ya binadamu na mwenendo wake mbele ya Mungu ulikuwa sawa; aliweka tabia yake na motisha yake mbele ya Mungu siku zote, ili hivi viwili viweze kuangaliwa na Mungu, na yeye alikuwa mmoja aliyemcha Mungu na kujiepusha na maovu. Hivyo, katika macho ya Mungu, kati ya watu duniani, ni Ayubu tu ambaye alikuwa mtimilifu na mnyofu, ndiye aliyemcha Mungu na kujiepusha na maovu.

Maonyesho Mahususi ya Kumcha Mungu kwa Ayubu na Kujiepusha na Maovu katika Maisha Yake ya Kila siku

Kisha, hebu tuangalie maonyesho mahususi ya kumcha Mungu kujiepusha na maovu kwa Ayubu. Juu ya vifungu hivi vinavyotangulia na kufuata, hebu pia tusome Ayubu 1:5, ambayo ni mojawapo ya maonyesho mahususi ya kumcha Mungu na kujiepusha kwa maovu kwa Ayubu. Inahusu namna ambavyo alimcha Mungu na kujiepusha na maovu katika maisha yake ya kila siku; muhimu zaidi, hakufanya tu kile alichostahili kufanya kwa minajili ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu kwake, lakini pia mara kwa mara alitoa sadaka iliyoteketezwa mbele ya Mungu kwa niaba ya wana wake. Alikuwa na hofu kwamba walikuwa mara nyingi “wametenda dhambi, na kumlaani Mungu katika mioyo yao” wakati wakiwa na karamu. Na uoga huu ulijionyesha vipi ndani ya Ayubu? Maandishi asilia yanatupa simulizi ifuatayo: “Na ilikuwa hivyo, hizo siku za karamu zao zilipokuwa zimetimia, Ayubu aliwatuma na kuwatakasa, kisha akaamka asubuhi na mapema, na kutoa sadaka za kuteketezwa kulingana na hesabu yao wote ilivyokuwa.” Mwenendo wa Ayubu unatuonyesha kwamba, badala ya kuonyeshwa katika tabia yake ya nje, kumcha Mungu kwake kulitokea ndani ya moyo wake, na kwamba kumcha Mungu kwake kungepatikana katika kila kipengele cha maisha yake ya kila siku, wakati wote, kwani hakujiepusha na maovu tu yeye mwenyewe, lakini pia alitoa sadaka zilizoteketezwa kwa niaba ya watoto wake wa kiume. Kwa maneno mengine, Ayubu hakuwa tu mwenye hofu ya kutenda dhambi dhidi ya Mungu na kumkataa Mungu katika moyo wake, lakini pia alikuwa na wasiwasi kwamba watoto wake wa kiume walitenda dhambi dhidi ya Mungu na kumkataa Yeye katika mioyo yao. Kutokana na haya ukweli unaweza kuonekana kwamba ukweli wa kumcha Mungu kwa Ayubu unapita uchunguzi, na ni zaidi ya shaka ya binadamu yeyote. Je, alifanya hivi mara kwa mara, au mara nyingi? Sentensi ya mwisho ya maandishi ni “Hivyo ndivyo Ayubu alivyofanya siku zote.” Maana ya maneno haya ni kwamba Ayubu hakuenda na kuangalia watoto wake mara kwa mara au wakati alipenda kufanya hivyo, wala hakutubu kwa Mungu kupitia kwa maombi. Badala yake, aliwatuma mara kwa mara na kuwatakasa watoto wake wa kiume kutoa sadaka iliyoteketezwa kwa niaba yao. Hiyo kauli “bila kusita” hapa haimaanishi alifanya hivyo kwa siku moja au mbili, au kwa muda mfupi tu. Inasema kwamba maonyesho ya kumcha Mungu kwa Ayubu hayakuwa ya muda, na hayakusita kwa maarifa aliyokuwa nayo au kwa maneno aliyotamka; badala yake, njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu iliongoza moyo wake, iliamuru tabia yake, na ilikuwa, ndani ya moyo wake mzizi wa uwepo wake. Kwamba alifanya hivyo bila kusita yaonyesha kwamba, katika moyo wake, mara nyingi alikuwa na hofu kwamba yeye mwenyewe angetenda dhambi dhidi ya Mungu na alikuwa na wasiwasi pia kwamba watoto wake wa kiume na binti zake walitenda dhambi dhidi ya Mungu. Inawakilisha namna tu ambavyo uzito wa njia ambayo alimcha Mungu na kujiepusha na maovu ulibebwa ndani ya moyo wake. Alifanya hivyo bila kusita kwa sababu, ndani ya moyo wake, alikuwa na hofu na wasiwasi—wasiwasi kwamba alikuwa ametenda maovu na kutenda dhambi dhidi ya Mungu, na kwamba alikuwa amepotoka kutoka kwenye njia ya Mungu, na basi alikuwa hawezi kutosheleza Mungu. Wakati huohuo, alikuwa pia na wasiwasi kuhusu watoto wake wa kiume na binti zake, akiogopa kwamba walikuwa wamemkosea Mungu. Hivyo ndivyo ulivyokuwa mwenendo wa kawaida wa Ayubu katika maisha yake ya kila siku. Kwa hakika ni mwenendo wa kawaida ambao unathibitisha kwamba kumcha Mungu na kujiepusha kwa maovu kwa Ayubu si maneno matupu tu, kwamba Ayubu aliishi kwa kudhihirisha kwa kweli ukweli kama huo. “Hivyo ndivyo Ayubu alivyofanya siku zote”: Maneno haya yanatuambia kuhusu matendo ya kila siku ya Ayubu mbele ya Mungu. Alipofanya hivi bila kusita, tabia yake na moyo wake vilifika mbele ya Mungu? Kwa maneno mengine, Mungu mara nyingi alipendezwa na moyo wake na tabia yake? Basi, ni katika hali gani na katika muktadha gani Ayubu alifanya hivi bila kusita? Baadhi ya watu wanasema kwamba ilikuwa ni kwa sababu Mungu alijitokeza kwa Ayubu mara kwa mara na ndiyo maana akatenda hivi; baadhi wanasema kwamba alifanya hivi bila kusita kwa sababu angejiepusha na maovu; na baadhi wanasema kwamba alifikiria kwamba utajiri wake ulikuwa haujaja kwa urahisi, na alijua kwamba alikuwa amepewa na Mungu, na hivyo alikuwa na uoga mwingi wa kupoteza mali yake kutokana na kutenda dhambi dhidi ya au kumkosea Mungu. Je, yapo madai yoyote kati ya haya yaliyo kweli? Bila shaka la. Kwani, kwa macho ya Mungu, kile Mungu amekubali na kupenda sana kuhusu Ayubu si tu kwamba alifanya hivi bila kusita; zaidi ya hapo, ilikuwa ni mwenendo wake mbele ya Mungu, binadamu, na Shetani alipokabidhiwa Shetani na kujaribiwa. Sehemu zilizo hapa chini zinatupa ithibati yenye ushawishi mkubwa zaidi, ithibati ambayo inatuonyesha ukweli wa ukadiriaji wa Mungu kwa Ayubu. Kinachofuata, hebu tusome maandiko kwenye vifungu vifuatavyo.
2. Shetani Anamjaribu Ayubu kwa Mara ya Kwanza (Mifugo Yake Yaibiwa na Janga Lawapata Watoto Wake)
a. Maneno Yaliyotamkwa na Mungu
(Ayubu 1:8) Je, umemwangalia mtumishi wangu Ayubu, kwa kuwa hakuna hata mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mnyofu, mwenye kumcha Mungu, na kuuepuka uovu?
(Ayubu 1:12) BWANA akamwambia Shetani, Tazama, yote aliyo nayo yamo katika uwezo wako; lakini usinyoshe mkono wako juu yake yeye mwenyewe. Basi Shetani akatoka mbele za uso wa BWANA.
b. Jibu la Shetani
(Ayubu 1:9-11) Kisha Shetani akamjibu BWANA, akasema, Je, Huyo Ayubu anamcha BWANA bure? Wewe hujamzingira kwa ukigo pande zote, na kwa nyumba yake, na vitu vyote alivyo navyo kwa kila upande? Umezibariki kazi za mikono yake, na mali yake imeongezeka katika nchi. Lakini nyosha mkono wako sasa, uyaguse hayo yote aliyo nayo, na yeye atakukufuru mbele ya uso wako.

Mungu Amruhusu Shetani Kumjaribu Ayubu ili Imani ya Ayubu iweze Kufanywa Kuwa Timilifu

Ayubu 1:8 ndiyo rekodi ya kwanza tunayoiona kwenye Biblia kuhusu mabadilishano kati ya Yehova Mungu na Shetani. Na ni nini alichosema Mungu? Maandishi asilia yanatupatia simulizi ifuatayo: “Kisha BWANA akamwuliza Shetani, Je, umemwangalia mtumishi wangu Ayubu, kwa kuwa hakuna hata mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mnyofu, mwenye kumcha Mungu, na kuuepuka uovu?” Huu ulikuwa ukadiriaji wa Mungu kuhusu Ayubu kwa Shetani; Mungu alisema kwamba alikuwa binadamu mtimilifu na mnyofu, yule aliyemcha Mungu na kujiepusha na maovu. Kabla ya maneno haya kati ya Mungu na Shetani, Mungu alikuwa ameamua kwamba Angemtumia Shetani kujaribu Ayubu—kwamba Angemkabidhi Ayubu kwa Shetani. Kwa mkondo mmoja, hali hii ingethibitisha kwamba uangalizi na utathmini wa Mungu kwa Ayubu ulikuwa sahihi na bila kosa, na ungesababisha Shetani kuaibishwa kupitia kwa ushuhuda wa Ayubu, kwa mkondo mwingine, ingefanya imani ya Ayubu kwa Mungu na kumcha Mungu kuwa timilifu. Hivyo, wakati Shetani alipokuja mbele ya Mungu, Mungu hakutatiza maneno. Alienda moja kwa moja kwenye hoja na kumuuliza Shetani: “Je, umemwangalia mtumishi wangu Ayubu, kwa kuwa hakuna hata mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mnyofu, mwenye kumcha Mungu, na kuuepuka uovu?” Katika swali la Mungu kunayo maana yafuatayo: Mungu alijua kwamba Shetani alizunguka kila pahali, na mara nyingi alikuwa amemnyemelea Ayubu, aliyekuwa mtumishi wa Mungu. Alikuwa mara nyingi amemjaribu na kumshambulia, akijaribu kupata njia ya kumwangamiza Ayubu ili kuthibitisha kwamba imani ya Ayubu katika Mungu na kumcha Mungu kwake kusingeweza kubadilika. Shetani pia alitafuta kwa haraka sana fursa za kumhangaisha Ayubu, ili Ayubu aweze kumkataa Mungu na kumruhusu Shetani kumpokonya kutoka kwenye mikono ya Mungu. Lakini Mungu aliuangalia moyo wa Ayubu na kuona kwamba alikuwa mtimilifu na mnyofu, na kwamba alimcha Mungu na kujiepusha na maovu. Mungu alitumia swali moja kumwambia Shetani kwamba Ayubu alikuwa binadamu mtimilifu na mnyofu aliyemcha Mungu na kujiepusha na maovu, kwamba Ayubu asingeweza kumwacha Mungu na kufuata Shetani. Baada ya kusikia utathmini wa Mungu kuhusu Ayubu, ndani ya Shetani kukatokea hasira kali iliyotokana na udhalilishaji, na akawa mwenye hasira zaidi, na aliyekosa subira ya kumpokonya Ayubu kutoka kwa Mungu, kwani Shetani alikuwa hajawahi kusadiki kwamba mtu angeweza kuwa mtimilifu na mnyofu, au kwamba angeweza kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Wakati huohuo, Shetani pia alichukizwa na utimilifu na unyofu kwa binadamu, na aliwachukia watu ambao wangeweza kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Na hivyo imeandikwa katika Ayubu 1:9-11 kwamba “Kisha Shetani akamjibu BWANA, akasema, Je, Huyo Ayubu anamcha BWANA bure? Wewe hujamzingira kwa ukigo pande zote, na kwa nyumba yake, na vitu vyote alivyo navyo kwa kila upande? Umezibariki kazi za mikono yake, na mali yake imeongezeka katika nchi. Lakini nyosha mkono wako sasa, uyaguse hayo yote aliyo nayo, na yeye atakukufuru mbele ya uso wako.” Mungu alikuwa amezoea kwa undani asili ya kijicho ya Shetani, na Alijua vizuri kabisa kwamba Shetani alikuwa na mpango wa muda mrefu wa kumwangamiza Ayubu, na hivyo kwa haya Mungu alitaka, kwa kumwambia Shetani kwa mara nyingine kwamba Ayubu alikuwa mtimilifu na mnyofu na kwamba alimwogopa Mungu na kujiepusha na maovu, kumrudisha Shetani pale anapofaa, kumfanya Shetani kufichua uso wake wa kweli na kumshambulia na kumjaribu Ayubu. Kwa maneno mengine, Mungu alitilia mkazo makusudi kwamba Ayubu alikuwa mtimilifu na mnyofu na kwamba alimcha Mungu na kujiepusha na maovu, na kwa njia hii alimfanya Shetani kumshambulia Ayubu kwa sababu ya chuki na hasira za Shetani kutokana na vile ambavyo Ayubu alikuwa binadamu mtimilifu na mnyofu, yule aliyemcha Mungu na kujiepusha na maovu. Kutokana na haya, Mungu angemletea Shetani aibu kupitia kwa ukweli kwamba Ayubu alikuwa binadamu mtimilifu na mnyofu, yule aliyemcha Mungu na kujiepusha na maovu, na Shetani angeachwa akiwa amedhalilishwa kabisa na kushindwa. Baada ya hapo, Shetani asingekuwa tena na shaka au asingetoa mashtaka kuhusu utimilifu, unyofu, ucha Mungu au hali ya kujiepusha na maovu ya Ayubu. Kwa njia hii, majaribio ya Mungu na yale ya Shetani yalikuwa karibu yasiyoepukika. Yule tu aliye na uwezo wa kustahimili majaribio ya Mungu na yale ya Shetani alikuwa ni Ayubu. Kufuatia mabadilishano haya, Shetani alipewa ruhusa kumjaribu Ayubu. Na hivyo raundi ya kwanza ya mashambulizi ya Shetani ikaanza. Kilengwa cha mashambulizi haya kilikuwa mali ya Ayubu, kwani Shetani alikuwa ametoa mashtaka yafuatayo dhidi ya Ayubu: “Je, Huyo Ayubu anamcha BWANA bure?… Umezibariki kazi za mikono yake, na mali yake imeongezeka katika nchi.” Kutokana na haya, Mungu alimruhusu Shetani kuchukua kila kitu ambacho Ayubu alikuwa nacho— ambalo ndilo lilikuwa kusudio lenyewe la Mungu kuzungumza na Shetani. Hata hivyo, Mungu alitoa sharti moja kwa Shetani: “yote aliyo nayo yamo katika uwezo wako; lakini usinyoshe mkono wako juu yake yeye mwenyewe” (Ayubu 1:12). Hili ndilo sharti ambalo Mungu alitoa baada ya kumruhusu Shetani kumjaribu Ayubu na akamweka Ayubu kwenye mikono ya Shetani, na hiyo ndiyo mipaka aliyomwekea Shetani: Alimwamuru Shetani kutodhuru Ayubu. Kwa sababu Mungu alijua kwamba Ayubu alikuwa mtimilifu na mnyofu, na kwamba Alikuwa na imani kwamba utimilifu na unyofu wa Ayubu kwake Yeye ulikuwa zaidi ya kutiliwa shaka, na kwamba angeweza kustahimili majaribio; hivyo, Mungu alimruhusu Shetani kumjaribu Ayubu, lakini akaweka hapo kizuizi kwa Shetani: Shetani aliruhusiwa kuchukua mali ya Ayubu yote, lakini asimguse hata kwa kidole. Hii inamaanisha nini? Inamaanisha kwamba Mungu hakumkabidhi Ayubu kabisa kwa Shetani wakati huo. Shetani angeweza kumjaribu Ayubu kwa mbinu zozote zile ambazo alitaka, lakini hakuweza kumdhuru Ayubu mwenyewe, hata unywele mmoja wa kichwa chake, kwa sababu kila kitu cha binadamu kinathibitiwa na Mungu, iwapo binadamu anaishi ama anakufa inaamuliwa na Mungu na Shetani hana leseni yoyote ya kuthibiti haya. Baada ya Mungu kumwambia Shetani maneno haya, Shetani asingeweza kusubiri kuanza. Alitumia kila mbinu kumjaribu Ayubu, na baada ya muda usiyokuwa mrefu Ayubu alipoteza kundi kubwa la kondoo na ng'ombe na mali yote aliyokuwa amepewa na Mungu... Na hivyo majaribio ya Mungu yakamjia yeye.
Ingawa Biblia inatuambia asili ya jaribio la Ayubu, je Ayubu mwenyewe, ambaye alipatwa na majaribio haya, alijua kuhusu kile kilichokuwa kikiendelea? Ayubu alikuwa tu binadamu wa kawaida; bila shaka hakujua chochote kuhusu hadithi ile iliyokuwa ikiendelea nyuma yake. Hata hivyo, kumcha Mungu kwake na utimilifu pamoja na unyofu wake, ulimfanya kutambua kwamba majaribio ya Mungu yalikuwa yamemjia. Hakujua ni nini kilichokuwa kimefanyika kwenye ufalme wa kiroho, wala nia alizokuwa nazo Mungu katika majaribio hayo. Lakini alijua kwamba haijalishi ni nini ambacho kingemfanyikia yeye, alifaa kuendelea kushikilia ukweli wa utimilifu na unyofu wake, na kwamba alifaa kutii njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Mwelekeo na mwitikio wa Ayubu katika masuala haya uliweza kutazamwa waziwazi na Mungu. Naye Mungu aliona nini? Aliuona moyo wa Ayubu uliyomcha Mungu, kwa sababu kutoka mwanzo hadi wakati ambapo Ayubu alijaribiwa, moyo wa Ayubu ulibakia wazi kwa Mungu, uliwekwa mbele ya Mungu, naye Ayubu hakuwacha utimilifu wala unyofu wake, wala hakutupilia mbali au kugeuka katika njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu—na hakuna kingine chochote kilichokuwa cha kumtosheleza na kumfurahisha Mungu kama haya. Kisha, tutaangalia ni majaribio yapi aliyoyapitia Ayubu na ni vipi ambavyo aliyashughulikia majaribio haya. Hebu tuyasome maandiko.
c. Mwitikio wa Ayubu
(Ayubu 1:20-21) Kisha Ayubu akainuka, akalipasua joho lake, na akanyoa kichwa chake, na akaanguka chini, na kuabudu, Na akasema, nilitoka tumboni mwa mama yangu nikiwa uchi, nami nitarudi tena huko uchi vilevile; BWANA alinipa, na BWANA amechukua; jina la BWANA libarikiwe.

Kwamba Ayubu Anajiwajibikia Yeye Mwenyewe Kurudisha Kila Kitu Anachomiliki Kinatokana na Kumcha Kwake Mungu

Baada ya Mungu kumwambia Shetani, “yote aliyo nayo yamo katika uwezo wako; lakini usinyoshe mkono wako juu yake yeye mwenyewe.” Shetani aliondoka, muda mfupi baadaye Ayubu alipata mashambulizi ya ghafla na makali: Kwanza, ng'ombe na punda wake waliibwa na watumishi wake kuuwawa; kisha, kondoo na watumishi wake waliteketezwa hadi kiwango cha kuangamia; baada ya hapo ngamia wake walichukuliwa na watumishi wake wakauliwa; hatimaye watoto wake wa kiume na wa kike waliaga dunia. Msururu huu wa mashambulizi ulikuwa ni mateso ambayo alipitia Ayubu kwenye jaribio hili la kwanza. Kama alivyoamrishwa na Mungu, kwenye kipindi hiki cha mashambulizi, Shetani alilenga tu mali ya Ayubu na watoto wake, na hakumdhuru Ayubu mwenyewe. Hata hivyo, Ayubu alibadilishwa papo hapo kutoka kuwa mtu tajiri aliyemiliki utajiri mwingi hadi kuwa mtu asiye na chochote wala lolote. Hakuna yeyote ambaye angestahimili mshangao huu mkubwa au ambaye angeitikia vizuri, ilhali Ayubu aliuonyesha upande wake usio wa kawaida. Maandiko yanaelezea yafuatayo: “Kisha Ayubu akainuka, akalipasua joho lake, na akanyoa kichwa chake, na akaanguka chini, na kuabudu.” Huu ndio uliokuwa mwitikio wa kwanza wa Ayubu baada ya kusikia kwamba watoto wake walikuwa wameaga dunia na alikuwa amepoteza mali yake yote. Zaidi ya yote, hakuonekana ni kana kwamba ameshangazwa, au amepigwa na butwaa chakari, isitoshe hakuonyesha hasira au chuki. Unaona, basi, kwamba moyoni mwake alikuwa tayari ametambua kuwa majanga haya hayakuwa ajali, au yalitokana na mkono wa binadamu, na wala hayakuwa kuwasili kwa kuadhibiwa au adhabu. Badala yake, majaribio ya Yehova yalikuwa yamemjia yeye; alikuwa ni Yehova ambaye alitaka kuchukua mali na watoto wake. Ayubu alikuwa mtulivu na mwenye akili-razini wakati huo. Ubinadamu wake wa utimilifu na unyofu ulimwezesha yeye kuweza kufanya uamuzi na uamuzi kwa usahihi kwa njia ya kiasili na kirazini hasa, kuhusu majanga yaliyokuwa yamemsibu, na matokeo yake ni kuwa, alijiendeleza kwa utulivu usio wa kawaida. “Kisha Ayubu akainuka, akalipasua joho lake, na akanyoa kichwa chake, na akaanguka chini, na kuabudu.”“Rarua joho lake” inamaanisha kwamba alikuwa hana nguo, na hakumiliki chochote; “alikinyoa kichwa chake” inamaanishwa kwamba alikuwa amerudi mbele ya Mungu kama mtoto mchanga aliyezaliwa; “akaanguka ardhini, na kusujudu” inamaanisha alikuwa amekuja ulimwenguni akiwa uchi, na bado hakuwa na chochote leo, alirudishwa kwa Mungu kama mtoto mchanga aliyezaliwa. Mwelekeo wa Ayubu kwa yote yaliyompata usingeweza kutimizwa na kiumbe yeyote wa Mungu. Imani yake kwa Yehova ilizidi ile ufalme wa imani; huku kulikuwa ni kumcha Mungu kwake, kuwa mtiifu kwa Mungu, na hakuweza tu kutoa shukrani kwa Mungu kwa kumpa yeye lakini pia kuchukua kutoka kwake. Na zaidi ya hayo, aliweza kujiwajibikia yeye mwenyewe ili kurudisha yale yote aliyomiliki, pamoja na maisha yake.
Kumcha Mungu na utiifu wa Ayubu kwa Mungu ni mfano kwa mwanadamu, na utimilifu na unyofu wake ulikuwa ndio kilele cha ubinadamu unaofaa kumilikiwa na binadamu. Ingawaje hakumwona Mungu, alitambua kwamba Mungu kwa kweli alikuwepo, na kwa sababu ya utambuzi huu alimcha Mungu— na kutokana na kumcha Mungu kwake, aliweza kumtii Mungu. Alimpa Mungu hatamu bila malipo ili kuchukua chochote alichokuwa nacho, ilhali hakulalamika, na akaanguka chini mbele ya Mungu na kumwambia kwamba kwa wakati huohuo, hata kama Mungu angeuchukua mwili wake, angemruhusu yeye kufanya hivyo kwa furaha, bila malalamiko. Mwenendo wake wote ulitokana na ubinadamu wake timilifu na mnyofu. Hivi ni kusema, kutokana na kutokuwa na hatia kwake, uaminifu, na upole wake, Ayubu hakutikisika katika utambuzi wake na uzoefu wa uwepo wa Mungu na juu ya msingi huu aliweza kujitolea madai yeye mwenyewe na kuwastanisha kufikiria kwake, tabia, mwenendo, na kanuni za vitendo mbele ya Mungu kulingana na mwongozo wa Mungu kwake yeye na vitendo vya Mungu ambavyo alikuwa ameviona miongoni mwa mambo mengine yote. Baada ya muda, uzoefu wake ulimsababisha yeye kuwa na hali halisi na ya kweli ya kumcha Mungu na kumfanya pia kujiepusha na maovu. Hiki ndicho kilikuwa chanzo cha uadilifu ambao Ayubu alishikilia. Ayubu aliumiliki ubinadamu wa uaminifu, usio na hatia, na wa upole, na alikuwa na uzoefu halisi wa kumcha Mungu, kumtii Mungu na kujiepusha na maovu, pamoja na maarifa kwamba “BWANA alinipa, na BWANA amechukua.” Ni kwa sababu tu ya mambo haya ndiyo aliweza kusimama imara na kushuhudia katikati ya mashambulizi mabaya kama yale yaliyomsibu kutoka kwa Shetani, na ni kwa sababu tu ya hayo ndiyo aliweza kutomkasirisha Mungu na kutoa jibu la kutosheleza kwake Mungu wakati majaribio ya Mungu yalipomjia. Ingawaje mwenendo wa Ayubu kwenye jaribio la kwanza ulikuwa wa moja kwa moja, vizazi vya baadaye havikuwa na uhakika wa kutimiza hali hiyo ya moja kwa moja hata baada ya kutia bidii maisha yao yote, wala hawangemiliki kwa vyovyote vile mwenendo wa Ayubu uliofafanuliwa hapo juu. Leo, wakikabiliwa na mwenendo wa moja kwa moja wa Ayubu, na katika kuulinganisha na kilio na bidii ya “utiifu wenye hakika na uaminifu hadi kifo” ulioonyeshwa kwa Mungu na wale wanaodai kusadiki Mungu na kufuata Mungu, je unahisi aibu kwa kina au la?
Wakati unaposoma maandiko kuhusu yale mateso yote aliyopitia Ayubu na familia yake, mwitikio wako ni upi? Unapotea kwenye fikira zako? Unashangazwa? Je, majaribio haya yaliyomsibu Ayubu yanaweza kufafanuliwa kama ya “kusikitisha” Kwa maneno mengine, inatisha vya kutosha kuyasoma majaribio ya Ayubu kama yalivyofafanuliwa kwenye maandiko, kutosema chochote kuhusu vile yangekuwa katika uhalisia. Unaona, basi, kwamba kile kilichomsibu Ayubu hakikuwa “mazoezi,” lakini “vita,” halisi vikiwa na “bunduki” na “risasi” za kweli. Lakini nani alisababisha yeye kuweza kupitia majaribio haya ? Yaliweza, bila shaka, kutekelezwa na Shetani, yalitekelezwa na Shetani mwenyewe—lakini yaliidhinishwa na Mungu. Je, Mungu alimwambia Shetani kumjaribu Ayubu kwa njia gani? Hakumwambia. Mungu alimpa Shetani sharti moja tu, na baadaye jaribio hilo likamjia Ayubu. Wakati jaribio lilipomjia Ayubu, liliwapatia watu hisia ya maovu na ubaya wa Shetani, ya uoneaji kijicho wake, na uchukivu wake kwa binadamu, na uadui wake kwa Mungu. Katika haya tunaona kwamba maneno yasingeweza kufafanua namna tu ambavyo jaribio hili lilikuwa la kikatili. Inaweza kusemekana kwamba asili ya kijicho ambayo Shetani alimnyanyasa binadamu na uso wake mbaya vyote vilichuliwa kabisa kwa wakati huu. Shetani alitumia fursa hii, fursa iliyotolewa kupitia kwa ruhusa ya Mungu, kumnyanyasa Ayubu kwa njia mbaya na ya kusikitisha, mbinu na kiwango cha ukatili ambao haufikiriki na hauvumiliki kabisa na watu wa leo. Badala ya kusema kwamba Ayubu alijaribiwa na Shetani, na kwamba alisimama imara katika ushuhuda wake wakati wa jaribio hili, ni bora zaidi kusema kwamba katika majaribio hayo yaliyokuwa mbele yake kutoka kwa Mungu Ayubu alianza kuwa katika mapambano na Shetani ili kuulinda utimilifu na unyofu wake, kutetea njia yake ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Katika shindano hili, Ayubu alipoteza kundi kubwa la kondoo na ng'ombe, alipoteza mali yake yote na watoto wake wa kike na kiume —lakini hakuacha utimilifu, unyofu, au hali yake ya kumcha Mungu. Kwa maneno mengine, katika pigano hili na Shetani alipendelea kunyang'anywa mali na watoto kuliko kupoteza utimilifu, unyofu na hali yake ya kumcha Mungu. Alipendelea kushikilia mzizi wa maana ya kuwa binadamu. Maandiko yanatoa simulizi halisi kuhusu mchakato wote ambao Ayubu alipoteza rasilimali zake, na pia ukasimulia mwenendo na mwelekeo wa Ayubu. Simulizi hizi za mkato, na wazi zinatoa hisia kwamba Ayubu alikuwa karibu anao utulivu wakati akipitia jaribio hili, lakini kama kile kilichofanyika kwa hakika kingeundwa upya, na kuongeza asili yale ya kijicho ya Shetani—basi mambo yasingekuwa rahisi au mepesi kama yalivyofafanuliwa kwenye sentensi hizi. Uhalisia ulikuwa wenye ukatili zaidi. Hicho ndicho kiwango cha uharibifu na chuki ambacho Shetani hushughulikia mwanadamu na wale wote wanaoidhinishwa na Mungu. Kama Mungu asingekuwa amemwomba Shetani kutodhuru Ayubu, Shetani bila shaka angekuwa amemwua bila ya shaka. Shetani hataki mtu yeyote kumwabudu Mungu, wala hataki wale wenye haki mbele ya macho ya Mungu na wale walio timilifu na wanyofu kuweza kuendelea kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Kwa watu kumcha Mungu na kujiepusha maovu kunamaanisha kwamba wanajiepusha na kumwacha Shetani, na hivyo Shetani alitumia ruhusa ya Mungu kumlimbikizia hasira yake na chuki kwake Ayubu bila huruma. Unaona, basi, mateso aliyoyapitia Ayubu yalikuwa mengi sana, haya yalikuwa mengi kiasi gani ambayo Ayubu alipitia, kuanzia kwenye akili hadi kwenye mwili, kutoka nje hadi ndani. Leo, hatuoni namna ambavyo kwa wakati huu na tunaweza tu kupata kutoka kwenye simulizi za Biblia, mtazamo mfupi wa hisia za Ayubu wakati alipokuwa akipitia yale mateso wakati huo.

Kutotikisika kwa Uadilifu wa Ayubu Kunaleta Aibu Kwake Shetani na Kusababisha Shetani Kutoroka kwa Wasiwasi

Na ni nini ambacho Mungu alifanya wakati Ayubu alipopitia mateso haya? Mungu aliangalia, na kutazama, na Akasubiri matokeo. Wakati Mungu Alipokuwa akiangalia na kutazama, Alihisi vipi? Alihisi kuwa mwenye huzuni, bila shaka. Lakini, kutokana na huzuni Yake, Aliweza kujuta ruhusa Yake kwa Shetani ya kumjaribu Ayubu? Jibu ni, La, Asingefanya hivyo. Kwani Yeye alisadiki kwa dhati kwamba Ayubu alikuwa mtimilifu na mnyofu, kwamba alimcha Mungu na kujiepusha na maovu. Mungu alikuwa amempa Shetani tu fursa ya kuthibitisha uhaki wa Ayubu mbele ya Mungu, na kufichua maovu yake Shetani na hali ya kudharauliwa kwake binafsi. Ilikuwa, zaidi ya hapo, fursa ya Ayubu kutolea ushuhuda utakatifu wake na kumcha Mungu kwake na kujiepusha na maovu mbele ya watu wa ulimwengu, Shetani, na hata wale wanaomfuata Mungu. Je, matokeo ya mwisho yalithibitisha kwamba ukadiriaji wa Mungu kuhusu Ayubu ulikuwa sahihi na bila makosa? Je, Ayubu alimshinda kweli Shetani? Hapa tunasoma kuyahusu maneno yale halisi yaliyozungumzwa na Ayubu, maneno ambayo ni thibitisho kwamba alikuwa amemshinda Shetani. Alisema: “Nilitoka tumboni mwa mama yangu nikiwa uchi, nami nitarudi tena huko uchi vilevile.”Huu ndio mwelekeo wa utiifu ambao Ayubu anao kwa Mungu. Kisha, akasema: “BWANA alinipa, na BWANA amechukua; jina la BWANA libarikiwe..” Maneno haya yaliyozungumzwa na Ayubu yanathibitisha kwamba Mungu anaangalia kina cha moyo wa binadamu, kwamba Anaweza kuangalia kwenye akili ya binadamu, na yanathibitisha kwamba kuidhinisha kwake kwa Ayubu hakuna kosa, kwamba binadamu huyu aliyeidhinishwa na Mungu alikuwa mwenye haki. “…BWANA alinipa, na BWANA amechukua; jina la BWANA libarikiwe.”Maneno haya ni ushuhuda wa Ayubu kwa Mungu. Yalikuwa maneno haya ya kawaida yaliyomfanya Shetani kuogopa, yaliyoleta aibu kwake na kumsababisha kutoroka kwa wasiwasi, na, vilevile, yaliyomfunga pingu Shetani na kumuacha bila rasilimali zozote. Hivyo, pia, ndivyo maneno haya yalivyomfanya Shetani kuhisi matendo ya kustaajabisha na yenye nguvu ya Yehova Mungu, na kumruhusu kuelewa haiba kubwa na isiyo ya kawaida ya yule ambaye moyo wake ulitawaliwa na njia ya Mungu. Zaidi, yalionyesha Shetani nguvu za kipekee zilizoonyeshwa na mtu mdogo asiyekuwa na umuhimu wowote katika kutii njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu Shetani hivyo basi alishindwa kwenye shindano la kwanza. Licha ya utambuzi wake “uliopatikana kwa hali ngumu,” Shetani hakuwa na nia ya kumwachilia Ayubu, wala hakukuwa na badiliko lolote katika asili yake ya unafiki. Shetani alijaribu kuendelea kumshambulia Ayubu, na kwa mara nyingine tena akamjia Mungu …
Kisha, hebu tuyasome maandiko kuhusu mara ya pili ambapo Ayubu alijaribiwa.
3. Shetani Amjaribu Ayubu Mara Nyingine Tena (Majipu Mabaya Yaupiga Mwili wa Ayubu)
a. Maneno Yaliyotamkwa na Mungu
(Ayubu 2:3) BWANA akamwuliza Shetani, je, umemwangalia mtumishi wangu Ayubu, kwa kuwa hakuna hata mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mnyofu, mwenye kumcha Mungu, na kuuepuka uovu; naye hata sasa anashikamana na utimilifu wake, ujapokuwa ulinichochea dhidi yake, ili nimwangamize pasipo sababu.
(Ayubu 2:6) BWANA akamwambia Shetani, Tazama, yeye yumo mkononi mwako; lakini uutunze uhai wake.
b. Maneno Yaliyotamkwa na Shetani
(Ayubu 2:4-5) Shetani akamjibu BWANA, na kusema, Ngozi kwa ngozi, naam, yote aliyo nayo mtu atayatoa kwa ajili ya uhai wake. Lakini sasa nyosha mkono wako, uuguse mfupa wake na nyama yake, naye atakukufuru mbele ya uso wako.
c. Namna Ayubu Anavyoshughulikia Majaribio
(Ayubu 2:9-10) Kisha mkewe akamwambia, Je, Wewe bado unashikamana na utimilifu wako? mkufuru Mungu, ufe. Lakini yeye akamwambia, Wewe unazungumza kama mmoja wa wanawake wapumbavu wanavyozungumza. Vipi? Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya? Katika yote haya Ayubu hakufanya dhambi kwa midomo yake.
(Ayubu 3:3) ) Itokomee mbali ile siku niliyozaliwa, na ule usiku uliosema, Mtoto mume ameingia katika mimba.

Upendo wa Ayubu ya Njia ya Mungu Inazidi Yoyote Ile Nyingine

Maandiko yanarekodi maneno haya yaliyozungumzwa kati ya Mungu na Shetani: “BWANA akamwuliza Shetani, je, umemwangalia mtumishi wangu Ayubu, kwa kuwa hakuna hata mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mnyofu, mwenye kumcha Mungu, na kuuepuka uovu; naye hata sasa anashikamana na utimilifu wake, ujapokuwa ulinichochea dhidi yake, ili nimwangamize pasipo sababu” (Ayubu 2:3). Katika maneno haya Mungu Anarudia swali moja kwa Shetani. Ni swali linalotuonyesha ukadiriaji wa uthibitisho wa Yehova Mungu kuhusu kile kilichoonyeshwa na kuishi na kudhihirishwa na Ayubu kwenye jaribio lake la kwanza, na ule ambao si tofauti na ukadiriaji wa Mungu wa Ayubu kabla ya kupitia jaribio lile la Shetani. Hivi ni kusema, kabla jaribio halijamfika, katika macho ya Mungu Ayubu alikuwa mtimilifu, na hivyo basi Mungu Alimlinda yeye na familia yake, na Akambariki, alistahili kubarikiwa kwa macho ya Mungu. Baada ya jaribio, Ayubu hakutenda dhambi kwa midomo yake kwa sababu alikuwa amepoteza mali yake na watoto wake, lakini aliendelea kulisifu jina la Yehova. Mwenendo wake halisi ulimfanya Mungu kumpongeza, na kumpa alama zote. Kwani machoni mwa Ayubu, watoto wake au rasilimali zake hazikutosha kumfanya yeye kumkataa Mungu. Nafasi ya Mungu katika moyo wake, kwa maneno mengine, isingeweza kusawazishwa na watoto wake au kipande chochote cha mali yake. Kwenye jaribio la kwanza la Ayubu, alimwonyesha Mungu kwamba upendo wake kwake na upendo wake wa njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu ulizidi kila kitu kingine. Ni kwa sababu tu jaribio hili lilimpa Ayubu uzoefu wa kupokea tuzo kutoka kwa Yehova Mungu na kufanya mali yake na watoto wake kuchukuliwa na Yeye.
Kwa Ayubu, hali hii aliyoipitia ilikuwa ya kweli na ambayo ilisafisha nafsi yake ikawa safi, ulikuwa ni ubatizo wa maisha uliotimiza uwepo wake, na, isitoshe, ilikuwa ni karamu ya kutosha iliyojaribu utiifu wake kwa, na yeye kumcha Mungu. Jaribio hili lilibadilisha hadhi ya Ayubu kutoka ule wa bwana tajiri hadi kwa mtu ambaye hakuwa na chochote, na pia likamruhusu kupitia dhuluma za shetani kwa mwanadamu. Ufukara wake haukumfanya kuchukia Shetani; badala yake, kwenye vitendo vibovu vya Shetani aliuona ubaya na hali ya kudharau ya Shetani pamoja na uadui wa Shetani na uasi wake kwa Mungu, na hali hii ilimhimiza vizuri zaidi kushikilia daima njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Aliapa kwamba asingewahi kumwacha Mungu na kugeuka njia ya Mungu kwa sababu ya mambo ya nje kama vile mali, watoto au urithi, wala hangewahi kuwa mtumwa wa Shetani, mali, au mtu yeyote; mbali na Yehova Mungu, hakuna mtu ambaye angekuwa Bwana wake, au Mungu wake. Hayo ndiyo yaliyokuwa maazimio ya Ayubu. Kwa upande mwingine wa jaribio, Ayubu alikuwa pia amepata jambo jingine: Alikuwa amepata utajiri mkubwa katikati ya majaribio hayo aliyoyapitia kutoka kwa Mungu.
Wakati wa maisha yake katika miongo kadhaa iliyopita, Ayubu aliyaona matendo ya Yehova na kupata baraka za Yehova Mungu kwake yeye. Zilikuwa ni baraka zilizomwacha akihisi wasiwasi mkubwa na mwenye wingi wa shukrani, kwani aliamini kwamba alikuwa hajamfanyia chochote Mungu, ilhali alikuwa amepata baraka nyingi na akawa anafurahia neema nyingi. Kwa sababu hii, ndani ya moyo wake mara nyingi aliomba, akitumai angeweza kumlipa Mungu, akitumai kwamba angekuwa na fursa ya Kuwa na ushuhuda wa matendo na ukubwa wa Mungu , na kutumai kwamba Mungu angeweza kuujaribu utiifu wake, na, zaidi, kwamba imani yake ingetakaswa, mpaka pale ambapo utiifu wake na imani yake vyote vingepata idhini ya Mungu. Na wakati Ayubu alipojaribiwa, alisadiki kwamba Mungu alikuwa amesikia maombi yake. Ayubu alifurahia sana fursa hii zaidi ya kitu kingine chochote, na hivyo basi hakuthubutu kuchukulia jambo hili vivi hivi, kwani tamanio kubwa zaidi la maisha yake lingetimia. Kufika kwa fursa hii kulimaanisha kwamba utiifu wake na kumcha Mungu vyote vingeweza kutiwa kwenye majaribu, na kutakaswa. Zaidi, ilimaanisha kwamba Ayubu alikuwa na fursa ya kupata idhini ya Mungu, hivyo kumleta karibu zaidi na Mungu. Wakati wa jaribio, imani kama hiyo na kufuatilia huko kulimruhusu yeye kuwa mtimilifu zaidi, na kupata uelewa mkubwa zaidi wa mapenzi ya Mungu. Ayubu alikuwa mwenye shukrani zaidi kwa baraka na neema za Mungu, katika moyo wake alimwaga sifa kubwa zaidi kwa matendo ya Mungu, na alizidi kumcha Mungu na kumstahi, na kutamani hata zaidi upendo, ukubwa, na utakatifu wa Mungu. Wakati huu, ingawaje Ayubu alikuwa bado yuleyule aliyemcha Mungu na kujiepusha na maovu kwenye macho ya Mungu, kuhusiana na yale aliyopitia, imani na maarifa ya Ayubu vyote vilikuwa vimeimarika pakubwa: Imani yake ilikuwa imeongezeka, utiifu wake ulikuwa umeimarika pakubwa, na hali yake ya kumcha Mungu ilikuwa ya kina zaidi. Ingawaje jaribio hili lilibadilisha roho na maisha ya Ayubu, mabadiliko kama hayo hayakumtosheleza Ayubu, wala hayakufanya maendeleo yake ya kwenda mbele kwenda polepole. Wakati huo, akiwa anapiga hesabu kile alichokuwa amepata kutoka kwenye jaribio hilo, na akitilia maanani upungufu wake binafsi, aliomba kimyakimya, akisubiri jaribio linalofuata ambalo lingemsibu yeye, kwa sababu alitamani sana, imani, utiifu, na kumcha Mungu kwake kuweze kuimarishwa kwenye jaribio linalofuata la Mungu.
Mungu Anaziangalia fikira za ndani zaidi za binadamu na yale yote ambayo binadamu anasema na kufanya. Fikira za Ayubu zilifikia masikio ya Yehova Mungu, na Mungu alisikiliza maombi yake na kwa njia hii jaribio la Mungu kwa Ayubu lililofuata liliwasili kama lilivyotarajiwa.

Katikati ya mateso makuu, Ayubu Anatambua kwa kweli utunzaji wa Mungu kwa mwanadamu

Kufuatia maswali ya Yehova Mungu kwa Shetani, Shetani alifurahi kisirisiri. Kwa sababu Shetani alijua kwamba angeweza kwa mara nyingine kuruhusiwa kumshambulia mtu aliyekuwa mtimilifu katika macho ya Mungu—jambo ambalo kwa Shetani lilikuwa fursa ya nadra. Shetani alitaka kutumia fursa hii kudhalilisha kabisa kujitolea kwa Ayubu kumfanya kupoteza imani yake kwa Mungu na hivyo basi kutomcha Mungu tena au kubariki jina la Yehova. Hali hii ingempa Shetani fursa: Haijalishi ni wapi au ni muda gani, angeweza kumfanya Ayubu kuwa kikaragosi cha kufuata amri zake. Shetani alificha njama zake za maovu bila kuacha alama, lakini hakuweza kudhibiti asili yake ya maovu. Ukweli huu unaashiriwa kupitia kwa majibu yake kwa maneno ya Yehova Mungu, kama yalivyorekodiwa kwenye maandiko. “Shetani akamjibu BWANA, na kusema, Ngozi kwa ngozi, naam, yote aliyo nayo mtu atayatoa kwa ajili ya uhai wake. Lakini sasa nyosha mkono wako, uuguse mfupa wake na nyama yake, naye atakukufuru mbele ya uso wako” (Ayubu 2:4-5). Haiwezekani kutopata maarifa makuu na hali ya kuonea kijicho ya Shetani kutokana na mabadilishano haya kati ya Mungu na Shetani. Baada ya kusikia uongo huu wa Shetani, wale wote wanaoupenda ukweli na kuchukia uovu bila shaka watakuwa na chuki kubwa zaidi kwa utwezo na kutokuwa na aibu kwa Shetani, watahisi wakiwa wametishika na kusinyika kutokana na uongo wa Shetani, na, wakati huohuo, watatoa maombi yao ya kina na heri zao za dhati kwa Ayubu, wakiomba kwamba binadamu huyu mwenye unyofu ataweza kutimiza utimilifu wake, wakitamani kwamba binadamu huyu anayemcha Mungu na kujiepusha na maovu aweze kushinda milele majaribio ya Shetani, na kuishi kwa mwangaza, na kuishi katikati ya mwongozo na baraka za Mungu, hivyo, pia ndivyo watakavyotaka matendo ya haki ya Ayubu yaweze milele kuenea na kuhimiza wale wanaofuatilia njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na Shetani. Ingawaje nia ya kijicho ya Shetani inaweza kuonekana kupitia kwa tangazo hili, Mungu alikubali kwa urahisi “ombi” la Shetani — lakini alikuwa pia na sharti moja: “yeye yumo mkononi mwako; lakini uutunze uhai wake” (Ayubu 2:6). Kwa sababu, wakati huu, Shetani aliomba kunyosha mbele mkono wake ili kudhuru mwili na mifupa ya Ayubu, Mungu Alisema, “lakini okoa maisha yake.” Maana ya maneno haya ni kwamba alimpa Shetani mwili wa Ayubu, lakini Akabakiza maisha yake. Shetani asingeweza kuyachukua maisha ya Ayubu, lakini isipokuwa haya angeweza kutumia njia au mbinu zozote dhidi ya Ayubu.
Baada ya kupata ruhusa kutoka kwa Mungu, Shetani alimkimbilia Ayubu na kunyosha mbele mkono wake ili kuathiri ngozi yake na akamsababishia majipu mabaya yaliyoupiga mwili wake wote, naye Ayubu akahisi maumivu kwenye ngozi yake. Ayubu aliyasifu maajabu na utakatifu wa Yehova Mungu, jambo ambalo lilimfanya Shetani hata kuwa wazi zaidi katika ufidhuli wake. Kwa sababu alikuwa amehisi furaha ya kumwumiza binadamu, Shetani aliunyosha mkono wake na akakwaruza nyama ya Ayubu, na kusababisha majipu yake mabaya kutunga usaha.. Mara moja Ayubu alihisi maumivu na mateso kwenye mwili wake ambayo hayakuwa na kifani, na asingeweza kujisaidia kwa vyovyote vile isipokuwa kujikanda yeye mwenyewe kutoka kwenye kichwa hadi miguu akitumia mikono yake, ni kana kwamba kufanya hivi kungetuliza balaa ile iliyofanyikia roho yake kutokana na maumivu haya ya nyama za mwili wake. Alitambua kwamba Mungu Alikuwa kando yake akimwangalia, na akajaribu kwa njia bora zaidi kujituliza. Kwa mara nyingine alipiga magoti kwenye ardhi, na kusema: Unaangalia ndani ya binadamu, unauona umaskini wake; kwa nini unyonge wake unakuhusu wewe? Jina la Yehova Mungu lisifiwe. Shetani aliyaona yale maumivu yasiyovumilika ya Ayubu, lakini hakumwona Ayubu akiliacha neno la Yehova Mungu. Hivyo aliunyoosha haraka haraka mkono wake mbele ili kudhuru mifupa ya Ayubu, akiwa na tamaa ya kudhuru kila kiungo cha mwili wake. Mara, Ayubu akahisi mateso asiyoyatarajia; ni kana kwamba mwili wake ulikuwa umepasuliwa katikati kutoka kwenye mifupa, na kana kwamba mifupa yake ilikuwa ikipasuliwa kipande hadi kipande. Mateso haya ya kuumiza yalimfanya akafikiria afadhali basi afe. …uwezo wake wa kuvumilia ulikuwa umefikia kilele. … Alitaka kulia kwa sauti, alitaka kuirarua ngozi kwenye mwili wake ili kupunguza maumivu—lakini alishikilia mayowe yake, na hakuirarua ngozi yake kutoka kwenye mwili wake, kwani hakutaka Shetani auone udhaifu wake. Na hivyo alipiga magoti chini kwa mara nyingine, lakini wakati huu hakuhisi uwepo wa Yehova Mungu. Alijua kwamba mara nyingi alikuwa mbele yake, na nyuma yake, na upande wake. Lakini kwenye maumivu haya, Mungu alikuwa hajawahi kuyatazama; Aliufunika uso wake na Akawa Amefichwa, kwa maana uumbaji wake wa binadamu haukuwa wa kumletea mateso binadamu. Wakati huu, Ayubu alikuwa akilia, na akijaribu kwa njia bora zaidi kuvumilia maumivu yake ya kimwili, lakini asingeweza kujizuia tena dhidi ya kutoa shukrani kwa Mungu: Binadamu aanguka kwa mpigo wa kwanza, yeye ni myonge na asiye na nguvu, yeye ni mchanga na asiyejua—kwa nini ukataka kumtunza na kuwa mzuri kwake yeye? Unanipiga, ilhali inakuumiza kufanya hivyo. Ni nini cha binadamu kinastahili utunzaji na kujali Kwako? Maombi ya Ayubu yalifikia masikio ya Mungu, na ya Mungu Alikuwa kimya, Akitazama tu bila kutoa sauti. … Akiwa amejaribu kila ujanja kwenye kitabu bila mafanikio, Shetani aliondoka kimyakimya, lakini haya hayakufikisha hadi tamati majaribio ya Ayubu kutoka kwa Mungu. Kwa sababu nguvu za Mungu zilizokuwa zimefichuliwa ndani ya Ayubu zilikuwa hazijajulikana kwa umma, hadithi ya Ayubu haikuishia pale ambapo Shetani alijiondoa. Huku wahusika wengine wakiingia katika tukio hilo, matukio mengine ya ajabu zaidi yalikuwa yaje.

Maonyesho Mengine ya Kumcha Mungu na Kujiepusha na Maovu kwa Ayubu ni Kutukuza Kwake kwa Jina la Mungu Katika Mambo Yote

Ayubu alikuwa ameteseka kutokana na maudhi ya Shetani, lakini bado hakuliacha jina la Yehova Mungu. Mke wake ndiye aliyekuwa wa kwanza kujiondoa na kuendeleza wajibu wa Shetani unaoweza kuonekana kwa kumshambulia Ayubu. Maandishi asilia yanafafanua hali hii hivyo basi: “Kisha mkewe akamwambia, Je, Wewe bado unashikamana na utimilifu wako? mkufuru Mungu, ufe.” (Ayubu2:9). Haya yalikuwa maneno yaliyozungumzwa na Shetani akisingizia kuwa binadamu. Yalikuwa ni shambulizi, na shtaka, pamoja na kichocheo, jaribio, na matusi. Baada ya kushindwa kushambulia mwili wa Ayubu, Shetani sasa alishambulia moja kwa moja uadilifu wa Ayubu, akitaka kutumia jambo hili kumfanya Ayubu kutupilia mbali uadilifu wake, kumwacha Mungu, na kusita kuishi. Hivyo, pia, ndivyo Shetani alivyotaka kutumia maneno kama hayo kumjaribu Ayubu: Kama Ayubu angeacha jina la Yehova, asingelazimika kuvumilia mateso kama hayo, angejiondolea mateso ya mwili. Akiwa amekabiliwa na ushauri wa mke wake, Ayubu alimkosoa kwa kusema, “Lakini yeye akamwambia, Wewe unazungumza kama mmoja wa wanawake wapumbavu wanavyozungumza. Vipi? Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya?” (Ayubu 2:10). Ayubu alikuwa amejua kwa muda mrefu maneno haya, lakini wakati huu ukweli wa maarifa ya Ayubu kuhusu maneno haya ulikuwa umethibitishwa.
Wakati mke wake alimshauri kulaani Mungu na kufa, maana yake ilikuwa: Mungu wako anakushughulikia hivi, kwa hivyo kwa nini usimlaani yeye? Kama ungali hai unafanya nini? Mungu wako hakufanyii haki, na ilhali ungali unabariki jina la Yehova. Angekuleteaje janga hili huku unabariki jina Lake? Harakisha na uliache jina la Mungu, na usimfuate yeye tena. Kwa njia hii matatizo yako yataisha. Kwa wakati huu, ushuhuda ulitolewa ambao Mungu alitaka kuuona kwa Ayubu. Hakuna mtu yeyote wa kawaida ambaye angeweza kuwa na ushuhuda huu, wala hatuusomi katika mojawapo ya hadithi za Biblia—lakini Mungu Alikuwa ameuona mapema kabla hata Ayubu kuongea maneno haya. Mungu Alitaka tu kutumia fursa hii kumruhusu Ayubu kuthibitisha kwa wote kwamba Mungu alikuwa sahihi. Akiwa amekabiliwa na ushauri wa mke wake, Ayubu hakutupilia tu mbali uadilifu wake au kumuacha Mungu, bali pia alimwambia mke wake: “Vipi? Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya?” Je, maneno haya yanao uzito mkuu? Hapa, kunayo ukweli mmoja tu unaoweza kuthibitisha uzito wa maneno haya. Uzito wa maneno haya ni kwamba yameidhinishwa na Mungu ndani ya moyo Wake, ndiyo yale yaliyotamaniwa na Mungu, ndiyo yale Mungu Alitaka kusikia, na ndiyo matokeo ambayo Mungu Alitamani kuona; maneno haya ndiyo pia kiini cha ushuhuda wa Ayubu. Katika haya, utimilifu, unyofu, kumcha Mungu, kujiepusha na maovu kwa Ayubu kulithibitishwa. Thamani ya Ayubu ilikuwa namna ambavyo, alipojaribiwa, na hata wakati mwili wake mzima ulikuwa umefunikwa na majipu mabaya, alipovumilia mateso ya kiwango cha juu zaidi, na wakati mke na watu wake wa ukoo walipomshauri, bado aliyatamka maneno hayo. Ili niweze kuiweka kwa njia nyingine, ndani ya moyo wake alisadiki kwamba, haijalishi ni kiasi kipi cha majaribio, au ni vipi ambavyo masaibu au mateso yalivyokuwa, hata kama kifo kingemjia, hangemuacha Mungu au kugeuka na kuacha kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Unaona, basi, kwamba Mungu Alishikilia sehemu muhimu sana ndani ya moyo wake, na kwamba kulikuwa tu na Mungu moyoni mwake. Ni kwa sababu ya haya ndipo tunasoma ufafanuzi kama huo kuhusu yeye katika maandiko kama: Katika yote haya Ayubu hakufanya dhambi kwa midomo yake. Hakutenda dhambi kwa kutumia mdomo wake tu, lakini ndani ya moyo wake hakulalamika katu kuhusu Mungu. Hakusema maneno mabaya kuhusu Mungu, wala hakutenda dhambi dhidi ya Mungu. Kinywa chake hakikubariki tu jina la Mungu, lakini ndani ya moyo wake alibariki pia jina la Mungu; mdomo na moyo wake ulikuwa kitu kimoja. Huyu ndiye aliyekuwa Ayubu wa kweli aliyeonekana na Mungu, na hii ndiyo iliyokuwa sababu ya kweli kwa nini Mungu alimthamini sana Ayubu.

Kutoelewa Kwingi Kwa Watu Kuhusu Ayubu

Ugumu aliopitia Ayubu haukuwa kazi ya malaika waliotumwa na Mungu, wala haukusababishwa na mkono wa Mungu mwenyewe. Badala yake, ulisababishwa na Shetani mwenyewe, adui wa Mungu. Hivyo basi, kiwango cha ugumu alioupitia Ayubu kilikuwa kikubwa. Ilhali kwa wakati huo Ayubu alionyesha, kwa moyo mkunjufu, maarifa yake ya kila siku kumhusu Mungu ndani ya moyo wake, kanuni za vitendo vyake vya kila siku, na mwelekeo wake kwa Mungu—na huu ndio ukweli. Kama Ayubu hangekuwa amejaribiwa, kama Mungu Asingekuwa Amemletea Ayubu majaribio, wakati Ayubu aliposema, “BWANA alinipa, na BWANA amechukua; jina la BWANA libarikiwe,” ungesema kwamba Ayubu alikuwa mnafiki; Mungu alikuwa amempa rasilimali nyingi, hivyo bila shaka alilibariki jina la Yehova. Kama, kabla ya kupitia majaribio, Ayubu angekuwa amesema, “Vipi? Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya?” Ungesema kwamba Ayubu alikuwa akipiga chuku, na kwamba hangeliacha jina la Mungu kwa sababu mara nyingi alibarikiwa kwa mkono wa Mungu. Kama Mungu Angekuwa Amemletea janga, basi kwa kweli angeliacha jina la Mungu. Lakini wakati Ayubu alipojipata katika hali hizi ambazo hakuna yeyote angetaka kujipata ndani au kutaka kuona, au kutaka zimpate, ambazo watu wangeogopa kupata, hali ambazo hata Mungu mwenyewe Hakuweza kuvumilia kuzitazama, bado Ayubu aliweza kushikilia uadilifu wake: “BWANA alinipa, na BWANA amechukua; jina la BWANA libarikiwe” na “Vipi? Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya??” Kama wangekumbwa na mwenendo wa Ayubu wakati huu, wale wanaopenda kuzungumzia maneno ya kuonyesha umuhimu na kuvutia, na wale wanaopenda kuongea barua na mafundisho ya dini, wanaachwa wanyamavu. Wale wanaotukuza jina la Mungu kwa matamshi pekee, ilhali hawajawahi kukubali majaribio ya Mungu, wanashutumiwa na uadilifu ambao Ayubu alishikilia kwa dhati, na wale ambao hawajawahi kusadiki kwamba binadamu anaweza kushikilia kwa dhati njia ya Mungu wanahukumiwa na ushuhuda wa Ayubu. Wakiwa wamekabiliwa na mwenendo wa Ayubu wakati wa majaribio haya na maneno aliyoyaongea, baadhi ya watu watahisi wakiwa wamechanganyikiwa, baadhi watamwonea wivu, baadhi wahisi shaka, baadhi wataonekana hata wasio na haja ya kufuatilia mambo haya, huku wakiukataa ushuhuda wa Ayubu kwa sababu hawayaoni tu mateso yaliyompata Ayubu wakati wa majaribio, na kusoma maneno yaliyozungumzwa na Ayubu, lakini pia ule “unyonge” wa binadamu uliofichuliwa na Ayubu wakati majaribio yalipomsibu. “Unyonge” huu wanaoamini kuwa ile hali ya kudaiwa ya kutokuwa mtimilifu katika utimilifu wa Ayubu, doa katika binadamu ambaye katika macho ya Mungu alikuwa mtimilifu. Hivi ni kusema kwamba, inasadikiwa kwamba wale walio watimilifu hawana doa wala toa, hawana dosari wala hila, kwamba hawana unyonge wowote, hawana habari yoyote kuhusu maumivu, kwamba hawahisi katu wakiwa wamehuzunika au wamekataliwa, na hawana chuki au tabia yoyote ya nje isiyofaa; kutokana na haya, watu wengi hawasadiki kwamba Ayubu alikuwa kwa kweli mtimilifu. Watu hawaidhinishi mambo mengi kuhusu tabia yake wakati wa majaribio yake. Kwa mfano, wakati Ayubu alipopoteza mali yake na watoto wake, hakuweza, kama vile watu wanavyofikiria, kuanza kulia. “Utovu wake wa adabu” unawafanya watu kufikiria alikuwa jiwe, kwani hakuwa na machozi wala upendo kwa familia yake. Hii ndiyo picha mbaya ya kwanza ambayo Ayubu anawaonyesha watu. Wanafikiri tabia yake baada ya hapo kuwa ya kushangaza zaidi: “Kulirarua joho lake” ni kauli iliyotafsiriwa na watu kuonyesha utovu wake wa heshima kwa Mungu, na “kunyoa kichwa chake” kunasadikiwa visivyo kumaanisha kukufuru kwa Ayubu na upinzani wake kwa Mungu. Mbali na maneno ya Ayubu kwamba “BWANA alinipa, na BWANA amechukua; jina la BWANA libarikiwe,” watu hawatambui uhaki wowote ndani ya Ayubu uliosifiwa na Mungu, na hivyo ukadiriaji kuhusu Ayubu kwa wengi wao si chochote zaidi ya kutofahamu, kutoelewa, shaka, lawama, na idhinisho kwa nadharia tu. Hakuna kati yao anayeweza kuelewa na kushukuru kwa kweli maneno ya Yehova Mungu kwamba Ayubu alikuwa binadamu mtimilifu na mnyofu, yule aliyemcha Mungu na kujiepusha na maovu.
Kutokana na picha yao kuhusu Ayubu hapo juu, watu wana shaka zaidi kuhusiana na uhaki wake, kwani vitendo na mwenendo wa Ayubu uliorekodiwa kwenye maandiko haukuwa wenye mguso wa kina kama vile watu wangefikiria. Hakutekeleza tendo lolote kubwa tu, lakini pia alikichukua kigae ili ajikwaruze akiwa ameketi kwenye jivu. Kitendo hiki kinawashangaza pia watu na kuwafanya kutilia shaka—na hata kukataa—uhaki wa Ayubu, kwani wakati akijikwaruza Ayubu hakumwomba Mungu, au kutoa ahadi kwa Mungu; wala, zaidi ya hayo, hakuonekana akilia machozi ya maumivu. Wakati huu, watu wanauona tu unyonge wa Ayubu na wala sio chochote kingine, na hivyo hata wanapomsikia Ayubu akisema “Vipi? Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya? hawaguswi kamwe, au vinginevyo hawaonekani kuamua chochote, na bado hawawezi kutambua uhaki wa Ayubu kutoka kwa maneno haya. Picha ya kimsingi ambayo Ayubu anapatia watu wakati wa mateso ya majaribio yake ni kwamba alikuwa si mnyenyekevu wala mwenye kiburi. Watu hawaioni hadithi inayotokana na tabia yake iliyojitokeza katika kina cha moyo wake, wala hawaioni ile hali yake ya kumcha Mungu ndani ya moyo wake au kutii kwa kanuni ya njia ya kujiepusha na maovu. Utulivu wake unawafanya watu kufikiria kuwa utimilifu na unyofu wake vyote vilikuwa ni maneno matupu tu, kwamba kumcha kwake Mungu kulikuwa tu uvumi; ule “unyonge” alioufichua kwa nje, wakati huo, unawaachia picha ya kina, ukiwapatia “mtazamo mpya” kuhusu, na hata “uelewa mpya” kuhusu binadamu yule ambaye Mungu anafafanua kuwa mtimilifu na mnyofu. “Mtazamo mpya” na “uelewa mpya” kama huo vyote vinathibitishwa wakati Ayubu alipokifungua kichwa chake na kulaani siku aliyozaliwa.
Ingawaje kiwango cha mateso aliyoyapitia hakifikiriki wala kufahamika kwa binadamu yeyote, hakuzungumza maneno yoyote ya uvumi, lakini alipunguza tu maumivu ya mwili wake kwa njia zake mwenyewe. Kama ilivyorekodiwa kwenye maandiko, alisema: “Itokomee mbali ile siku niliyozaliwa, na ule usiku uliosema, Mtoto mume ameingia katika mimba.” (Ayubu3:3). Pengine, hakuna yeyote aliyewahi kutilia maanani maneno haya na kuona kwamba ni muhimu, na pengine kunao watu ambao wameyatilia maanani. Kwa maoni yako, yanamaanisha kwamba Ayubu alimpinga Mungu? Je, ni malalamiko dhidi ya Mungu? Najua kwamba wengi wenu mnayo mawazo fulani kuhusu maneno haya yaliyozungumzwa na Ayubu na mnasadiki kwamba kama Ayubu alikuwa mtimilifu na mnyofu, hakufaa kuonyesha unyonge wowote au huzuni yoyote, na badala yake alifaa kukabiliana vilivyo na shambulizi lolote kutoka kwa Shetani kwa njia nzuri, na hata kutabasamu wakati alikumbwa na majaribio ya Shetani. Hakufaa kuwa na mwitikio hata mdogo kuhusiana na mateso aliyoyapata kwenye mwili wake kutokana na Shetani, wala hakufaa kuonyesha hisia zozote ndani ya moyo wake. Alifaa hata kuuliza kwamba Mungu Ayafanye majaribio haya kuwa mabaya zaidi. Haya ndiyo yanayofaa kuonyeshwa na kumilikiwa na mtu ambaye hatikisiki na ambaye anamcha Mungu kwa kweli na kujiepusha na maovu. Katikati ya mateso haya makuu, Ayubu hakufanya chochote ila kulaani siku aliyozaliwa. Hakulalamika kuhusu Mungu, hakuwa na nia yoyote ya kumpinga Mungu. Hali hii ni rahisi zaidi ikisemwa kuliko kutendwa, kwani tangu enzi za zamani hadi wa leo, hakuna yeyote ambaye amewahi kupitia majaribio kama hayo au kuteseka kama vile Ayubu alivyoteseka. Na kwa nini hakuna yeyote ambaye amepitia aina hiyo ya majaribio ya Ayubu? Kwa sababu, kama vile Mungu Anavyoona, hakuna yeyote anayeweza kuvumilia wajibu au agizo kama hilo, hakuna anayeweza kufanya kama Ayubu alivyofanya, na, zaidi, hakuna yule ambaye bado, mbali na kuilaani siku ya kuzaliwa kwake, anaweza kutoliacha jina la Mungu na kuendelea kubariki jina la Yehova Mungu, kama vile Ayubu alivyofanya wakati mateso kama hayo yalimpata. Je, mtu yeyote angeweza kufanya hivi? Tunaposema haya kumhusu Ayubu, tunapongeza tabia yake? Alikuwa binadamu mwenye haki, na aliyeweza kuwa na ushuhuda kama huo kwa Mungu, aliyeweza kumfanya Shetani kutoroka kwa haraka sana, ili asiwahi kuja mbele ya Mungu tena na kumshtaki yeye—kwa hivyo nini mbaya na kumpongeza? Inaweza kuwa kwamba kunavyo viwango vya juu zaidi kuliko Mungu? Inaweza kuwa kwamba ungechukua hatua hata bora zaidi kuliko Ayubu wakati majaribio yatakapokusibu? Ayubu alisifiwa na Mungu—ni upinzani upi unaoweza kuwa nao?

Ayubu Anailaani Siku Ya Kuzaliwa Kwake Kwa Sababu Hataki Mungu Kupata Maumivu Kwa Sababu Yake Yeye

Mara nyingi mimi husema kwamba Mungu huangalia ndani ya mioyo ya watu, na watu huangalia namna watu walivyo kwa nje. Kwa sababu Mungu anaangalia ndani ya mioyo ya watu, Anaelewa kiini chao, huku nao watu wanafafanua kiini cha watu wengine kutokana na wanavyoonekana kwa nje. Wakati Ayubu alipoufunua mdomo wake na kulaani siku ya kuzaliwa kwake, kitendo hiki kilishangaza wahusika wote wa kiroho, wakiwemo wale marafiki watatu wa Ayubu. Binadamu alitoka kwa Mungu, na anafaa kuwa mwenye shukrani kwa maisha na mwili, pamoja na siku yake ya kuzaliwa, aliopewa na Mwenyezi Mungu, na wala hafai kuilaani. Hali hii inaeleweka na kufahamika na watu wengi. Kwa yeyote yule anayemfuata Mungu, uelewa huu ni takatifu na wenye dhabiti, ni ukweli usioweza kubadilika. Ayubu, kwa mkono mwingine, alizivunja sheria: Aliilaani siku ya kuzaliwa kwake. Hiki ni kitendo ambacho watu wengi huchukulia kuwa ni kuvuka hadi kwenye eneo haramu. Yeye hastahili tu uelewa na huruma ya watu, lakini pia hastahili msamaha wa Mungu. Wakati huohuo, hata watu wengi zaidi wanatilia shaka uhaki wa Ayubu, kwani inaonekana kana kwamba kibali cha Mungu kwake yeye kilimfanya Ayubu kujifikiria yeye mwenyewe, kilimfanya kuwa jasiri sana na asiyejali kiasi cha kwamba hakuweza tu kutoshukuru Mungu kwa kumbariki yeye na kumtunza yeye wakati wa maisha yake, lakini pia aliilaani siku ya kuzaliwa kwake na kuomba ingeangamizwa. Hii ni nini, kama si kumpinga Mungu? Mambo ya juujuu kama hayo yanawapa watu ithibati ya kushutumu kitendo hiki cha Ayubu, lakini ni nani anayejua kile Ayubu alichokuwa akifikiria kwa kweli wakati huo? Na ni nani anayeweza kujua sababu ya Ayubu kufanya hivyo? Mungu pekee na Ayubu mwenyewe ndio wanaojua hadithi ya ndani na sababu husika hapa.
Wakati Shetani alipounyosha mbele mkono wake ili kudhuru mifupa ya Ayubu, Ayubu aliangukia mashiko yake, bila ya mbinu za kutoroka au nguvu za kumpinga. Mwili na nafsi yake iliteseka na kupata maumivu makali, na maumivu haya yalimfanya kufahamu kwa kina kuhusu kutokuwa na umuhimu, unyonge, na hali ya kutokuwa na mamlaka iliyokuwemo ndani ya mwili. Wakati huohuo, alipata uelewa mkubwa wa kwa nini Mungu Anatilia maanani kujali na kumtunza mwanadamu. Akiwa ameangukia mashiko ya shetani, Ayubu alitambua kwamba binadamu, aliye katika mwili na damu, kwa hakika hana nguvu kamwe. Wakati aliposujudu na kumwomba Mungu, alihisi ni kana kwamba Mungu Alikuwa akiufunika uso Wake, na kujificha, kwani Mungu Alikuwa Amemweka kabisa katika mikono ya Shetani. Wakati huohuo, Mungu Alimlilia yeye, na, zaidi, Alimsikitikia yeye; Mungu Aliumizwa na maumivu yake na Aliumia kwa maumivu yake. … Ayubu alihisi maumivu ya Mungu, pamoja na namna ambavyo haikuweza kuvumilika kwa Mungu. … Ayubu hakutaka kuleta huzuni wowote zaidi kwa Mungu, wala hakutaka Mungu kulia kwa ajili yake yeye, isitoshe hakutaka kumwona Mungu akiwa katika maumivu kwa sababu yake yeye. Wakati huu, Ayubu alitaka tu kujiondoa mwenyewe kwenye mwili wake, kuacha kuvumilia tena maumivu yaliyoletewa kwake kupitia kwa mwili wake, kwani kufanya hivi kungekomesha Mungu kuteseka kwa maumivu yake—lakini hakuweza kufanya hivyo, na alifaa kuvumilia tu maumivu ya mwili, na pia mateso ya kutotaka kumfanya Mungu kuwa na wasiwasi. Maumivu haya mawili—moja kutoka kwa mwili, na mengine kutoka kwa roho—yalileta maumivu makali ya moyoni, yakusokotesha tumbo kwake Ayubu, na kumfanya yeye kuhisi namna ambavyo mipaka ya binadamu aliye na mwili na damu inavyoweza kumfanya mtu kuhisi akiwa amedhalilishwa na asiye na njia ya kusaidika. Katika hali hizi, tamanio lake la Mungu lilizidi kukua, na chuki yake kwa Shetani ikazidi kuwa nyingi. Wakati huu, Ayubu angependelea kutowahi kuzaliwa kwenye ulimwengu huu wa binadamu, afadhali asingekuwepo badala ya kumuona Mungu Akilia au Akihisi maumivu kwa sababu yake. Alianza kuchukia kwa kina mwili wake, kuwa mgonjwa na mchovu ndani yake mwenyewe, siku yake ya kuzaliwa, na hata ya hayo yote ambayo yalikuwa yameunganishwa kwake. Hakutaka kuwepo na kutajwa kokote zaidi kuhusu siku yake ya kuzaliwa au chochote kilichohusu siku hiyo, na hivyo aliufunua mdomo wake na kuilaani siku yake ya kuzaliwa: “Itokomee mbali ile siku niliyozaliwa, na ule usiku uliosema, Mtoto mume ameingia katika mimba. Siku hiyo na iwe giza; acha Mungu asiiangalie kutoka juu, wala mwanga usiiangazie.” (Ayubu3:3-4). Maneno ya Ayubu yanaonyesha kuchukia kwake kwa nafsi yake mwenyewe, “Itokomee mbali ile siku niliyozaliwa, na ule usiku uliosema, Mtoto mume ameingia katika mimba,” pamoja na yeye kujilaumu mwenyewe na kuwa katika hali ya kuhisi kwamba yuko katika hatia kwa kumsababishia Mungu maumivu, “Siku hiyo na iwe giza; acha Mungu asiiangalie kutoka juu, wala mwanga usiiangazie.” Vifungu hivi viwili ni maonyesho ya namna Ayubu alivyohisi wakati huo, na vinaonyesha kikamilifu utimilifu wake na unyofu wake kwa wote. Wakati huohuo, kama vile tu Ayubu alivyokuwa ametaka, imani na utiifu wake kwa Mungu, pamoja na kumcha Mungu kwake, vyote viliinuliwa. Bila shaka, kuinuliwa huku kwa hakika ni athari ambayo Mungu Alikuwa Ametarajia.

Ayubu Amshinda Shetani na Kuwa Binadamu Wa Kweli Machoni mwa Mungu

Wakati Ayubu alipopitia majaribio yake kwa mara ya kwanza, alinyang’anywa mali yake yote na watoto wake wote, lakini hakujisujudia na kusema chochote ambacho kilikuwa dhambi dhidi ya Mungu kutokana na hayo. Alikuwa ameshinda majaribio ya Shetani, na alikuwa ameshinda rasilimali zake zote za dunia na watoto wake, na majaribio ya kupoteza mali yake ya dunia, hivi ni kusema kwamba aliweza kutii Mungu kuchukua na kutwaa kutoka kwake na akatoa shukrani na sifa kwa Mungu kwa sababu ya hayo. Hivyo ndivyo ulivyokuwa mwenendo wa Ayubu wakati wa jaribio la kwanza la Shetani, na huo ndio uliokuwa ushuhuda wa Ayubu wakati wa jaribio la kwanza la Mungu. Kwenye jaribio la pili, Shetani aliunyosha mbele mkono wake ili kumdhuru Ayubu, na ingawaje Ayubu alipitia maumivu yaliyokuwa makubwa zaidi kuliko yale aliyokuwa amepitia awali, bado ushuhuda wake ulikuwa wa kutosha wa kuacha watu wakiwa wameshangazwa. Alitumia ujasiri wake, imani yake, na utiifu kwa Mungu, pamoja na kumcha Mungu kwake, kwa mara nyingine tena kumshinda Shetani, na mwenendo wake na ushuhuda wake viliweza kwa mara nyingine tena kuidhinishwa na kupata kibali cha Mungu. Wakati wa majaribio haya, Ayubu alitumia mwenendo wake halisi kumtangazia Shetani kwamba maumivu ya mwili wake yasingebadilisha imani yake na utiifu wake kwa Mungu au kuchukua ule upendo wake kwa Mungu na kumcha Mungu; asingemuacha Mungu au kutupilia mbali utimilifu wake binafsi na unyofu kwa sababu alikuwa amekabiliwa na kifo. Bidii ya Ayubu ilimfanya Shetani mwoga, imani yake ilimuacha Shetani akiwa na dukuduku na kutetemeka, nguvu za vita vya maisha yake na kifo chake na Shetani viliweza kuzua chuki na dharau nyingi kwa Shetani, utimilifu na unyofu wake ulimuacha Shetani akiwa hana chochote zaidi cha kumfanya kiasi cha kwamba Shetani aliyaacha mashambulizi yake kwake na kukata tamaa na mashtaka yake dhidi ya Ayubu mbele ya Yehova Mungu. Hii ilimaanisha kwamba Ayubu alikuwa ameushinda ulimwengu, alikuwa ameushinda mwili wake, alikuwa amemshinda Shetani, na alikuwa ameshinda kifo; alikuwa kwa kweli na hakika binadamu aliyemilikiwa na Mungu. Wakati wa majaribio haya mawili, Ayubu alisimama imara katika ushuhuda wake, na kwa hakika aliishi kwa kudhihirisha utimilifu wake na unyofu, na akapanua upana wa kanuni zake za kuishi za kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Baada ya kupitia majaribio haya mawili, ndani ya Ayubu kulizaliwa uzoefu mwingi, na uzoefu huu ulimfanya yeye kuwa mwenye kimo na uzoefu zaidi, ilimfanya kuwa mwenye nguvu zaidi, na imani kubwa zaidi, na ilimfanya yeye kuwa na ujasiri zaidi kuhusu haki na ustahili wa uadilifu ambao yeye alishikilia kwa dhati. Majaribio ya Yehova Mungu kwa Ayubu yalimpa uelewa wa kina na hisia za wasiwasi wa Mungu kwa binadamu, na kumruhusu yeye kuhisi thamani ya upendo wa Mungu, ambapo vyote vinaelekezwa katika utiliaji maanani kwa na kuhusu upendo wa Mungu na vyote viliweza kuongezwa katika kumcha Mungu. Majaribio ya Yehova Mungu kumwondoa tu Ayubu kutoka Kwake, lakini pia yaliuleta moyo wake karibu na Mungu. Wakati maumivu yale ya mwili yaliyovumiliwa na Ayubu yalifikia kilele, wasiwasi aliouhisi kutoka kwa Yehova Mungu haukumpa chaguo lolote ila kuilaani siku yake ya kuzaliwa. Mwenendo kama huo haukuwa umepangiliwa mapema lakini ulikuwa ni ufunuo wa kiasili wa kutilia maanani na kumpenda Mungu kutoka ndani ya moyo wake, ulikuwa ni ufunuo wa kiasili uliotoka kwenye kutilia maanani na kumpenda Mungu kwake. Hivi ni kusema, kwa sababu alijichukia, na hakuwa na radhi na hakuweza kuvumilia kuona Mungu Akiteswa, hivyo kutilia maanani na upendo wake vilifika hali ya kutojijali. Wakati huu, Ayubu aliimarisha kuabudu kwake kwa muda mrefu na kutamani kwake kwa Mungu na upendo kwa Mungu hadi katika kiwango cha utiliaji maanani na upendo. Wakati huohuo, aliweza kupandisha imani na utiifu wake kwa Mungu na kumcha Mungu kwake hadi katika kiwango cha kutilia maanani na upendo. Hakujiruhusu kufanya chochote ambacho kingesababisha madhara kwa Mungu, hakujiruhusu mwenendo ambao ungemuumiza Mungu, na hakujiruhusu kuleta masikitiko, huzuni au hata kutokuwa na furaha kokote kwake Mungu kwa sababu zake mwenyewe.. Katika Macho ya Mungu, ingawaje Ayubu alikuwa bado Ayubu wa hapo awali, imani, utiifu na kumcha Mungu kwake kulikuwa kumemletea Mungu utoshelezi kamilifu. Wakati huu, Mungu alitarajia Ayubu kuweza kutimiza, alikuwa amegeuka kuwa mtu aliyestahili kuitwa “mtimilifu na mnyofu” mbele ya macho ya Mungu. Vitendo vyake vya haki vilimruhusu yeye kumshinda Shetani na kuwa makini katika ushuhuda wake kwa Mungu. Hivyo, pia, matendo yake ya haki yalimfanya kuwa mtimilifu, na kuruhusu thamani ya maisha yake kuimarishwa, kuzidishwa zaidi kuliko awali, na kumfanya yeye kuwa mtu wa kwanza kutoweza kushambuliwa au kujaribiwa zaidi na Shetani. Kwa sababu Ayubu alikuwa mwenye haki, alishtakiwa na kujaribiwa na Shetani; kwa sababu Ayubu alikuwa mwenye haki, alikabidhiwa Shetani; na kwa sababu Ayubu alikuwa mwenye haki, alishinda na kumlemea Shetani, na kuweza kusimama imara katika ushuhuda wake. Kuendelea mbele, Ayubu akawa binadamu wa kwanza ambaye hangewahi tena kukabidhiwa Shetani, kwa kweli alikuja mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, na akaishi kwenye nuru, katika baraka za Mungu bila ya kupelelezwa au kuangamizwa na shetani. … Alikuwa amekuwa binadamu wa kweli katika macho ya Mungu, alikuwa ameachiliwa huru. …

Kuhusu Ayubu

Baada ya kusikia namna Ayubu alivyopitia majaribio, kunao uwezekano kwamba wengi wenu watataka kujua maelezo zaidi kuhusu Ayubu mwenyewe, hasa kuhusiana na siri iliyomfanya akapata sifa za Mungu. Hivyo basi leo, hebu tuzungumzie kuhusu Ayubu!

Katika Maisha ya Kila Siku ya Ayubu Tunaona Utimilifu, Unyofu, Kumcha Mungu, na Kujiepusha na Maovu

Kama tutazungumzia Ayubu, basi lazima tuanze na namna ambavyo alitathminiwa kwa mujibu wa matamshi kutoka kwa kinywa cha Mungu mwenyewe: “hakuna hata mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mnyofu, mwenye kumcha Mungu, na kuuepuka uovu.”
Hebu kwanza tujifunze kuhusu utimilifu na unyofu wa Ayubu.
Unaelewa vipi maneno haya “utimilifu” na “unyofu”? Unasadiki kwamba Ayubu hakuwa na lawama, na kwamba aliheshimika? Hili, bila shaka, litakuwa ni ufasiri wa moja kwa moja na uelewa wa “mtimilifu” na “mnyofu.” Muhimu katika uelewa wa kweli wa Ayubu ni maisha halisi—maneno, vitabu, na nadharia pekee haviwezi kutupa majibu yoyote. Tutaanza na kuyaangalia maisha ya Ayubu ya nyumbani, kuangalia namna mwenendo wake wa kawaida ulivyokuwa maishani mwake. Kufanya hivi kutatwambia kuhusu kanuni na malengo yake maishani, pamoja na kuhusu hulka yake na mambo yale aliyoyafuatilia. Sasa, hebu tuyasome maneno ya mwisho katika Ayubu 1:3: “mtu huyo alikuwa ni mkuu sana kuliko watu wote wa mashariki.” Kile ambacho maneno haya yanasema ni kwamba hadhi na heshima ya Ayubu ilikuwa ya juu sana, na ingawaje hatuambiwi kama alikuwa ndiye mkubwa zaidi kati ya wanaume wote wa mashariki kwa sababu ya wingi wa rasilimali zake au kwa sababu alikuwa mtimilifu na mnyofu, na kwamba alimcha Mungu na kujiepusha maovu, kwa ujumla tunajua kwamba hadhi na heshima ya Ayubu vyote vilithaminiwa sana. Kama ilivyorekodiwa kwenye Biblia, picha za kwanza za Ayubu kwa watu zilikuwa kwamba Ayubu alikuwa mtimilifu, kwamba alimcha Mungu na kujiepusha na maovu na kwamba alimiliki utajiri mkubwa na alikuwa na hadhi ya kuheshimika. Kwa mtu wa kawaida anayeishi katika mazingira kama haya na hali kama hizo, mlo wa Ayubu, ubora wa maisha, na vipengele mbalimbali vya maisha yake ya kibinafsi vyote vingekuwa malengo ya umakinifu wa watu wengi; hivyo lazima tuendelee kuyasoma maandiko: “Nao wanawe walienda na kufanya karamu katika nyumba zao, kila kwa siku yake; nao wakatuma na kuwaita ndugu wao wa kike watatu ili waje kula na kunywa pamoja nao. Na ilikuwa hivyo, hizo siku za karamu zao zilipokuwa zimetimia, Ayubu aliwatuma na kuwatakasa, kisha akaamka asubuhi na mapema, na kutoa sadaka za kuteketezwa kulingana na hesabu yao wote ilivyokuwa; kwani Ayubu alisema, Inaweza kuwa kwamba wanangu wamefanya dhambi, na kumkufuru Mungu mioyoni mwao. Hivyo ndivyo Ayubu alivyofanya siku zote” (Ayubu 1:4-5). Kifungu hiki kinatuambia mambo mawili: Jambo la kwanza ni kwamba watoto wa kiume na wa kike wa Ayubu walishiriki kwenye karamu mara kwa mara, wakila na wakinywa; pili ni kwamba Ayubu mara kwa mara alitoa sadaka za kuteketezwa kwa sababu alikuwa na wasiwasi na wao, akiogopa kwamba walikuwa wakitenda dhambi, kwamba katika mioyo yao walikuwa wamemlaani Mungu. Katika maandiko haya maisha ya watu wa aina mbili tofauti yanafafanuliwa. Maisha ya kwanza, watoto wa kiume na kike wa Ayubu, mara nyingi walishiriki kwenye karamu kwa sababu ya ukwasi wao, waliishi kwa ubadhirifu, wakinywa na wakila hadi mioyo yao kutosheka, wakifurahia maisha ya kiwango cha juu yaliyoletwa na utajiri wa anasa. Wakiishi maisha kama haya, ilikuwa lazima kwamba mara kwa mara wangetenda dhambi na kumkosea Mungu—ilihali hawakujitakasa wala kutoa sadaka za kuteketezwa kutokana na hayo yote. Waona, basi, kwamba Mungu hakuwa na nafasi katika mioyo yao, kwamba hawakufikiria kuhusu neema za Mungu, wala kuogopa kumkosea Mungu, isitoshe hawakuogopa kumuacha Mungu katika mioyo yao. Bila shaka zingatio letu si watoto wa Ayubu, lakini ni kwa kile ambacho Ayubu alifanya alipokabiliwa na mambo kama haya; hili ndilo suala lile jingine lililofafanuliwa katika kifungu, na ambalo linahusisha maisha ya kila siku ya Ayubu na kiini cha ubinadamu wake. Wakati Biblia inapofafanua kushiriki kwa watoto wa kike na kiume katika karamu mbalimbali hakuna mahali ambapo Ayubu anatajwa; yasemekana tu kuwa ni watoto wake wa kiume na wa kike walio kula na kunywa pamoja. Kwa maneno mengine, hakuandaa karamu, wala hakujiunga na watoto wake wa kiume na kike katika karamu hizo ili kuendeleza ubadhirifu. Ingawaje alikuwa tajiri, na alimiliki raslimali nyingi na watumishi wengi, maisha ya Ayubu hayakuwa ya anasa. Hakudanganywa na mazingira yake ya juu kabisa aliyoyaishi na wala hakujawa na ulafi wa anasa za mwili au kusahau kutoa sadaka za kuteketezwa kwa sababu za utajiri wake, isitoshe pia haya yote hayakumsababisha kuanza kujiepusha na Mungu ndani ya moyo wake kwa utaratibu. Ni dhahiri shairi, hivyo basi, kwamba Ayubu alikuwa na nidhamu katika hali ya maisha yake, na wala hakuwa mlafi au na imani ya kuwa anasa ni kitu muhimu katika maisha, wala hakushikilia na kupumbazwa na ubora wa maisha, kutoka na baraka za Mungu kwake. Badala yake, alinyenyekea na akawa asiye na majivuno, na kuwa mtulivu na makini mbele ya Mungu, mara nyingi alifikiria kuhusu neema na baraka za Mungu, na siku zote alimcha Mungu. Katika maisha yake ya kila siku, Ayubu mara nyingi alirauka mapema ili kutoa sadaka zilizoteketezwa kwa niaba ya watoto wake wa kiume na kike. Kwa maneno mengine, Ayubu mwenyewe alimcha Mungu na pia alitumaini kwamba watoto wake wangeweza vilevile kumcha Mungu na kutotenda dhambi dhidi ya Mungu. Utajiri wa anasa wa Ayubu haukuwa na mahali popote ndani ya moyo wake, wala haukusawazisha ile nafasi iliyoshikiliwa na Mungu; haijalishi kama ilikuwa ni kwa ajili yake mwenyewe au watoto wake, vitende vyote vya kila siku vya Ayubu viliunganishwa katika kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Kumcha Yehova Mungu kwake hakukuishia kwenye kinywa chake lakini kulitiwa katika vitendo, na kukajionyesha katika kila sehemu ya maisha yake. Mwenendo huu halisi wa Ayubu unatuonyesha kwamba alikuwa mwaminifu, na alimiliki kiini kilichopenda haki na mambo yaliyokuwa mazuri. Kwamba Ayubu mara nyingi alituma sadaka ya kuwateketeza na kwa niaba ya watoto wake wa kiume na kike na kuwatakasa kunamaanisha kwamba hakuruhusu wala kuidhinisha tabia ya watoto wake; badala yake katika moyo wake alichoshwa na tabia yao, na akawashutumu vikali. Alikuwa amedhibitisha kwamba tabia ya watoto wake wa kike na kiume haikupendeza Yehova Mungu na hivyo basi mara nyingi aliwaita kwenda mbele ya Yehova Mungu na kutubu dhambi zao. Vitendo vya Ayubu vinatuonyesha upande mwingine wa ubinadamu wake: ule ambao unaonyesha kwamba hakuwahi kutembea na wale ambao mara nyingi walitenda dhambi na kumkosea Mungu, lakini badala yake alijiepusha na kutotaka kuwa nao. Hata ingawaje watu hawa walikuwa watoto wake wa kike na kiume, hakuziacha kanuni zake za kibinafsi kwa sababu walikuwa ukoo wake binafsi wala hakujihusisha kwa dhambi zao kwa sababu ya hisia zake binafsi za moy0ni. Badala yake aliwasihi kutubu na kupata ustahimilivu wa Yehova Mungu na akawaonya kutomwacha Mungu kwa ajili ya kujifurahisha kwao kwa ulafi. Kanuni za namna ambavyo Ayubu aliwashughulikia wengine haziwezi kutenganishwa na zile kanuni za kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Alipenda kile kilichokubalika na Mungu na kuchukia kile Alichokiona Mungu kuwa mbaya, na akawapenda wale waliomcha Mungu katika mioyo yao, na kuchukia wale waliotenda maovu au kutenda dhambi dhidi ya Mungu. Upendo na chuki kama hiyo zilionyeshwa katika maisha yake ya kila siku, na ndio uliokuwa unyofu wenyewe wa Ayubu ulioonekana katika macho ya Mungu. Kiasili, haya pia ndiyo maonyesho na kuishi kulingana na ubinadamu wa kweli wa Ayubu katika mahusiano yake na wengine katika maisha yake ya kila siku ambao lazima tujifunze kuhusu.

Maonyesho ya Ubinadamu wa Ayubu Wakati wa Majaribio Yake (Kuelewa Utimilifu wa Ayubu, Unyofu, Kumcha Mungu na Kujiepusha na Maovu Wakati wa Majaribio Yake)

Kile tulichozungumzia hapo juu ni vipengele mbalimbali vya ubinadamu wa Ayubu zilizoonyeshwa katika maisha yake ya kila siku kabla ya majaribio yake. Bila shaka, maonyesho haya mbalimbali yanatupa ufahamu wa mwanzo pamoja na uelewa wa unyofu wa Ayubu, kumcha Mungu na kujiepusha na maovu kwake, na unatupa uthibitisho wa mwanzo. Sababu inayonifanya kusema “mwanzo” ni kwa kuwa watu wengi bado hawana uelewa wa kweli wa hulka ya Ayubu na kiwango ambacho alifuatilia njia ya kutii na kumcha Mungu. Hivi ni kusema, uelewa wa watu wengi kuhusu Ayubu hauendi zaidi ya ile picha ambayo kwa kiasi fulani inamfaa yeye kama ilivyoelezewa kwa maneno yake kwenye Biblia kwamba “BWANA alinipa, na BWANA amechukua; jina la BWANA libarikiwe” na “Vipi? Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya??” Hivyo, kunayo haja kubwa yetu sisi kuelewa namna ambavyo Ayubu aliishi kwa kudhihirisha ubinadamu wake alipokuwa akipokea majaribu ya Mungu; kwa njia hii, ubinadamu wote wa kweli wa Ayubu utaweza kuonyeshwa kwa wote.
Wakati Ayubu aliposikia kwamba mali yake yalikuwa yameibwa, kwamba watoto wake wa kike na kiume walikuwa wameaga dunia, na kwamba watumishi wake walikuwa wameuliwa, aliitikia hivi: “Kisha Ayubu akainuka, akalipasua joho lake, na akanyoa kichwa chake, na akaanguka chini, na kuabudu;” (Ayubu 1:20). Maneno haya yanatuambia ukweli mmoja: Baada ya kuzisikiza habari hizi, Ayubu hakushikwa na wasiwasi, hakulia, au kuwalaumu wale watumishi ambao walikuwa wamempa habari hizo, isitoshe hakukagua eneo la uhalifu ili kuchunguza na kudhibitisha ni kwa nini na ni vipi hali ilikuwa hivyo na kutaka kujua ni nini haswa kilichofanyika. Hakuonyesha maumivu au majuto yoyote kutokana na kupoteza mali yake wala hakuanza kupukutikwa na machozi kutokana na kuwapoteza watoto wake, wapendwa wake. Kinyume ni kwamba, akalirarua joho lake kisha akanyoa kichwa chake, na kuanguka chini, na kuabudu. Vitendo vya Ayubu ni tofauti sana na vile vya binadamu wa kawaida. Vinawachanganya watu wengi, na kuwaruhusu kumkosoa Ayubu ndani ya mioyo yao kwa “kukosa huruma na rehema. Kwa kupotea ghafla kwa mali yao, watu wa kawaida wangeonekana wamevunjwa moyo, au wanasikitika kweli— au kama ilivyo kwa baadhi ya watu, wanaweza hata kujipata wakiwa wamefadhaishwa moyo. Hii ni kwa sababu, katika mioyo yao, mali ya watu inawakilisha jitihada ya maisha yao yote, ndiyo ambayo maisha yao yanategemea, ndilo tumaini linalowafanya kuishi; kupoteza mali yao kunamaanisha jitihada zao zimeambulia patupu na kwamba hawana tumaini tena na kwamba pia hawana siku za usoni. Huu ndio mwelekeo wa mtu yeyote wa kawaida kuhusiana na mali yake na uhusiano wa karibu alio na mali hiyo, na huu ndio pia umuhimu wa mali katika macho ya watu. Hivyo, idadi kubwa ya watu wanahisi wakiwa wamechanganyikiwa na mwelekeo mtulivu wa Ayubu kuhusiana na kupoteza[c]mali yake. Leo, tutauondoa mkanganyiko huo wa watu hawa wote kwa kuelezea kile kilichokuwa kikipitia moyoni mwa Ayubu.
Akili za kawaida zinakariri kwamba, kwa kuwa alikuwa amepewa rasilimali hizo nyingi na Mungu, Ayubu anafaa kuaibika mbele ya Mungu kwa sababu ya kuzipoteza rasilimali hizi, kwani alikuwa hajazitunza, alikuwa hajashikilia zile rasilimali alizopewa na Mungu . Hivyo, aliposikia kwamba mali yake ilikuwa imeibwa, mwitikio wake wa kwanza ulifaa kuwa kuenda kwenye eneo la uhalifu na kuchukua hesabu ya kila kitu kilichokuwa kimeenda[d] na kisha kutubu kwa Mungu ili aweze kwa mara nyingine kupokea baraka za Mungu. Ayubu, hata hivyo hakufanya hivi—na kiasili alikuwa na sababu zake za kutofanya hivyo. Ndani ya Moyo wake, Ayubu alisadiki pakubwa kwamba kila kitu alichomiliki alikuwa amepewa na Mungu na hakikuwa kimetokana na jitihada zake yeye mwenyewe. Hivyo, hakuziona baraka hizo kama jambo la kutilia maanani, lakini alishikilia ile njia alifaa kuchukua kwa udi na uvumba kama kanuni zake za kuishi. Alizitunza baraka za Mungu, na akatoa shukrani kutokana nazo, lakini hakutamanishwa nazo wala hakutafuta baraka zaidi. Huo ndio uliokuwa mwelekeo wake kuhusu mali. Hakufanya chochote kwa minajili ya kupata baraka, wala kuwa na wasiwasi kuhusu au kuhuzunishwa kutokana na ukosefu au kupoteza baraka za Mungu; hakufurahi kwa njia ya kupindukia na isiyo na mipaka kwa sababu ya baraka za Mungu na wala hakupuuza njia ya Mungu wala kusahau neema ya Mungu kwa sababu ya zile baraka ambazo alifurahia mara kwa mara. Mtazamo wa Ayubu kwa mali yake unafichulia watu ubinadamu wake wa kweli: Kwanza, Ayubu hakuwa binadamu mlafi, na hakuwa na madai katika maisha yake yakinifu. Pili, Ayubu hakuwahi kuwa na wasiwasi au kuogopa kwamba Mungu angechukua kila kitu alichokuwa nacho, na ndio uliokuwa mwelekeo wake wa utiifu kwa Mungu ndani ya moyo wake; yaani, hakuwa na madai au malalamiko kuhusu ni lini au kama Mungu angechukua kutoka kwake, na wala hakuuliza sababu, lakini alilenga tu kutii mipango ya Mungu. Tatu, hakuwahi kusadiki kwamba rasilimali zake zilitokana na jitihada zake, lakini kwamba alipewa yeye na Mungu. Hii ilikuwa imani ya Ayubu kwa Mungu, na onyesho la imani yake. Je, ubinadamu wa Ayubu na ufuatiliaji wake wa kweli wa kila siku umefanywa kuwa wazi katika mhutasari huu wa hoja tatu kumhusu yeye? Ubinadamu na ufuatiliaji wa Ayubu ni vitu vilivyokuwa muhimu katika mwenendo wake mtulivu alipokabiliwa na hali ya kupoteza mali yake. Ilikuwa hasa kwa sababu ya ufuatiliaji wake wa kila siku ndipo Ayubu akawa na kimo na imani ya kusema, “BWANA alinipa, na BWANA amechukua; jina la BWANA libarikiwe,” kwenye majaribio ya Mungu. Maneno haya hayakupatwa kwa mkesha mmoja, na wala hayakujitokeza tu kwa ghafla kwenye kichwa chake Ayubu. Yalikuwa yale ambayo alikuwa ameona na kupata kwa miaka mingi ya kupitia safari ya maisha. Akilinganishwa na wale wote wanaotafuta tu baraka za Mungu na wanaoogopa Mungu atachukua kutoka kwao, nao wanachukia hali hio na wanalalamikia kuhusu hali hiyo, je utiifu wa Ayubu ni wa kweli haswa? Tukilinganisha na wale wote wanaosadiki kwamba Mungu yupo, lakini ambao hawajawahi kusadiki kwamba Mungu anatawala mambo yote, Ayubu anamiliki uaminifu na unyofu mkubwa?

Urazini wa Ayubu

Uzoefu halisi wa Ayubu na ubinadamu wake wenye unyofu na uaminifu ulimaanisha kwamba alifanya uamuzi na uchaguzi wenye urazini zaidi alipozipoteza rasilimali zake na watoto wake. Machaguo kama hayo ya kirazini yasingeweza kutenganishwa na shughuli zake za kila siku na vitendo vya Mungu ambavyo alikuwa amejua kwenye maisha yake ya siku baada ya siku. Uaminifu wa Ayubu ulimfanya kuweza kusadiki kwamba mkono wa Yehova unatawala mambo yote; imani yake ilimruhusu kujua ukweli wa ukuu wa Yehova Mungu juu ya vitu vyote; maarifa yake ilimfanya kuwa radhi na kuwa na uwezo wa kutii ukuu na mipangilio ya Yehova Mungu juu ya vitu vyote; utiifu wake ulimwezesha kuwa mkweli na mkweli zaidi katika kumcha kwake kwa Yehova Mungu; kumcha kwake kulimfanya kuwa halisi zaidi na zaidi katika kujiepusha kwake na maovu; hatimaye, Ayubu alikuwa mtimilifu kwa sababu alimcha Mungu na kujiepusha na maovu; na ukamilifu kwake kulimfanya kuwa na hekima zaidi na kukampa urazini wa kipekee.
Tunafaa kulielewa vipi neno hili “urazini”? Ufasiri wa moja kwa moja unamaanisha kwamba kuwa mwenye hisia nzuri, kuwa mwenye mantiki na wa kueleweka katika kufikiria kwako, kuwa na maneno ya kueleweka, vitendo na hukumu ya kueleweka, na kumiliki viwango visivyo na makosa na maadili ya mara kwa mara. Lakini urazini wa Ayubu hauelezwi sana kwa urahisi. Inaposemekana hapa kwamba Ayubu alimiliki urazini wa kipekee, inahusiana na ubinadamu wake na mwenendo wake mbele ya Mungu. Kwa sababu Ayubu alikuwa mwaminifu, aliweza kuusadiki na kuutii ukuu wa Mungu, uliompa maarifa ambayo yasingeweza kupatikana na wengine na maarifa haya yalimfanya kuweza kutambua, kuhukumu, na kufafanua kwa usahihi zaidi yale yaliyompata, na yaliyomwezesha kuchagua ni nini cha kufanya na ni nini cha kushikilia kwa usahihi na wepesi zaidi wa kukata ushauri. Hivi ni kusema kwamba maneno, tabia, na kanuni zake ziliandamana na hatua zake, na msimbo ambao aliufanyia kazi, ulikuwa wa mara kwa mara, ulio wazi, na mahususi na haukukosa mwelekeo, wenye uamuzi wa haraka au wa kihisia. Alijua namna ya kushughulikia chochote kile kilichompata yeye, alijua namna ya kusawazisha na kushughulikia mahusiano kati ya matukio magumu, alijua namna ya kushikilia mambo kwa njia ambayo mambo hayo yalifaa kushikiliwa, na, vilevile, alijua namna ya kushughulikia ule utoaji na uchukuaji wa Yehova Mungu. Huu ndio uliokuwa urazini wenyewe wa Ayubu. Ilikuwa hasa kwa sababu Ayubu alijihami na urazini kama huu ndiposa akasema, “BWANA alinipa, na BWANA amechukua; jina la BWANA libarikiwe,” alipozipoteza rasilimali zake na watoto wake wa kiume na kike.
Wakati Ayubu alipokabiliwa na maumivu kali ya mwili, na malalamiko ya watu wa ukoo na marafiki zake, na wakati alipokabiliwa na kifo, mwenendo wake halisi kwa mara nyingine tena ulionyesha kimo chake kwa mambo yote.

Uso Halisi wa Ayubu: Mkweli, Aliyetakaswa, na Asiye na Uongo

Hebu tusome maandiko yafuatayo: “Hivyo Shetani akatoka mbele za uso wa BWANA, na akampiga Ayubu na majipu mabaya kutoka kwenye wayo wa mguu mpaka utosi wa kichwa. Na akajishikia kigae ili ajikune nacho; akaketi chini kwenye majivu” (Ayubu 2:7-8). Huu ni ufafanuzi wa mwenendo wa Ayubu wakati ambapo majipu yawashayo yalipoota kwenye mwili wake. Wakati huu, Ayubu aliketi kwenye majivu huku akiyavumilia. Hakuna aliyemtibu yeye, na hakuna aliyemsaidia kupunguza maumivu kwenye mwili wake; badala yake, alitumia kigaye cha chungu kukwaruza sehemu ya juu ya majipu yake yenye maumivu. Juu juu, hii ilikuwa awamu tu ya mateso ya Ayubu na haina uhusiano wowote na ubinadamu wake na kumcha Mungu kwake, kwani Ayubu hakuongea maneno yoyote kuonyesha hali na maoni yake wakati huo. Lakini matendo na mwenendo wake Ayubu bado ni onyesho la kweli la ubinadamu wake. Kwenye rekodi za sura ya awali tunasoma kwamba Ayubu alikuwa ndiye mkuu zaidi kati ya wanaume wote wa mashariki. Kifungu hiki cha sura ya pili, nayo, inatuonyesha kwamba binadamu huyu mkuu wa mashariki anafaa kuchukua kigae cha chungu na kujikwaruza nacho huku akiwa ameketi kwenye jivu. Je, hakuna ulinganuzi wowote wa wazi kati ya fafanuzi hizi mbili? Ni ulinganuzi unaotuonyesha nafsi ya kweli ya Ayubu: Licha ya nafasi na hadhi yake ya kifahari, hakuwahi kuzipenda wala kuzitilia maanani yoyote; hakujali namna wengine walivyoangalia nafasi yake wala kuhusu kama hatua au mwenendo wake ungekuwa na athari mbaya kwa nafasi yake; hakujihusisha katika utajiri wa hali, wala hakufurahia utukufu uliokuja pamoja na hadhi na nafasi yake katika jamii. Alijali tu kuhusu thamani yake na umuhimu wa kuishi kwake mbele ya macho ya Yehova Mungu. Nafsi ya kweli ya Ayubu ilikuwa kiini chake: Hakupenda umaarufu na utajiri, na wala hakuishi kwa ajili ya umaarufu na utajiri; alikuwa mkweli, na aliyetakaswa, na aliye bila ya uongo wowote.

Utenganisho wa Ayubu kati ya Upendo na Chuki

Upande mwingine wa ubinadamu wa Ayubu unaonyeshwa katika mazungumzo yake na mke wake: “Kisha mkewe akamwambia, Je, Wewe bado unashikamana na utimilifu wako? mkufuru Mungu, ufe. Lakini yeye akamwambia, Wewe unazungumza kama mmoja wa wanawake wapumbavu wanavyozungumza. Vipi? Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya? …” (Ayubu 2:9-10). Kuona mateso aliyokuwa akipitia, mke wa Ayubu alijaribu kumshauri Ayubu ili amsaidie kutoroka mateso yake— lakini zile “nia nzuri” hazikupata idhini ya Ayubu; badala yake, ziliamsha ndani yake hasira, kwani alikataa imani yake katika na utiifu wake kwa Yehova Mungu na pia akakataa uwepo wa Yehova Mungu. Hali hii isingeweza kuvumilika kwa Ayubu, kwani hakuwahi kujiruhusu kufanya chochote ambacho kingepinga au kingemdhuru Mungu, bila kusema chochote kuhusu wengine. Angewezaje kubakia vilevile bila kujali chochote wakati alipowaona wengine wakiongea maneno yaliyomkufuru na kumtukana Mungu? Hivyo basi akamuita mke wake “mwanamke mjinga.” Mwelekeo wa Ayubu kwa mke wake ulikuwa ule wa hasira na chuki, pamoja na ule wa kushutumu na kukemea. Haya ndiyo yaliyokuwa maonyesho ya kiasili ya ubinadamu wa Ayubu ambayo yalitofautisha kati ya upendo na chuki na yalikuwa uwakilishi wa kweli wa ubinadamu wake uliokuwa na unyofu. Ayubu alimiliki hali fulani ya haki—hali ambayo ilimfanya kuchukia upepo na mawimbi ya maovu, na kumfanya kuchukia, kushutumu, na kukataa uzushi wa ajabu, mabishano ya kijinga na madai yasiyokuwa na msingi, na ikamruhusu kushikilia kanuni zake sahihi, za kweli kwake yeye mwenyewe na msimamo ule aliochukua wakati alipokuwa amekataliwa na wengi na kuachwa na wale walio kuwa karibu na yeye.

Ukarimu na Uaminifu wa Ayubu

Kwa sababu, katika mwenendo wa Ayubu, tunaweza kuona maonyesho ya vipengele mbalimbali vya ubinadamu wake, tunauona ubinadamu wa Ayubu upi anapokifunua kinywa chake kuilaani siku aliyozaliwa? Hii ndiyo mada tutakayozungumzia hapa chini.
Hapo juu, Nimezungumzia asili ya laana la Ayubu ya siku ya kuzaliwa kwake. Unaona nini katika haya? Kama Ayubu asingekuwa mkarimu na asiye na upendo, kama angekuwa mnyama na asiye na hisia, na mpungufu wa ubinadamu, angejali kuhusu tamanio la moyoni mwa Mungu? Na je angedharau siku ya kuzaliwa kwake kutokana na kuutunza moyo wa Mungu? Kwa maneno mengine kama Ayubu alikuwa hana ukarimu na aliyepungukiwa na ubinadamu, angedhikishwa na maumivu ya Mungu? Angeilaani siku yake ya kuzaliwa kwa sababu Mungu alikuwa amedhulumiwa na yeye? Jibu ni, bila shaka la! Kwa sababu alikuwa mkarimu, Ayubu aliutunza moyo wa Mungu; kwa sababu aliutunza moyo wa Mungu, Ayubu alihisi maumivu ya Mungu; kwa sababu alikuwa mkarimu, alipata maumivu makali zaidi kutokana na kuyahisi maumivu ya Mungu; kwa sababu aliyahisi maumivu ya Mungu, alianza kuichukia siku ya kuzaliwa kwake, na hivyo akailaani siku yake ya kuzaliwa. Kwa watu wa nje, mwenendo wote wa Ayubu wakati wa majaribio yake ni wa kupigiwa mifano. Kulaani kwake tu kwa siku ya kuzaliwa ndiko kunakoweka picha ya kiulizo juu ya utimilifu na unyofu wake, au kutoa utathmini tofauti. Kwa hakika, haya ndiyo yaliyokuwa maonyesho ya kweli zaidi ya kiini cha ubinadamu wa Ayubu. Kiini cha ubinadamu wake hakikufichwa au kubadilishwa, au kudurusiwa na mtu mwingine. Alipoilaani siku yake ya kuzaliwa, alionyesha ukarimu na uaminifu uliokuwa ndani ya moyo wake; alikuwa kama chemichemi ya maji ambayo maji yake yalikuwa safi sana na angavu kiasi cha kufichua sehemu ya chini kabisa ya chemichemi hio.
Baada ya kujifunza haya yote kuhusu Ayubu, watu wengi zaidi bila shaka watakuwa na utathmini sahihi kwa kiasi fulani na usiopendelea kuhusu kiini cha ubinadamu wa Ayubu. Wanafaa pia kuwa na uelewa na kina kikuu cha kimatendo, na uliopevuka zaidi wa utimilifu na unyofu wa Ayubu kama ulivyozungumzwa na Mungu. Ni tumaini langu kwamba, uelewa na kina hiki kitawasaidia watu kuanza kushughulikia njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu.

Uhusiano Kati ya Uwakilishi wa Mungu ya Ayubu na Shetani na Malengo ya Kazi ya Mungu

Ingawaje watu wengi sasa wanatambua kwamba Ayubu alikuwa mtimilifu na mnyofu na kwamba alimcha Mungu na kujiepusha na maovu, utambuzi huu hauwapi uelewa mkubwa zaidi wa nia ya Mungu. Wakati huohuo wakionea wivu ubinadamu na ushughulikaji wa Ayubu, wanamuuliza Mungu swali lifuatalo: Ayubu alikuwa mtimilifu na mnyofu sana, watu walimpenda sana, kwa hivyo kwa nini Mungu akamkabidhi kwa Shetani na kumpitishia maumivu haya makali? Maswali kama hayo yanatarajiwa kuwepo katika mioyo ya watu wengi—au, kushuku huku ndiko hasa swali katika mioyo ya watu wengi. Kwa sababu kushuku huku kumeshangaza watu wengi sana, lazima tuliwasilishe swali hili waziwazi na kulielezea kikamilifu.
Kila kitu ambacho Mungu anafanya kinahitajika, na kina umuhimu usio wa kawaida, kwani kila kitu anachofanya ndani ya binadamu kinahusu usimamizi wake na wokovu wa mwanadamu. Kiasili kazi ambayo Mungu alimfanyia Ayubu si tofauti, ingawaje Ayubu alikuwa mtimilifu na mnyofu mbele ya macho ya Mungu kwa maneno mengine, licha ya kile ambacho Mungu anafanya au mbinu ambazo Anatumia kufanya, licha ya gharama, au lengo Lake, kusudio la hatua Zake halibadiliki. Kusudio Lake ni kuweza kumshughulikia binadamu ili maneno ya Mungu yaingie ndani yake, mahitaji ya Mungu, na mapenzi ya Mungu kwa binadamu; kwa maneno mengine, ni kufanyia kazi huyu binadamu ili vyote ambavyo Mungu Anasadiki kuwa vizuri kulingana na hatua Zake, kumwezesha binadamu kuuelewa moyo wa Mungu na kufahamu kiini cha Mungu, na kumruhusu yeye kutii ukuu na mipangilio ya Mungu, na hivyo basi kumruhusu binadamu kuweza kufikia kiwango cha kumcha Mungu na kujiepusha na maovu—yote ambayo ni kipengele kimoja ya kusudio la Mungu katika kila kitu Anachofanya. Kipengele kingine ni kwamba, kwa sababu Shetani ndiye foili[e] na chombo cha huduma katika kazi ya Mungu, mara nyingi binadamu hukabidhiwa Shetani; hizi ndizo mbinu ambazo Mungu hutumia ili kuwaruhusu watu kuweza kuona maovu, ubaya, kudharaulika kwa Shetani katikati ya majaribio na mashambulizi ya Shetani na hivyo basi kuwasababisha watu kumchukia Shetani na kuweza kutambua kile ambacho ni kibaya. Mchakato huu unawaruhusu kwa utaratibu kuanza kuwa huru dhidi ya udhibiti wa Shetani, na dhidi ya mashtaka, uingiliaji kati, na mashambulizi ya Shetani—mpaka, kwa sababu ya maneno ya Mungu, maarifa yao na utiifu wao kwa Mungu, na imani yao kwa Mungu na kuweza kwao kumcha Mungu, wanashinda dhidi ya mashambulizi ya Shetani na kushinda dhidi ya mashtaka ya Shetani; hapo tu ndipo watakapokuwa wamekombolewa kabisa dhidi ya utawala wa Shetani. Ukombozi wa watu unamaanisha kwamba Shetani ameshindwa, unamaanisha kwamba wao si tena chakula kwenye kinywa cha Shetani— kwamba badala ya kuwameza wao, shetani amewaachilia. Hii ni kwa sababu watu kama hao ni wanyofu, kwa sababu wanayo imani, utiifu na wanamcha Mungu, na kwa sababu wako huru kabisa dhidi ya Shetani. Wamemleta Shetani aibu, wamemfanya kuonekana mjinga, na wamemshinda kabisa Shetani. Imani yao katika kumfuata Mungu, na utiifu na kumcha Mungu kunamshinda Shetani, na kumfanya Shetani kukata tamaa kabisa na wao. Watu kama hawa ndio ambao Mungu amewapata kwa kweli, na hili ndilo lengo kuu la Mungu katika kumwokoa binadamu. Kama wangependa kuokolewa, na wangependa Mungu awapate kabisa, basi wote wanaomfuata Mungu lazima wakabiliane na majaribio na mashambulizi yakiwa makubwa na hata madogo kutoka kwa Shetani. Wale wanaoibuka katika majaribio na mashambulizi haya na wanaweza kumshinda Shetani ni wale waliookolewa na Mungu. Hivi ni kusema kwamba wale waliookolewa na Mungu ni wale ambao wamepitia majaribio ya Mungu, na ambao wamejaribiwa na kushambuliwa na Shetani mara nyingi. Wale waliookolewa na Mungu wanayaelewa mapenzi na mahitaji ya Mungu, na wanaweza kuukubali ukuu na mipangilio ya Mungu na hawaachi njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu katikati ya majaribio ya Shetani. Wale waliookolewa na Mungu wanamiliki uaminifu, wao ni wakarimu, na wanaweza kutofautisha upendo na chuki, wanayo hisia ya haki na urazini, na wanaweza kumtunza Mungu na kuthamini sana kila kitu ambacho ni cha Mungu. Watu kama hao hawatekwi bakunja, kufanyiwa upelelezi, kushtakiwa au kudhulumiwa na Shetani, wako huru kabisa, wamekombolewa na kuachiliwa kabisa. Ayubu alikuwa mtu kama huyo mwenye uhuru na huu ndio umuhimu hasa wa kwa nini Mungu alimkabidhi kwa Shetani.
Ayubu alidhulumiwa na Shetani, lakini pia aliweza kupata uhuru na ukombozi wa milele, na kupata haki ya kutowahi kukabidhiwa tena kwa upotovu, unyanyasaji, na mashtaka ya Shetani, na badala yake kuishi katika nuru ya udhibiti wa Mungu usio na pingamizi na kuishi katikati ya baraka kutoka kwa Mungu. Hakuna ambaye angechukua au kuangamiza, au kupata haki hii. Ilipewa kwa Ayubu kutokana na imani, bidii, na utiifu wake kwa na kumcha Mungu; Ayubu alilipia gharama ya maisha yake ili kuweza kupata shangwe na furaha duniani, ili kufanikiwa kupata haki na kuweza kustahili, kama ilivyoamriwa mbinguni na kutambuliwa na dunia, ili kumwabudu Muumba bila ya uingiliaji kati kama kiumbe wa kweli wa Mungu duniani. Hivyo pia ndivyo yalivyokuwa matokeo makubwa zaidi ya majaribio yaliyovumiliwa na Ayubu.
Wakati watu bado hawajaokolewa, maisha yao mara nyingi yanaingiliwa kati na hata kudhibitiwa na, Shetani. Kwa maneno mengine, watu ambao hawajaokolewa ni wafungwa wa Shetani, hawana uhuru, hawajaachiliwa na Shetani, hawajafuzu wala kustahili kumwabudu Mungu, na wanafuatiliwa kwa karibu na kushambuliwa kwa ukali na Shetani. Watu kama hawa hawana furaha ya kuzungumzia, hawana haki ya uwepo wa kawaida wa kuzungumzia, na zaidi hawana heshima ya kuzungumzia. Ni pale tu unaposimama imara na kupigana na Shetani, kwa kutumia imani yako katika Mungu na utiifu kwake, pamoja na kumcha Mungu kama silaha ambazo utatumia kupigana vita vya maisha na mauti dhidi ya Shetani, kiasi cha kwamba utamshinda kabisa Shetani na kumsababisha kukata tamaa na kuwa mwoga kila anapokuona wewe, ili aache kabisa mashambulizi na mashtaka yake dhidi yako—hapo tu ndipo utakapookolewa na kuwa huru. Kama umeamua kutengana kabisa na Shetani lakini huna silaha zitakazokusaidia kupigana na Shetani, basi bado utakuwa katika hatari; kwa kadri muda unaposonga, baada ya wewe kuteswa na Shetani kiasi cha kwamba huna hata usuli wa nguvu uliobakia ndani mwako, lakini bado hujaweza kuwa na ushuhuda, bado hujajifungua kabisa kuwa huru dhidi ya mashtaka na mashambulizi ya Shetani dhidi yako, basi utakuwa na tumaini dogo la wokovu. Mwishowe, wakati hitimisho la kazi ya Mungu itakapotangazwa, bado utakuwa katika mashiko ya Shetani, usiweze kujiachilia kuwa huru, na hivyo hutawahi kuwa na fursa au tumaini. Matokeo yake, hivyo basi, ni kwamba watu kama hao watakuwa mateka kabisa wa Shetani.

Kubali Mitihani ya Mungu, Shinda Majaribio ya Shetani, na Ruhusu Mungu Kupata Nafsi Yako Nzima

Wakati wa kazi wa utoaji Wake wa kudumu na msaada kwa binadamu, Mungu anaambia binadamu kuhusu wa mapenzi Yake na mahitaji Yake yote, na anaonyesha vitendo Vyake, tabia, na kile Anacho na alicho kwa binadamu. Lengo ni kuweza kumtayarisha binadamu ili awe na kimo, na kumruhusu binadamu kupata ukweli mbalimbali kutoka kwa Mungu wakati anaendelea kumfuata Yeye— ukweli ambao ni silaha alizopewa binadamu na Mungu ambazo atatumia kupigana na Shetani. Hivyo akiwa na silaha hizo, binadamu lazima akabiliane na mitihani ya Mungu. Mungu anazo mbinu na njia nyingi za kumjaribu binadamu, lakini kila mojawapo inahitaji “ushirikiano” wa adui wa Mungu: Shetani. Hivi ni kusema, baada ya kumpa binadamu silaha ambazo atatumia kupigana na shetani, Mungu anamkabidhi binadamu kwa Shetani na kuruhusu Shetani “kujaribu” kimo cha binadamu. kama binadamu anaweza kufanikiwa dhidi ya uundaji wa vita vya Shetani, kama anaweza kutoroka mizunguko ya Shetani na bado akaishi, basi mwanadamu atakuwa ameupita mtihani. Lakini kama binadamu atashindwa kuondoka kwenye uundaji wa vita vya Shetani, na kujinyenyekeza kwa Shetani, basi hatakuwa ameupita mtihani. Haijalishi ni kipengele kipi cha binadamu ambacho mungu anachunguza, kigezo ni kama binadamu atasimama imara katika ushuhuda wake atakaposhambuliwa na Shetani au la, kujua kama amemuacha Mungu au la na akajisalimisha na akajinyenyekeza kwa Shetani baada ya kunaswa na Shetani. Inaweza kusemekana kwamba, iwapo binadamu anaweza kuokolewa au la yote haya yanategemea kama anaweza kumzidi na kumshinda Shetani, na kama ataweza kupata uhuru au la yanategemea kama anaweza kuinua, yeye binafsi, silaha alizopewa na Mungu ili kushinda utumwa wa Shetani, na kumfanya Shetani kuwacha kabisa tumaini na kumwacha pekee. Kama Shetani ataliacha tumaini na kumwachilia mtu, hii inamaanisha kwamba Shetani hatawahi tena kujaribu kuchukua mtu huyu kutoka kwa Mungu hatawahi tena kumshtaki na kuingilia kati mtu huyu, hatawahi tena kutaka kumtesa au kumshambulia; mtu kama huyu tu ndiye atakuwa kwa kweli amepatwa na Mungu. Huu ndio mchakato mzima ambao Mungu anapata watu.

Onyo na Upataji Nuru Ulilotolewa kwa Vizazi vya Baadaye Na Ushuhuda wa Ayubu

Huku wakielewa mchakato ambao Mungu anampata kabisa mtu, watu wataweza pia kuelewa nia na umuhimu wa Mungu kumpeleka Ayubu kwa Shetani. Watu hawasumbuliwi tena na maumivu makali ya Ayubu, na wanatambua upya umuhimu wake. Hawawi na wasiwasi tena kuhusu kama wao wenyewe watapitia majaribio sawa na yale ya Ayubu, na hawapingi tena au kukataa tena ujio wa majaribio ya Mungu. Imani, utiifu, na ushuhuda wake Ayubu wa kushinda Shetani, vyote hivi vimekuwa ni chanzo cha msaada mkubwa na himizo kwa watu. Kwa Ayubu, wanaona tumaini la wokovu wao binafsi, na wanaona kwamba kupitia kwa imani na utiifu kwa na kumcha Mungu, inawezekana kabisa kushinda Shetani, na kumshinda Shetani. Wanaona kwamba mradi tu waukubali ukuu na mipangilio ya Mungu, na kumiliki uamuzi na imani ya kutomwacha Mungu baada ya kupoteza kila kitu, basi wanaweza kumletea Shetani aibu na hali ya kushindwa, na kwamba wanahitaji tu kumiliki uamuzi na ustahimilivu wa kusimama imara katika ushuhuda wao—hata kama itamaanisha kupoteza maisha yao—ili Shetani aweze kuaibika na kurejea nyuma haraka. Ushuhuda wa Ayubu ni onyo kwa vizazi vya baadaye, na onyo hili linawaambia kwamba kama hawatamshinda Shetani, basi hawatawahi kuweza kujiondolea mashtaka na uingiliaji kati wa Shetani, na wala hawatawahi kuweza kutoroka dhulma na mashambulizi ya Shetani. Ushuhuda wa Ayubu ulipatia nuru vizazi vya baadaye. Upatiaji Nuru huu unafunza watu kwamba ni pale tu wanapokuwa watimilifu na wanyofu ndipo watakapoweza kumcha Mungu na kujiepusha na maovu; unawafunza kwamba ni pale tu wanapomcha Mungu na kujiepusha na maovu ndipo watapoweza kuwa na ushuhuda wenye udhabiti na wa kipekee kwa Mungu; pale tu watakapokuwa na ushuhuda dhabiti na wakipekee wa Mungu ndipo hawatawahi kudhibitiwa na Shetani, na kuishi katika mwongozo na ulinzi wa Mungu—na hapo tu ndipo watakapokuwa wameokolewa kwa kweli. Hulka ya Ayubu na ufuatiliaji wake wa maisha unafaa kuigwa na kila mmoja anayefuata wokovu. Kile alichoishi kwa kudhihirisha katika maisha yake yote na mwenendo wake wakati wa majaribio yake ni hazina yenye thamani kwa watu wote wanaotaka kufuata njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu.

Ushuhuda wa Ayubu Waleta Tulizo kwa Mungu

Nikikwambia sasa kwamba Ayubu ni mtu mzuri, huenda usiweze kutambua maana yaliyomo kwenye maneno haya, na huenda usiweze kung’amua mawazo yaliyopo katika yale maneno Niliyoyaongea kwa ujumla; lakini subiri mpaka siku ile utakapokuwa umepitia majaribio sawa na au yale yanayofanana na yale ambayo Ayubu alipitia, wakati utakapokuwa umepitia magumu, wakati utakapokuwa umepitia majaribio wewe binafsi yaliyopangiliwa kwa ajili yako na Mungu, wakati utakapojitolea kila kitu ulichonacho, na kuvumilia udhalilishaji na ugumu, ili kuweza kushinda Shetani na kuwa na ushuhuda kwa Mungu katikati ya majaribio hayo yote—basi utaweza kutambua maana ya maneno haya Ninayoyaongea. Wakati huo, utahisi kwamba wewe ni duni kuliko Ayubu, utahisi namna Ayubu alivyo mzuri, na kwamba anastahili kuigwa; wakati huo utakapowadia, utatambua namna ambavyo maneno yale ya kimapokeo yaliyozungumzwa na Ayubu yalivyo muhimu kwa yule aliyepotoka na anayeishi kwenye nyakati hizi, na utatambua namna ambavyo ilivyo vigumu kwa watu wa leo kuweza kutimiza kile Ayubu alitimiza. Unapohisi kuwa ni vigumu, utatambua na kuona namna ambavyo moyo wa Mungu ulivyo na dukuduku na wasiwasi, utatambua namna bei aliyolipa Mungu kuwapata watu kama hao ilivyo ya juu kupata watu kama hao, na jinsi lilivyo tukio la thamani kufanywa na kutekelezwa na Mungu kwa wanadamu. Kwa sababu sasa umeyasikia maneno haya, unao uelewa sahihi na ukadiriaji wa kweli kuhusu Ayubu? Katika macho yako, Ayubu alikuwa kweli mtu mtimilifu na mnyofu aliyejiepusha na maovu? Nasadiki kwamba watu wengi bila shaka watasema, ndio. Kwani ukweli kuhusu zile hatua ambazo Ayubu alichukua na kufichua haziwezi kupingwa na binadamu au Shetani yeyote. Hizo ndizo ithibati zenye nguvu zaidi kuhusu ushindi wa Ayubu dhidi ya Shetani. Ithibati hii ilitolewa kwa Ayubu, na ndio ushuhuda wa kwanza uliopokelewa na Mungu. Hivyo, wakati Ayubu aliposhinda majaribio ya Shetani na kuwa na ushuhuda kwa Mungu, Mungu aliona tumaini kwake Ayubu, na moyo wake ulitulizwa na Ayubu. Tangu uumbaji mpaka wakati wa Ayubu, huu ndio ulikuwa wakati wa kwanza ambao Mungu kwa kweli alipitia na kujua tulizo lilikuwa nini, na nini iliyokuwa maana ya kutulizwa na binadamu, na ndio uliokuwa wakati wa kwanza ambao Alikuwa ameona, na kupata, ushuhuda wa kweli uliotokana na Yeye.
Ninaamini kwamba, baada ya kuusikia ushuhuda wa Ayubu na simulizi za vipengele mbalimbali vya Ayubu, wengi wa watu watakuwa na mipango ya njia iliyo mbele yao. Hivyo, pia, Ninaamini kwamba watu wengi zaidi walio na wasiwasi na woga wataanza kwa utaratibu kuwa watulivu katika mwili na akili zao, na wataanza kuhisi tulizo, hatua kwa hatua. …
Vifungu vilivyo hapa chini ni simulizi pia kumhusu Ayubu. Wacha tuendelee kusoma.
4. Ayubu Amesikia Kuhusu Mungu kwa Kusikiliza juu ya Sikio
(Ayubu 9:11) “Tazama, anapita karibu nami, na mimi simwoni: Tena anapita kwenda mbele, lakini mimi simtambui.”
(Ayubu 23:8-9) “Tazama, naenda mbele, lakini hayuko huko; narudi nyuma, lakini siwezi kumwona; Katika mkono wa kushoto, anapofanya kazi, lakini siwezi kumwona: anajificha katika upande wa mkono wa kuume, hata siwezi kumwona.”
(Ayubu 42:2-6) “Najua ya kwamba unaweza kufanya mambo yote, na ya kuwa hakuna kusudi lako linaloweza kuzuilika. Ni nani yeye anayeficha ushauri bila maarifa? Hivyo, nimesema maneno nisiyoyafahamu; mambo ya ajabu kwangu nisiyoyajua. Sikiliza, nakusihi, nami nitazungumza: Nitauliza kutoka kwako, nawe ujiweke wazi kwangu. Nimesikia habari zako, kwa kusikia kwa masikio: Lakini sasa jicho langu linakuona. Ndiyo sababu najichukia nafsi yangu, na kutubu kwenye vumbi na jivu.”

Ingawaje Mungu Hajajifichua kwa Ayubu, Ayubu Anasadiki Mamlaka Ya Mungu

Ni nini Nguvu za maneno haya? Je, Yupo yeyote aliyetambua kwamba kunayo ukweli hapa? Kwanza, ni vipi ambavyo Ayubu alijua kwamba Mungu yupo? Na ni vipi alivyojua kwamba mbingu na ardhi na mambo yote yanatawaliwa na Mungu? Kunayo kifungu kinachojibu maswali haya mawili: Nimesikia habari zako, kwa kusikia kwa masikio: Lakini sasa jicho langu linakuona. Ndiyo sababu najichukia nafsi yangu, na kutubu kwenye vumbi na jivu (Ayubu 42:5-6). Kutokana na maneno haya tunajifunza kwamba, badala ya kuwa kwamba alimwona Mungu kwa macho yake mwenyewe, Ayubu alikuwa amejifunza kuhusu Mungu kutoka kwa hekaya. Ni katika hali hizi ndipo alipoanza kutembea njia ya kumfuata Mungu, na baadaye akathibitisha uwepo wa Mungu katika Maisha yake, na miongoni mwa mambo yote. Kunayo ukweli usiopingika hapa—nayo ni gani? Licha ya kuweza kufuata njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu, Ayubu alikuwa hajawahi kumwona Mungu. Katika haya, hakuwa sawa na watu wa leo? Ayubu alikuwa hajawahi kumwona Mungu, matokeo yake ni kwamba ingawaje alikuwa amewahi kumsikia Mungu, hakujua ni wapi Mungu alikuwa, au ni vipi Mungu alifanana, au ni nini Mungu alikuwa akifanya, mambo ambayo ni ya kibinafsi; tukiongea bila mapendeleo, ingawaje alimfuata Mungu, Mungu alikuwa hajawahi kumwonekania yeye au kumzungumzia yeye. Je, huu si ukweli? Ingawaje Mungu alikuwa hajaongea na Ayubu au kumpa amri zozote, Ayubu alikuwa ameuona uwepo wa Mungu, na kutazama ukuu Wake miongoni mwa mambo yote na katika hekaya ambazo Ayubu alikuwa amesikia kumhusu Mungu kwa kusikia kwa sikio, na baadaye alianza maisha ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Hizi ndizo zilizokuwa asili na mchakato ambao Ayubu alimfuata Mungu. Lakini haikujalisha ni vipi alivyomcha Mungu na kujiepusha na maovu, ni vipi ambavyo alishikilia uadilifu wake, bado Mungu alikuwa hajawahi kujitokeza kwake. Hebu tuisome kifungu hiki. Alisema, “Tazama, anapita karibu nami, na mimi simwoni: Tena anapita kwenda mbele, lakini mimi simtambui.” (Ayubu 9:11). Yale ambayo maneno haya yanasema ni kwamba Ayubu huenda alihisi Mungu karibu naye au pengine hakuhisi— lakini alikuwa hajawahi kuweza kumwona Mungu. Kunazo nyakati ambapo alifikiria Mungu akipita mbele yake au akitenda, au akimwongoza binadamu, lakini alikuwa hajawahi kujua. Mungu humjia binadamu wakati hatarajii; binadamu hajui ni lini Mungu atamjia, au ni wapi anapomjia yeye, kwa sababu binadamu hawezi kumwona Mungu, kwa hivyo, kwa binadamu Mungu amefichwa kutoka kwake.

Imani ya Ayubu Katika Mungu Haitikisiki kwa Sababu Mungu Amefichwa Kutoka Kwake

Katika kifungu kifuatacho ya maandiko, Ayubu anasema, “Tazama, naenda mbele, lakini hayuko huko; narudi nyuma, lakini siwezi kumwona; Katika mkono wa kushoto, anapofanya kazi, lakini siwezi kumwona: anajificha katika upande wa mkono wa kuume, hata siwezi” (Ayubu 23:8-9). Katika simulizi hii, tunajifunza kwamba katika hali alizopitia Ayubu, Mungu alikuwa amefichwa kutoka kwake wakati wote huo; Mungu alikuwa hajajitokeza waziwazi kwake yeye, na alikuwa hajamzungumzia waziwazi maneno yoyote kwake yeye, lakini katika moyo wake Ayubu alikuwa na ujasiri wa uwepo wa Mungu. Alikuwa siku zote amesadiki kwamba Mungu huenda anatembea na yeye au huenda Anatenda akiwa kando yake, na kwamba ingawaje hakuweza kumwona Mungu, Mungu alikuwa kando yake yeye akitawala mambo yake yote. Ayubu alikuwa hajawahi kumwona Mungu, lakini aliweza kuwa mkweli katika imani yake, jambo ambalo hakuna mtu yeyote aliwahi kuweza kufanya. Na kwa nini watu hawakuweza kufanya hivyo? Kwa sababu Mungu hakuongea na Ayubu, au kujitokeza kwake yeye, na kama asingekuwa amesadiki kwa kweli, asingeweza kuendelea, wala asingeweza kushikilia njia hiyo ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Je, huu si ukweli? Unahisi vipi unaposoma kumhusu Ayubu akisema maneno haya? Unahisi kwamba utimilifu na unyofu wa Ayubu, na haki yake mbele ya Mungu, ni kweli, na wala si kupiga chuku kwa upande wa Mungu? Ingawaje Mungu alimshughulikia Ayubu kwa njia sawa na watu wengine, na hakujitokeza wala kuongea na yeye, Ayubu bado alishikilia ubinadamu wake, bado alisadiki ukuu wa Mungu, na, isitoshe, mara kwa mara alitoa sadaka za kuteketezwa na kuomba mbele ya Mungu kutokana na hofu yake ya kumkosea Mungu. Katika uwezo wa Ayubu wa kumcha Mungu bila ya kuwahi kumwona Mungu, tunaona ni kiasi kipi alichopenda mambo mazuri na ni vipi imani yake ilivyokuwa thabiti na ya kweli. Hakukataa uwepo wa Mungu kwa sababu Mungu alikuwa amefichwa kutoka kwake, wala hakupoteza imani yake na kumkataa Mungu kwa sababu hakuwahi kumwona Yeye. Badala yake, katikati ya kazi fiche ya Mungu ya kutawala mambo yote, alikuwa ametambua uwepo wa Mungu na akahisi ukuu wa Mungu na Nguvu za Mungu. Hakukata tamaa katika kuwa mnyofu kwa sababu Mungu alikuwa amefichwa, wala hakuiacha njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu kwa sababu Mungu alikuwa hajawahi kujitokeza kwake yeye. Ayubu alikuwa hajawahi kuuliza kwamba Mungu aonekane waziwazi kwake ili kuthibitisha uwepo Wake, kwani alikuwa tayari ametangaza ukuu wa Mungu miongoni mwa mambo yote na alisadiki kwamba alikuwa amepata baraka na neema ambazo wengine hawakuwa wamepata. Ingawaje Mungu alibakia fiche kwake yeye, imani ya Ayubu kwa Mungu haikuwahi kutikisika. Hivyo, alivuna kile ambacho hakuna yeyote aliwahi kuvuna. Idhini ya Mungu na baraka za Mungu.

Ayubu Abariki Jina la Mungu na Wala Hafikirii Baraka au Janga

Kunayo ukweli ambao haurejelewi katu kwenye hadithi za maandiko kuhusu Ayubu, ambayo ndio itakayokuwa zingatio letu leo. Ingawaje Ayubu alikuwa hajawahi kumwona Mungu au kusikia maneno ya Mungu kwa masikio yake mwenyewe, Mungu alikuwa na nafasi katika moyo wa Ayubu. Na mwelekeo wa Ayubu kwa Mungu ulikuwa upi? Ulikuwa, kama ulivyorejelewa awali, “libarikiwe jina la Bwana.” Baraka yake kwa jina la Mungu haikuwa ya masharti, wala isiyofuzu, na bila ya sababu. Tunaona kwamba Ayubu alikuwa ameukabidhi moyo wake kwa Mungu, na kuuruhusu kudhibitiwa na Mungu; kila kitu alichofikiria, kila kitu alichoamua, na kila kitu alichopangilia katika moyo wake kilikuwa wazi kwa Mungu na wala moyo wake haukuwa umefungwa kuzuia Mungu. Moyo wake haukumpinga Mungu, na hakuwahi kuuliza Mungu kumfanyia chochote au kumpa chochote yeye, na wala hakuwa na matamanio yasiyo ya kawaida ambayo angepata chochote kutoka kwa kumwabudu Mungu. Ayubu hakuzungumzia biashara na Mungu, na wala hakutoa ombi lolote au madai yoyote kwa Mungu. Hali yake ya kusifia jina la Mungu ilikuwa kwa sababu ya nguvu kuu na mamlaka ya Mungu katika kutawala mambo yote, na haikutegemea kama alipata baraka au alipigwa na janga. Aliamini kwamba haijalishi kama Mungu anawabariki watu au analeta janga kwao, mamlaka na nguvu vyote havitabadilika, na hivyo, haikujalisha hali za mtu, jina la Mungu linafaa kusifiwa. Kwamba binadamu amebarikiwa na Mungu ni kwa sababu ya ukuu wa Mungu, na wakati janga lilipompata binadamu, hivyo, pia ni kwa sababu ya ukuu wa Mungu. Nguvu na mamlaka ya Mungu vyote vinatawala na kupangilia kila kitu cha binadamu; matukio yasiyo ya kawaida kuhusu utajiri wa binadamu ni maonyesho ya nguvu na mamlaka ya Mungu, na licha ya maoni yake mtu, jina la Mungu linafaa kusifiwa. Haya ndiyo ambayo Ayubu alipitia na kuishia kujua katika miaka ya maisha yake. Fikira na matendo yote ya Ayubu vyote vilifikia masikio ya Mungu na vikawasili mbele ya Mungu, na vikaonekana kuwa muhimu na Mungu. Mungu aliyapenda sana maarifa haya ya Ayubu na akathamini sana Ayubu kwa kuwa na moyo kama huo. Moyo huu ulisubiria amri ya Mungu siku zote, na pahali pote, na haijalishi ni muda au mahali gani ulikaribisha chochote kile kilichomsibu. Ayubu hakutoa mahitaji yoyote kwa Mungu. Kile alichohitaji kutoka kwake kilikuwa kusubiria, kukubali, kukabiliana na kutii mipangilio yote iliyotoka kwa Mungu; Ayubu alisadiki hili kuwa wajibu wake, na ndio hasa kile ambacho Mungu Alitaka. Ayubu alikuwa hajawahi kumwona Mungu wala kumsikiliza Akiongea mambo yoyote, akitoa amri zozote, akiyatoa mafundisho yoyote, au kuelekeza yeye kuhusu chochote. Kwa maneno ya leo, kwake yeye kuweza kumiliki mwelekeo kama huo kwa Mungu, wakati Mungu alikuwa hajampa nuru, mwongozo, au toleo kuhusiana na ukweli—hili lilikuwa lenye thamani sana, na kwake yeye kuonyesha mambo kama hayo kulitosha kwa Mungu, na ushuhuda wake ulipongezwa na Mungu, na kutunzwa na Mungu. Ayubu alikuwa hajawahi kumwona Mungu au kumsikia Mungu binafsi akitamka mafundisho yoyote kwake yeye, lakini kwa Mungu moyo wake na yeye mwenyewe vyote vilikuwa vyenye thamani zaidi kuliko wale watu ambao, mbele ya Mungu waliweza tu kuongea kuhusu nadharia kuu, ambao waliweza tu kujigamba na kuongea kuhusu kutoa sadaka lakini walikuwa hawajawahi kuwa na maarifa ya kweli ya Mungu na walikuwa hawajawahi kumcha Mungu kwa kweli. Kwani moyo wa Ayubu ulikuwa safi, na haukufichwa kuonekana na Mungu, na ubinadamu wake ulikuwa wenye uaminifu na ukarimu, na alipenda haki na kile kilichokuwa kizuri. Binadamu kama huyu pekee aliyemiliki moyo kama huo na ubinadamu ndiye aliyeweza kufuata njia ya Mungu, na kuwa na uwezo wa kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Binadamu kama huyo angeona ukuu wa Mungu, angeona mamlaka na nguvu Yake, na angeweza kutimiza utiifu kwa ukuu Wake na mipangilio. Binadamu tu kama huyo ndiye angeweza kusifu jina la Mungu kwa kweli. Hii ni kwa sababu hakuangalia kama Mungu angembariki yeye au Angemletea janga, kwa sababu alijua kwamba kila kitu kinadhibitiwa na mkono wa Mungu, na kwamba binadamu kuwa na wasiwasi ni ishara ya ujinga, kutojua, na kutoweza kufikiria vyema, kuwa na shaka katika ukweli wa ukuu wa Mungu juu ya mambo yote, na ya kutomcha Mungu. Maarifa ya Ayubu hasa ndiyo ambayo Mungu alitaka. Hivyo basi, Ayubu alikuwa na maarifa makubwa ya kinadharia kumhusu Mungu kuliko wewe? Kwa sababu kazi na matamko ya Mungu wakati huo yalikuwa machache, halikuwa jambo rahisi kutimiza maarifa ya Mungu. Mafanikio kama hayo ya Ayubu hayakukuwa jambo dogo. Alikuwa hajapitia kazi ya Mungu wala hakuwahi kusikia Mungu akiongea, au kuuona uso wa Mungu. Kwamba aliweza kuwa na mwelekeo kama huo kwa Mungu yalikuwa ni hasa matokeo yaliyoonyesha ubinadamu wake na ufuatiliaji wake wa kibinafsi, ubinadamu na ufuatiliaji ambao haujamilikiwa na watu leo. Hivyo, katika enzi hiyo, Mungu alisema, “hakuna kama yeye duniani, mtu mkamilifu na aliye mnyoofu mwenye kumcha Mungu, na kuuepuka uovu.” Katika enzi hiyo, Mungu alikuwa tayari amefanya ukadiriaji wake Ayubu, na alikuwa amefikia hitimisho fulani. Ungekuwa ukweli zaidi kwa kiasi kipi hii leo?

Ingawaje Mungu Amefichwa Kutoka kwa Binadamu, Matendo Yake Miongoni mwa Mambo Yote Yanatosha Binadamu Kumjua Yeye

Ayubu alikuwa hajauona uso wa Mungu, wala kusikia matamshi yaliyoongelewa na Mungu, isitoshe yeye mwenyewe binafsi alikuwa hajapitia kazi ya Mungu, lakini kumcha kwake Mungu na ushuhuda aliyokuwa nao wakati wa majaribio kunashuhudiwa na kila mmoja, na kunapendwa, kunafurahiwa, na kupongezwa na Mungu na watu wakayaonea wivu na kuvutiwa nayo, na vilevile, wakaimba nyimbo zao za sifa. Hakukuwepo chochote kikubwa au kisicho cha kawaida kuhusu maisha yake: Kama vile tu mtu yeyote wa kawaida, aliishi maisha yasiyo ya kina, akienda kufanya kazi wakati wa macheo na akirudi nyumbani kupumzika wakati wa magharibi. Tofauti ni kwamba wakati wa miongo hii mbalimbali isiyo ya kina, alipata maono kuhusu njia ya Mungu, na akatambua na kuelewa nguvu kubwa na ukuu wa Mungu, kuliko mtu yeyote mwingine.. Hakuwa mwerevu zaidi kuliko mtu yeyote wa kawaida, maisha yake hayakukuwa sanasana yenye ushupavu, wala, zaidi, yeye hakuwa na mbinu maalum zisizoonekana. Kile alichomiliki, hata hivyo, kilikuwa ni hulka iliyokuwa na uaminifu, upole, unyofu, na hulka iliyopenda kutopendelea na haki, na iliyopenda mambo mazuri—hakuna kati ya haya aliyomiliki yalimilikiwa na watu wa kawaida wengi. Alitofautisha kati ya upendo na chuki, alikuwa na hisia ya haki, hakukubali kushindwa na alikuwa hakati tamaa, na alikuwa mwenye bidii katika fikira zake, na hivyo basi wakati wake usio wa kina duniani aliyaona mambo yote yasiyo ya kawaida ambayo Mungu alikuwa amefanya, na akauona ukubwa, utakatifu, na uhaki wa Mungu, aliona kujali kwa Mungu, neema yake, na ulinzi wake wa binadamu, na kuona utukufu na mamlaka ya Mungu mwenye mamlaka zaidi. Sababu ya kwanza iliyomfanya Ayubu kuweza kupata mambo haya yaliyokuwa zaidi ya mtu yeyote wa kawaida ilikuwa ni kwa sababu alikuwa na moyo safi, na moyo wake ulimilikiwa na Mungu na kuongozwa na Muumba. Sababu ya pili ilikuwa ni ufuatiliaji wake: ufuatiliaji wake wa kuwa maasumu, na mtimilifu, na mtu aliyekubaliana na mapenzi ya Mbinguni, aliyependwa na Mungu, na kujiepusha na uovu. Ayubu alimiliki na kufuata mambo haya huku akiwa hawezi kumwona Mungu au kusikia maneno ya Mungu; ingawaje alikuwa hajawahi kumwona Mungu, alikuwa amejua mbinu ambazo Mungu alitawala mambo yote, na kuelewa hekima ambayo Mungu anatumia ili kufanya hivyo. Ingawaje alikuwa hajawahi kusikia maneno ambayo yalikuwa yametamkwa na Mungu, Ayubu alijua kwamba matendo ya kutuna binadamu na kuchukua kutoka kwa binadamu yote yalitoka kwa Mungu. Ingawaje miaka ya maisha yake haikuwa tofauti na ile ya mtu wa kawaida, hakuruhusu ukosefu wa kina hiki cha maisha yake kuathiri maarifa yake ya ukuu wa Mungu juu ya mambo yote, au kuathiri kufuata kwake kwa njia za kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Katika macho yake, sheria za mambo yote zilijaa matendo ya Mungu na ukuu wa Mungu ungeweza kuonekana katika sehemu yoyote ya maisha ya mtu. Alikuwa hajamwona Mungu lakini aliweza kutambua kwamba Matendo ya Mungu yako kila pahali, na katika wakati wake usiokuwa wa kina duniani, katika kila kona ya maisha yake aliweza kuona na kutambua matendo ya kipekee na ya maajabu ya Mungu, na aliweza kuona mipangilio ya ajabu ya Mungu. Ufiche na kimya cha Mungu hakikuzuia utambuzi wa Ayubu wa matendo ya Mungu, wala hakikuathiri maarifa yake kuhusu ukuu wa Mungu juu ya mambo yote. Maisha yake yalikuwa utambuzi wa ukuu na mipangilio ya mungu, ambaye amefichwa miongoni mwa mambo yote, katika maisha yake ya kila siku. Katika maisha yake ya kila siku alisikia pia na kuelewa sauti na maneno ya moyoni, ambayo Mungu, akiwa kimya miongoni mwa mambo yote, alionyesha kupitia kwa kutawala Kwake kwa sheria ya mambo yote. Unaona, basi, kwamba kama watu wanao ubinadamu sawa na ufuatiliaji kama Ayubu, basi wanaweza kupata utambuzi na maarifa sawa kama Ayubu, na kupata ule uelewa na maarifa sawa ya ukuu wa Mungu juu ya mambo yote kama Ayubu. Mungu alikuwa hajajionyesha kwa Ayubu au kuongea na yeye, lakini Ayubu aliweza kuwa mtimilifu na mnyofu, na pia aliweza kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Kwa maneno mengine, bila ya Mungu kuweza kujitokeza kwa au kuongea na binadamu, matendo ya Mungu miongoni mwa mambo yote na ukuu Wake juu ya mambo yote ni tosha kwa binadamu ili kuweza kuwa na ufahamu wa uwepo wa Mungu, nguvu na mamlaka ya Mungu ni tosha kumfanya binadamu huyu kufuata njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Kwa sababu binadamu wa kawaida kama vile Ayubu aliweza kutimiza hali ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu, basi kila mtu wa kawaida anayemfuata Mungu anafaa pia kuweza kufanya hivyo. Ingawaje maneno haya yanaweza kusikika ni kana kwamba ni hitimisho ya kimantiki. Hii haikiuki sheria ya mambo. Bado ukweli haujalingana na matarajio: Kumcha Mungu na kujiepusha na maovu, kunaweza kuonekana, ni hifadhi ya Ayubu na Ayubu pekee. Kwa kutaja “kumcha Mungu na kujiepusha na maovu,” watu hufikiria kwamba hii inafaa tu kufanywa na Ayubu, ni kana kwamba njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu ilikuwa imebandikwa jina la Ayubu na haikuhusika na watu wengine. Sababu ya hii ni wazi: Kwa sababu Ayubu tu ndiye aliyemiliki hulka iliyokuwa na uaminifu, ukarimu, na nyofu, na iliyopenda kutopendelea na haki na mambo yaliyokuwa mazuri, hivyo ni Ayubu tu ambaye angeweza kufuata njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Lazima nyinyi wote mkuwe mmeelewa matokeo hapa—ambayo ni kwamba kwa sababu hakuna yule anayemiliki ubinadamu ulio na uaminifu, ukarimu, na unyofu, na ule ambao unapenda kutopendelea na haki na ule ambao ni mzuri, hakuna mtu anayeweza kumcha Mungu na kujiepusha na maovu, na hivyo hawezi kupata furaha ya Mungu au kusimama imara katikati ya majaribio. Ambayo pia inamaanisha kwamba, bila kujumuisha Ayubu, watu wote wangali wamefungwa na kunaswa na Shetani, wote wanashtakiwa, wanashambuliwa, na kudhulumiwa na Shetani, na wale ambao Shetani anajaribu kumeza, na wote hawana uhuru, ni wafungwa ambao wametekwa nyara na Shetani.

Kama Moyo wa Binadamu Unao Uadui na Mungu, Anawezaje Kumcha Mungu na Kujiepusha na Maovu

Kwa sababu watu wa leo hawamiliki ubinadamu sawa na Ayubu, na je kiini cha asili yao, na mwelekeo wao kwa Mungu? Wanamcha Mungu? Wanajiepusha na maovu? Wale wasiomcha Mungu na kujiepusha na maovu wanaweza kujumuishwa tu kwa maneno manne: Ni adui za Mungu. Mara nyingi mnasema maneno haya, lakini hamjawahi kujua maana yake halisi. Maneno “ni adui za Mungu” yanayo kiini ndani yake: Hayasemi kwamba Mungu anamuona binadamu kama adui, lakini kwamba binadamu anamuona Mungu kama adui. Kwanza, wakati watu wanapoanza kusadiki Mungu, ni nani asiyekuwa na nia, motisha na maono yake binafsi? Ingawaje sehemu moja yao inasadiki uwepo wa Mungu, na imeona uwepo wa Mungu, imani yao katika Mungu bado inayo hiyo motisha, na nia yao kuu ya kusadiki Mungu ni kupokea baraka Zake na mambo wanayotaka. Katika uzoefu wa watu katika maisha yao, mara nyingi wanafikiria ndani yao, nimetoa familia yangu na ajira yangu kwa Mungu, na Amenipatia nini? Lazima niongezee na kuthibitisha haya—je, nimepokea baraka zozote hivi majuzi? Nimetoa mengi sana wakati huu, nimekimbia na kukimbia na kuteswa sana—je Mungu amenipa ahadi zozote baada ya haya? Je Amekumbuka matendo yangu mazuri? Mwisho wangu utakuwa vipi? Ninaweza kuzipokea baraka za Mungu? … Kila mtu kila wakati, na mara nyingi hufanya hesabu kama hizi ndani ya mioyo yao, na wao wanatoa madai yao kwa Mungu yanayoonyesha motisha yao na malengo na mipango. Hivi ni kusema, ndani ya moyo wake binadamu siku zote anamweka Mungu majaribuni, siku zote anaunda njama kumhusu Mungu, na kila wakati anabishana na Mungu kuhusu kesi yake na kujaribu kumfanya Mungu kutoa kauli, ili aweze kuona kama Mungu anaweza kumpa kile anachotaka au hawezi. Wakati huohuo akimfuata Mungu, binadamu hamchukulii mungu kama Mungu. Siku zote amejaribu kufanya mipango na Mungu, akitoa madai bila kusita kwake Yeye na hata akimsukuma Yeye kwa kila hatua, akijaribu kupiga hatua ya maili licha ya kupewa inchi moja. Wakati huohuo akijaribu kuunda mipango na Mungu, binadamu pia anabishana na Yeye, na wapo hata watu ambao, wakati majaribio yanapowapata au wanapojipata katika hali ya kuteketea, mara nyingi wanakuwa wanyonge, wananyamaza na kuzembea katika kazi yao, na wanajaa malalamiko kuhusu Mungu. Tangu wakati ule alipoanza kusadiki Mungu, binadamu amemchukulia Mungu kama alama ya pembe inayoonyesha wingi wa neema, kisu cha Kijeshi cha Uswisi, na amejichukulia yeye mwenyewe kuwa mdaiwa mkubwa zaidi wa Mungu, ni kana kwamba kujaribu kupata baraka na ahadi kutoka kwa Mungu ni haki yake ya asili na jukumu, huku jukumu la Mungu likiwa ni kulinda na kutunza binadamu na kumtoshelezea. Huu ndio uelewa wa kimsingi wa “imani katika Mungu” wa wale wote wanaosadiki Mungu, na uelewa wao wa kina zaidi wa dhana ya imani katika Mungu. Kutoka kwenye kiini cha asili ya binadamu hadi katika ufuatiliaji wake wa kibinafsi, hakuna kitu chochote kinachohusiana na kumcha Mungu. Nia ya binadamu kwa kusadiki Mungu huenda isiwe na uhusiano na kuabudu Mungu. Hivi ni kusema kwamba, binadamu hajawahi kufikiria wala kuelewa kwamba imani katika Mungu inahitaji kumcha Mungu, na kumwabudu Mungu. Kwa mujibu wa haya yote, kiini cha binadamu ni wazi. Na kiini hicho ni nini? Ni kwamba moyo wa binadamu una kijicho, unabeba udanganyifu na ujanja, haupendi mambo ya kutopendelea na haki, au kile kilicho kizuri, nao ni wenye kuleta dharau na ulafi. Moyo wa binadamu usingeweza kumzuia Mungu zaidi, hajaupatia Mungu kamwe. Mungu hajawahi kuona moyo wa kweli wa binadamu, wala hajawahi kuabudiwa na binadamu. Haijalishi ni gharama gani ambayo Mungu amelipia, au ni kiasi kipi cha kazi Anachofanya, au ni kiwango kipi Anachompa binadamu, binadamu anabakia yule asiyeona hayo yote, na hajali. Binadamu hajawahi kumpa Mungu moyo wake, anataka tu kujali moyo wake wenyewe, kufanya uamuzi wake mwenyewe—mada madogo ambayo ni kwamba binadamu hataki kufuata njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu, au kutii ukuu na mipangilio ya Mungu, wala hataki kumwabudu Mungu kama Mungu. Hivyo ndivyo mwanadamu anavyozungukwa na hali mbalimbali leo. Sasa hebu tumwangalie tena Ayubu. Kwanza kabisa, aliweza kufanya mpango na Mungu? Alikuwa na nia zozote fiche katika kushikilia njia ile ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu? Wakati huo, je, Mungu alikuwa ameongea na yeyote kuhusu mwisho ujao? Wakati huo, Mungu alikuwa hajatoa ahadi zozote kwa yeyote kuhusu mwisho, na ilikuwa katika hali hii ndipo Ayubu aliweza kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Je, watu wa leo wanaweza kulinganishwa na Ayubu? Kunazo tofauti nyingi, wanapatikana katika nyanja tofauti. Ingawaje Ayubu hakuwa na maarifa mengi ya Mungu, alikuwa ameutoa moyo wake kwa Mungu na ulimilikiwa na Mungu. Hakuwahi kupanga chochote na Mungu, na hakuwa na matamanio yoyote ya zaidi au madai kwa Mungu; badala yake, alisadiki kwamba “Bwana alitoa na Bwana atatwaa.” Hii ndiyo alikuwa ameona na kupata kutokana na kushikilia ukweli njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu wakati wa miaka yake mingi ya maisha. Vilevile, alikuwa amepata matokeo ya “Vipi? Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya?” Sentensi hizi mbili ndizo ambazo alikuwa ameona na akaja kujua kutokana na mwelekeo wake wa utiifu kwa Mungu katika uzoefu wa maisha yake, na ndizo pia zilikuwa silaha zake zenye nguvu zaidi ambazo alitumia akashinda majaribio ya Shetani, na msingi wa yeye kusimama imara katika ushuhuda kwa Mungu. Wakati huu, bado unamwona Ayubu kama mtu mzuri? Je unatumaini kuwa mtu kama huyo? Unaogopa kupitia majaribio ya Shetani? Unaamua kumwomba Mungu ili aweze kukupitisha kwenye majaribio kama haya ya Ayubu? Bila shaka watu wengi wasingethubutu kuombea mambo kama hayo. Ni wazi, basi, kwamba imani yako ni ndogo ya kusikitiwa; ikilinganishwa na ile ya Ayubu, imani yako haistahili kutajwa. Nyinyi ndio adui za Mungu, hamchi Mungu, hamwezi kusimama imara katika ushuhuda kwa Mungu, na hamwezi kushangilia dhidi ya mashambulio, mashtaka, na majaribio ya Shetani. Ni nini kinachowafanya kufuzu ili kupokea ahadi za Mungu? Baada ya kusikia hadithi ya Ayubu na kuelewa nia ya Mungu katika kuokoa binadamu, na maana ya wokovu wa binadamu, je mnayo sasa imani ya kukubali majaribio sawa na ya Ayubu? Hamfai kuwa na kusudio kidogo, ili mjiruhusu kufuata njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu?

Msiwe na Wasiwasi Wowote Kuhusu Majaribio ya Mungu

Baada ya kuupokea ushuhuda kutoka kwa Ayubu kufuatia mwisho wa majaribio yake, Mungu aliamua kwamba angepata kundi au zaidi ya kundi—la watu kama Ayubu, ilhali aliamua kutowahi tena kumruhusu Shetani kushambulia au kunyanyasa mtu yeyote mwingine kwa kutumia mbinu ambazo alikuwa amemjaribu, akamshambulia na kumnyanyasa Ayubu, kwa kucheza karata na Mungu; Mungu hakumruhusu Shetani tena kufanya mambo kama hayo kwa binadamu ambaye ni mnyonge, mjinga, na asiyejua—ilikuwa tosha kwamba Shetani alikuwa amemjaribu Ayubu! Kutomruhusu Shetani kuwanyanyasa watu vyovyote anavyotaka ndiyo rehema ya Mungu. Kwa Mungu, ilitosha kwamba Ayubu alikuwa ameteseka majaribio na minyanyaso ya Shetani. Mungu hakumruhusu Shetani tena kufanya mambo kama hayo, kwani maisha na kila kitu cha watu wanaomfuata Mungu yanatawaliwa na kupangiliwa na Mungu, na Shetani hastahili kutawala waliochaguliwa na Mungu apendavyo—unafaa kuwa wazi kuhusu hoja hii! Mungu anajali kuhusu unyonge wa binadamu, na kuelewa ujinga na kutojua kwake. Ingawaje, ili binadamu aweze kuokolewa kabisa, lazima Mungu amkabidhi kwa Shetani, Mungu hayuko radhi kumwona tena binadamu akichezewa tena kama kikaragosi na Shetani na kunyanyaswa na Shetani na hataki kumwona binadamu siku zote akiteseka. Binadamu aliumbwa na Mungu, na inaeleweka kikamilifu kwamba Mungu anatawala na anapangilia kila kitu cha binadamu; hili ni jukumu la Mungu na mamlaka ambayo Mungu anatawala mambo yote! Mungu hamruhusu Shetani kunyanyasa na kutumia vibaya binadamu apendavyo, Hamruhusu Shetani kutumia mbinu mbalimbali za kumpotosha binadamu, na vilevile, Hamruhusu Shetani kuingilia kati ukuu wa Mungu wa binadamu, wala Hamruhusu Shetani kukanyaga na kuangamiza Sheria ambazo Mungu anatawalia mambo yote, kutosema chochote kuhusu kazi kuu ya Mungu ya kusimamia na kuwaokoa wanadamu! Wale ambao Mungu anataka kuokoa na wale ambao wanaweza kuwa na ushuhuda kwa Mungu, ndio msingi na hali halisi ya kazi ya Mungu ya mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita, pamoja na bei ya jitihada zake katika kazi yake ya miaka elfu sita. Mungu anawezaje kuwakabidhi watu hawa kwa Shetani hivihivi.
Watu mara nyingi wanakuwa na wasiwasi kuhusu na wana uoga ya majaribio ya Mungu, ilhali siku zote wanaishi katika mtego wa Shetani na kuishi katika maeneo hatari ambapo wanashambuliwa na kunyanyaswa na Shetani—lakini hawaogopi na hawashangazwi. Nini kinaendelea? Imani ya binadamu katika Mungu ni finyu mno kwa mambo anayoweza kuona. Hana shukrani hata chembe kuhusu upendo na kujali kwa Mungu kwa binadamu, au wema Wake na utiliaji maanani kwa binadamu. Lakini kwa hofu na wasiwasi kidogo kuhusu majaribio, hukumu na kuadibu kwa Mungu na adhama na hasira Yake, binadamu hana hata chembe cha uelewa wa nia nzuri za Mungu. Kwa kutajwa kwa majaribio, watu wanahisi ni kana kwamba Mungu anazo nia nyingine zisizo wazi na hata baadhi wanasadiki kwamba Mungu ana mipango ya maovu, wasijue hata kile ambacho Mungu atawafanyia; hivyo, wakati huohuo kutaka kuwa watiifu kabisa kwa ukuu na mipangilio ya Mungu, wanafanya kila wawezalo kuzuia na kupinga ukuu wa Mungu juu ya binadamu na mipangilio kwa binadamu, kwani wanasadiki kwamba kama hawatakuwa makini watapotoshwa na Mungu, na kama hawatakuwa na mshikilio thabiti ya hatima yao binafsi, basi kila kitu walichonacho kinaweza kuchukuliwa na Mungu, na maisha yao huenda hata yakaisha. Binadamu yumo kwenye kambi la Shetani, lakini hawi na wasiwasi kamwe kuhusu kunyanyaswa na Shetani, na ananyanyaswa na Shetani lakini haogopi kamwe kutekwa nyara na Shetani. Siku zote anasema kwamba anaukubali wokovu wa Mungu, ilhali hajawahi kumwamini Mungu au kusadiki kwamba Mungu atamwokoa kwa kweli binadamu kutoka kwenye makucha ya Shetani. Kama, sawa na Ayubu, binadamu anaweza kunyenyekea kwa mipango na mipangilio ya Mungu na anaweza kuitoa nafsi nzima kwa mikono ya Mungu, basi hatima ya binadamu haitakuwa sawa na ile ya Ayubu—kupokea baraka za Mungu? Kama binadamu anaweza kukubali na kunyenyekea Sheria ya Mungu, nini kipo cha kupoteza? Na hivyo Napendekeza kwamba uwe makinifu kwa vitendo vyako, utahadhari na kila kitu ambacho kiko karibu kukufanyikia wewe. Usiwe wa pupa au msukumo na umshughulikie Mungu na watu, masuala, vitu alivyokupangilia kwa namna mshawasha unavyokupeleka, au kulingana na nafsi yako ya kiasili au kufikiria na dhana zako; lazima uwe mmakinifu katika vitendo vyako na lazima uombe na utafute zaidi, kuepuka kuchochea hasira ya Mungu. Kumbuka hili!
Kisha, tutaangalia vile Ayubu alikuwa baada ya majaribio yake.
5. Ayubu Baada ya Majaribio yake
(Ayubu 42:7-9) Basi ikawa, baada ya BWANA kumwambia Ayubu maneno hayo, BWANA akamwambia huyo Elifazi Mtemani, Hasira yangu inawaka juu yako, na juu ya hao rafiki zako wawili: kwa kuwa nyinyi hamjanena yaliyo sawa kunihusu, kama alivyofanya mtumishi wangu Ayubu. Basi sasa, jichukulieni ng’ombe waume saba, na kondoo waume saba, muende kwa mtumishi wangu Ayubu, na mjitolee sadaka ya kuteketezwa; na mtumishi wangu Ayubu atawaombea: kwa kuwa yeye Nitamkubali: nisije Nikawatendea kulingana na makosa yenu, hivi kwamba nyinyi hamkunena maneno yaliyo sawa kunihusu, kama alivyofanya mtumishi wangu Ayubu. Hivyo Elifazi, Mtemani, na Bildadi, Mshuhi, na Sofari, Mnaamathi, wakaenda, wakafanya vile BWANA alivyowaamuru: BWANA pia akamkubali Ayubu.
(Ayubu 42:10) Kisha BWANA akaugeuza uteka wa Ayubu, alipowaombea rafiki zake: BWANA pia akampa Ayubu mara mbili kuliko hayo aliyokuwa nayo kabla.
(Ayubu 42:12) Basi hivyo BWANA akaubariki mwisho wa Ayubu zaidi ya mwanzo wake: kwani alikuwa na kondoo kumi na nne elfu, na ngamia elfu sita, na jozi za ng’ombe elfu moja, na punda wa kike elfu moja.
(Ayubu 42:17) Basi Ayubu akafa, akiwa mzee sana na mwenye kujawa na siku.

Wale Wanaomcha Mungu na Kujiepusha Na Maovu Wanatazamiwa kwa Utunzwaji na Mungu, Huku Wale Walio Wajinga Wanaonekana kuwa Wanyenyekevu

Katika Ayubu 42:7-9, Mungu Anasema kwamba Ayubu ni mtumishi Wake. Matumizi Yake ya neno “mtumishi” kumrejelea Ayubu yanaonyesha umuhimu wa Ayubu katika moyo Wake; ingawaje Mungu hakumwita Ayubu kitu chenye heshima zaidi, jina hili halikuwa na uamuzi wowote katika umuhimu wa Mungu ndani ya moyo wa Ayubu. “Mtumishi” hapa ni jina la lakabu la Mungu kwa Ayubu. Marejeleo mbali mbali ya Mungu kwa “mtumishi wangu Ayubu” yanaonyeshwa ni vipi ambavyo Alipendezwa na Ayubu, ingawaje Mungu hakuongea kuhusu maana ya nyuma ya neno “Mtumishi,” ufafanuzi wa Mungu wa neno “mtumishi” unaweza kuonekana kupitia kwa maneno Yake katika kifungu hiki ya maandiko. Kwanza Mungu alimwambia Elifazi Mtemani: “Hasira yangu inawaka juu yako, na juu ya hao rafiki zako wawili: kwa kuwa nyinyi hamjanena yaliyo sawa kunihusu, kama alivyofanya mtumishi wangu Ayubu.” Maneno haya ndiyo ya mara ya kwanza kwa Mungu kuambia watu waziwazi kwamba alikuwa amekubali yale yote yaliyokuwa yamesemwa na kufanywa na Ayubu baada ya majaribio ya Mungu kwake yeye, na ndiyo mara ya kwanza Alikuwa amedhibitisha waziwazi ukweli na usahihi wa yale yote Ayubu alikuwa amefanya na kusema. Mungu alikuwa na ghadhabu kwake Elifazi na wengine kwa sababu ya mazungumzo yao yasiyokuwa sahihi na mabovu, kwa sababu, kama Ayubu wasingeweza kuona mwonekano wa Mungu au kusikia maneno aliyoongea katika maisha yao ilhali Ayubu alikuwa na maarifa sahihi Kumhusu Mungu, huku nao waliweza tu kukisia bila mpango kuhusu Mungu, kukiuka mapenzi ya Mungu na kujaribu uvumilivu wake kwa yote waliyoyafanya Kwa hivyo, wakati sawa na kukubali yote yalikuwa yamefanywa na kusemwa na Ayubu, Mungu alizidi kuongeza hasira zake kwa wale wengine, kwani ndani yao Hakuweza tu kuuona uhalisia wowote wa kumcha Mungu, lakini pia Hakusikia chochote cha kumcha Mungu kwa yale waliyoyasema. Na hivyo Mungu kwa kilichofuata Alisema madai yafuatayo kuwahusu. “Basi sasa, jichukulieni ng’ombe waume saba, na kondoo waume saba, muende kwa mtumishi wangu Ayubu, na mjitolee sadaka ya kuteketezwa; na mtumishi wangu Ayubu atawaombea: kwa kuwa yeye Nitamkubali: Nisije Nikawatendea kulingana na makosa yenu.” Katika kifungu hiki Mungu anamwambia Elifazi na wengine kufanya jambo ambalo litakomboa dhambi zao, kwani upumbavu wao ulikuwa ni dhambi dhidi ya Yehova Mungu, na hivyo wangelazimika kutoa sadaka zilizoteketezwa ili kusuluhisha makosa yao. Sadaka zilizoteketezwa mara nyingi zinatolewa kwa Mungu, lakini kile kisicho cha kawaida kuhusu sadaka hizi zilizoteketezwa ni kwamba zilitolewa kwa Ayubu. Ayubu alikubaliwa na Mungu kwa sababu alikuwa nao ushuhuda kwa Mungu wakati wa majaribio yake. Rafiki hawa wa Ayubu, nao walifichuliwa katika kipindi kile cha majaribio yake, kwa sababu ya upumbavu wao, walishutumiwa na Mungu na wakachochea hasira ya Mungu, na wanafaa kuadhibiwa na Mungu—kuadhibiwa kwa kutoa sadaka zilizoteketezwa mbele ya Ayubu—na baadaye Ayubu aliwaombea wao ili kuiondoa ile adhabu na hasira ya Mungu kwao. Nia ya Mungu ilikuwa ni kuwaaibisha wao, kwani hawakuwa watu waliomcha Mungu na wa kujiepusha na maovu, na walikuwa wameshutumu uadilifu wa Ayubu. Kwa upande mmoja, Mungu alikuwa akiwaambia kwamba Hakukubali vitendo vyao lakini Alikubali pakubwa na Alifurahishwa na Ayubu; kwa upande mwingine, Mungu alikuwa akiwaambia kwamba kukubaliwa na Mungu kunampandisha daraja binadamu mbele ya Mungu, kwamba binadamu anachukiwa na Mungu kwa sababu ya upumbavu wake, na anamkosea Mungu kwa sababu ya hali hii, na anakuwa mdogo na mbaya mbele ya macho ya Mungu. Huu ndio ufafanuzi uliotolewa na Mungu kuhusu watu wa aina mbili, ni mielekeo ya Mungu kwa watu hawa wa aina mbili na ni ufafanuzi wa Mungu kuhusu thamani na hadhi ya watu wa aina hizi mbili. Ingawaje Mungu alimwita Ayubu mtumishi Wake, ndani ya macho ya Mungu huyu “mtumishi” alikuwa mpendwa Wake, na alipewa mamlaka ya kuwaombea wengine na kuwasamehe makosa yao. “Mtumishi huyu” aliweza kuongea moja kwa moja na Mungu na kuwa na mgusano wa moja kwa moja na Mungu, hadhi yake ilikuwa ya juu zaidi na ya heshima zaidi kuliko ya wale wengine. Haya ndiyo maana halisi ya neno “mtumishi” kama Mungu alivyoongea. Ayubu alipewa heshima hii maalum kwa sababu ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu, na sababu iliyofanya wengine kutoitwa watumishi na Mungu ni kwa sababu hawakumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Mielekeo hii miwili tofauti na maalum ya Mungu ndiyo mielekeo yake kwa watu wa aina mbili: Wale wanaomcha Mungu na kujiepusha na maovu wanakubaliwa na Mungu, na wanaonekana wenye thamani mbele ya macho Yake, huku wale walio wapumbavu hawajamcha Mungu na hawawezi kujiepusha na maovu, na hawawezi kupokea kibali cha Mungu, mara nyingi wanachukiwa na kushutumiwa na Mungu, na ni wadogo mbele ya macho ya Mungu.

Mungu Anamtawaza Mamlaka Ayubu

Ayubu aliwaombea rafiki zake, na baadaye, kwa sababu ya maombi ya Ayubu, Mungu hakushughulika nao kama walivyostahili juu ya upumbavu wao —Hakuwaadhibu au kuchukua adhabu yoyote dhidi yao. Na sababu ilikuwa nini? Kwa sababu kulingana na wao maombi yanayohusu mtumishi wa Mungu, Ayubu, yalikuwa yamefikia masikio Yake; Mungu naye aliwasamehe kwa sababu Aliyakubali maombi ya Ayubu. Na tunaona nini katika haya? Wakati Mungu anapombariki mtu, Anampa tuzo nyingi, na si tu zile za kidunia, pia: Mungu anawapa pia mamlaka, na Kuwaambia kuwa wanastahili kuwaombea wengine, naye Mungu husahau na kusamehe makosa ya hao watu kwa sababu Anayasikia maombi haya. Haya ndiyo mamlaka yenyewe ambayo Mungu alimpa Ayubu. Kupitia kwa maombi ya Ayubu kusitisha kushutumiwa kwao, Yehova Mungu aliwaletea aibu wale watu wapumbavu— ambayo, bila shaka, ndiyo iliyokuwa adhabu Yake maalum kwa Elifazi na wale wengine.

Ayubu Anabarikiwa kwa Mara Nyingine Tena na Mungu, na Hashtakiwi Tena na Shetani

Miongoni mwa matamko ya Yehova Mungu ni maneno kwamba “hivi kwamba nyinyi hamkunena maneno yaliyo sawa kunihusu, kama alivyofanya mtumishi wangu Ayubu.” Ni nini kile ambacho Ayubu alikuwa amesema? Ni kile tulichozungumzia awali, pamoja na kile ambacho kurasa nyingi za maneno kwenye kitabu cha Ayubu ambacho Ayubu amerekodiwa kuwa alisema. Katika kurasa hizi nyingi za maneno, Ayubu hajawahi hata mara moja kuwa na malalamiko au mashaka yoyote kumhusu Mungu. Yeye anasubiria tu matokeo. Ni kusubiri huku ambako ndiko mwelekeo wake wa uaminifu, matokeo yake yakiwa, na kutokana na maneno aliyomwambia Mungu, Ayubu alikubaliwa na Mungu. Alipovumilia majaribio na kupata mateso ya Ugumu, Mungu alikuwa upande wake na ingawaje ugumu wake hukupunguzwa na uwepo wa Mungu, Mungu aliona kile Alichotaka kuona na kusikia kile Alichotaka kusikia. Kila mojawapo ya vitendo na maneno ya Ayubu kiliweza kufikia macho na masikio ya Mungu; Mungu alisikia na Akaona—na hii ni ukweli. Maarifa ya Ayubu kumhusu Mungu na fikira zake kumhusu Mungu katika moyo wake wakati huo, katika kipindi hicho, hazikuwa kwa hakika kama zile za watu wa leo, lakini katika muktadha wa wakati huo, Mungu aliweza kutambua bado kila kitu alichokuwa amesema, kwa sababu tabia yake na fikira zake ndani ya moyo wake, na kile alichokuwa ameelezea na kufichua, kilikuwa tosha kwa mahitaji Yake. Katika kipindi hiki cha wakati ambao Ayubu alipitia majaribio, yale ambayo alifikiria katika moyo wake na kuamua kufanya yaliweza kumwonyesha Mungu matokeo, yale ambayo yalimtosheleza Mungu, na baadaye Mungu akayaondoa majaribio ya Ayubu, Ayubu akaibuka kutoka kwenye matatizo yake, na majaribio yake yakawa yameondoka yasiwahi kumpata tena yeye. Kwa sababu Ayubu alikuwa tayari amepitia majaribio, na akawa amesimama imara katika majaribio haya, na akamshinda kabisa Shetani, Mungu alimpatia baraka ambazo kwa kweli alistahili. Kama ilivyorekodiwa katika Ayubu 42:10, 12, Ayubu alibarikiwa kwa mara nyingine tena, na akabarikiwa zaidi ya hata mara ya kwanza. Wakati huu Shetani alikuwa amejiondoa, na hakusema tena au kufanya chochote, na kutoka hapo kuenda mbele Ayubu hakuhitilafiana tena na Shetani au kushambulia Shetani, na Shetani hakutoa mashtaka tena dhidi ya baraka za Mungu kwa Ayubu.

Ayubu Atumia Nusu ya Mwisho ya Maisha Yake Katikati ya Baraka za Mungu

Ingawaje baraka Zake wakati huo zilikuwa tu zinajumuisha kondoo, ng'ombe, ngamia, na rasilimali za dunia, na kadhalika, baraka ambazo Mungu alitaka kumpa Ayubu katika moyo Wake zilikuwa mbali zaidi na hizi. Kwa wakati huo ziliporekodiwa, ni aina gani za ahadi za milele ambazo Mungu alipenda kumpa Ayubu? Katika baraka Zake kwa Ayubu, Mungu hakugusia au kutaja kuhusu mwisho wake, na haijalishi umuhimu au cheo ambacho Ayubu alishikilia ndani ya moyo wa Mungu, kwa ujumla Mungu alikuwa akitambua katika baraka Zake. Mungu hakutangaza mwisho wa Ayubu. Hii inamaanisha nini? Wakati huo, wakati mpango wa Mungu ulikuwa bado haujafikia sehemu ya kutangaza mwisho wa binadamu, mpango huo ulikuwa bado uingie kwenye awamu ya mwisho ya kazi yake, Mungu hakutaja chochote kuhusu mwisho, huku akimpa binadamu baraka za rasilimali za dunia tu. Maana ya hii ni kwamba nusu ya mwisho ya maisha ya Ayubu ilipita katikati ya baraka za Mungu na hii ndiyo iliyomfanya kuwa tofauti na wale watu wengine—lakini kama wao alizeeka, na kama mtu yeyote yule wa kawaida siku ilifika ambapo aliuambia ulimwengu kwaheri. Na hivyo imerekodiwa kwamba “Basi Ayubu akafa, akiwa mzee sana na mwenye kujawa na siku” (Ayubu 42:17). Nini maana ya “akafa… mwenye kujawa na siku” hapa? Katika enzi ya kabla Mungu kutangaza mwisho, Mungu alimwekea Ayubu matarajio ya maisha ambayo angeishi, na wakati umri huo ulipofikiwa Alimruhusu Ayubu kuondoka kiasili kutoka ulimwengu huu. Kutoka baraka ya pili ya Ayubu hadi kifo chake, Mungu hakuongezea ugumu wowote. Kwake Mungu, kifo cha Ayubu kilikuwa cha kiasili, na pia kilihitajika, kilikuwa kitu cha kawaida sana na wala si hukumu au shutuma. Alipokuwa hai, Ayubu alimwabudu na kumcha Mungu; kuhusiana na ni aina gani ya mwisho aliyokuwa nayo kufuatia kifo chake, Mungu hakusema chochote, wala kutoa maoni yoyote kuhusu hilo. Mungu ni mwenye busara katika kile Anachosema na kufanya, na maudhui na kanuni za maneno na vitendo vyake yanalingana na awamu ya kazi Yake na kipindi Anachofanyia kazi. Ni aina gani ya mwisho ambayo mtu kama Ayubu alikuwa nayo katika moyo wa Mungu? Je, Mungu alikuwa amefikia aina yoyote ya uamuzi katika moyo Wake? Bila shaka Alikuwa! Ni vile tu hili lilikuwa halijulikani kwa binadamu; Mungu hakutaka kumwambia binadamu wala Hakuwa na nia yoyote ya kumwambia binadamu. Na hivyo, kwa kuongea juujuu tu, Ayubu alikufa akiwa amejawa na siku, na hivyo ndivyo maisha ya Ayubu yalivyokuwa.

Gharama Iliyoishi kwa kudhihirishwa na Ayubu Wakati wa Maisha Yake

Je Ayubu aliishi maisha ya thamani? Thamani yake ilikuwa wapi? Ni kwa nini inasemwa kwamba aliishi maisha yenye thamani? Kwa binadamu, thamani yake ilikuwa gani? Kutoka katika mtazamo wa binadamu, aliwawakilisha wanadamu ambao Mungu alitaka kuokoa, kwa kuwa na ushuhuda wa kipekee kwa Mungu mbele ya Shetani na watu wa ulimwengu. Alitimiza wajibu ambao ulistahili kutimizwa na kiumbe wa Mungu, na kuweka mfano halisi wa kuigiwa, na kutenda kama kielelezo, kwa wale wote ambao Mungu angependa kuwaokoa, akiruhusu watu kuona kwamba inawezekana kabisa kushinda Shetani kwa kumtegemea Mungu. Nayo thamani yake kwa Mungu ilikuwa gani? Kwa Mungu, thamani ya maisha ya Ayubu ilikuwa ndani ya uwezo wake wa kumcha Mungu, kumwabudu Mungu, kutolea ushuhuda vitendo vya Mungu, na kusifu vitendo vya Mungu, kumpa Mungu tulizo na kitu cha kufurahia; kwa Mungu, thamani ya maisha ya Ayubu ilikuwa pia kwa namna ambavyo, kabla ya kifo chake, Ayubu alipitia majaribio na kushinda Shetani, na akawa na ushuhuda wa kipekee kwa Mungu mbele ya Shetani na watu wa ulimwengu, akimtukuza Mungu miongoni mwa wanadamu, akiutuliza moyo wa Mungu na kuruhusu moyo wa Mungu wenye hamu kuyaona matokeo, na kuliona tumaini. Ushuhuda wake uliweka mfano wa kufuatwa kutokana na uwezo wake wa kusimama imara katika ushuhuda wa Mungu, na kuweza kumwaibisha Shetani kwa niaba ya Mungu, katika kazi ya Mungu ya kuwasimamia wanadamu. Je, hii si thamani ya maisha ya Ayubu? Ayubu alileta tulizo kwa moyo wa Mungu, alimpa Mungu kionjo cha furaha ya kutukuzwa, na akaanzisha mwanzo mzuri kwa mpango wa usimamizi wa Mungu. Na kuanzia hapo kuenda mbele jina la Ayubu likawa ishara ya utukuzaji wa Mungu na ishara ya kushinda kwa wanadamu dhidi ya Shetani. Kile Ayubu aliishi kwa kudhihirisha wakati wa maisha yake na ushindi wake wa kipekee dhidi ya Shetani milele utabakia ukifurahiwa mno na Mungu na utimilifu wake, unyofu, na hali yake ya kumcha Mungu itaheshimiwa na kuigwa na vizazi vitakavyokuja. Milele atafurahiwa mno na Mungu kama johari lisilo na makosa, wala dosari, na pia ndivyo alivyo na thamani ya kuthaminiwa sana na binadamu!
Kisha, hebu tuangalie kazi ya Mungu wakati wa Enzi ya Sheria.
D. Taratibu za Enzi ya Sheria.
1. Amri Kumi
2. Kanuni za Kujenga Madhabahu
3. Taratibu za Ushughulikiaji wa Watumishi
4. Taratibu za Wizi na Fidia
5. Kutimiza Mwaka wa Sabato na Karamu Tatu
6. Taratibu za Siku ya Sabato
7. Taratibu za Kutoa Sadaka
a. Sadaka zilizoteketezwa
b. Sadaka za Unga
c. Sadaka za Amani
d. Sadaka za Dhambi
e. Sadaka za Hatia
f. Taratibu za Sadaka za Kuhani (Aroni na Watoto Wake wa Kiume Waamrishwa Kutii)
1) Sadaka za Kuteketezwa na Kuhani
2) Sadaka za Unga na Kuhani
3) Sadaka za Dhambi na Kuhani
4) Sadaka za Hatia na Kuhani
5) Sadaka za Amani na Kuhani
8. Taratibu za Ulaji wa Sadaka na Kuhani
9. Wanyama Walio Halali na Wale Walio Haramu (Wale Wanaoweza na Wasioweza Kuliwa)
10. Taratibu za Utakasaji Wanawake Baada ya Kujifungua
11. Viwango vya Uchunguzi wa Ukoma
12. Taratibu kwa Wale Ambao Wameponywa Ukoma
13. Taratibu za Kuzitakasa Nyumba Zilizoambukizwa
14. taratibu za Wale Wanaougua Kisonono Kisicho cha Kawaida
15. Siku ya Upatanisho Wa Mungu na Binadamu Ambayo Lazima Iadhimishwe Mara Moja Kwa Mwaka
16. Sheria za Kuchinja Ng'ombe na Mbuzi
17. Kuzuiliwa kwa Mazoea Yafuatayo Yanayochukiza Ya Watu wa Mataifa (Si Kutenda Kujamiiana Kwa Maharimu, na Kadhalika)
18. Taratibu Ambazo Lazima Zifuatwe na Watu (“Utakuwa mtakatifu: kwani Mimi BWANA Mungu wako ni mtakatifu.”)
19. Kutendewa kwa Wale Wanaotoa Kafara Watoto Wao kwa Molka
20. Taratibu za Adhabu ya Uhalifu wa Uasherati
21. Sheria Zinazofaa Kufuatiliwa na Kuhani (Sheria za Tabia Yao Ya Kila Siku, Sheria za Matumizi ya Mambo matakatifu, Sheria za Kutoa Sadaka na Kadhalika)
22. Karamu Zinazofaa Kufuatiliwa (siku ya Sabato, Pentekoste, Siku ya Upatanisho wa Mungu na Binadamu kwa Maisha ya Kifo cha Yesu, na Kadhalika)
23. Taratibu Nyingine (Kuteketezwa kwa Taa, Mwaka wa Jubilii, Ukombozi wa Ardhi, Ulaji wa Viapo, Utoaji wa Zaka, na Kadhalika)

Taratibu za Enzi ya Sheria ni Thibitisho la Kweli la Maelekezo ya Mungu kwa Wanadamu Wote

Hivyo, umezisoma taratibu na kanuni hizi za Enzi ya Sheria, kweli? Je, taratibu hizi zinajumuisha mseto mpana? Kwanza, zinajumuisha Amri Kumi, na baadaye kuna taratibu za namna ya kujenga madhabahu, na kadhalika. Hizi zinafuatwa na taratibu za kuitimiza Sabato na kuzidumisha zile karamu tatu, na baadaye kuna taratibu za kutoa sadaka. Je, unaona ni aina ngapi za sadaka ambazo zimo? Kunazo sadaka zilizoteketezwa, sadaka za unga, sadaka za amani, sadaka za dhambi, na kadhalika, ambazo zinafuatwa na taratibu za sadaka za kuhani, zikiwemo sadaka zilizoteketezwa na sadaka za unga zilizotolewa na Kuhani, na aina nyingine za sadaka. Taratibu za nane ni za ulaji wa sadaka na Kuhani, na kisha kunazo taratibu zinazofaa kudumishwa wakati wa maisha ya watu. Kunayo masharti ya vipengele vingi vya maisha ya watu, kama vile taratibu zinazotawala kile wanachoweza au wasichoweza kula, kwa utakasaji wa wanawake baada ya wao kujifungua, na kwa wale ambao wameponywa ugonjwa wa ukoma. Katika taratibu hizi, Mungu Anafikia hadi kiwango cha kuzungumzia kuhusu ugonjwa, na kunazo hata sheria za kuchinja kondoo na ng’ombe, na kadhalika. Kondoo na ng'ombe waliumbwa na Mungu, na unafaa kuwachinja hata hivyo Mungu anakuambia kufanya hivyo; kunayo, bila shaka, sababu ya maneno ya Mungu, na ni sahihi bila shaka kutenda kama inavyokaririwa na Mungu, na kwa hakika itakuwa ya manufaa kwa watu! Kunazo pia karamu na sheria za kufuatwa, kama vile siku ya Sabato, Pasaka, na zaidi—Mungu aliweza kuzungumzia yote haya. Hebu tuangalie zile za mwisho: taratibu nyingine—kuteketezwa kwa taa, mwaka wa Jubilii, ukombozi wa ardhi, ulaji wa viapo, utoaji wa zaka, na kadhalika. Je, hizi zinajumuisha mseto mpana? Kitu cha kwanza cha kuzungumziwa ni suala la sadaka la watu, kisha kunazo taratibu za wizi na fidia, na udumishaji wa siku ya Sabato...; kila mojawapo ya maelezo ya maisha yanahusishwa.. Hivi ni kusema, wakati Mungu alianza kazi Yake rasmi ya mpango Wake wa usimamizi, Aliweka wazi taratibu nyingi ambazo zilifaa kufuatwa na binadamu. Taratibu hizi zilikuwa ili kumruhusu binadamu kuishi maisha ya kawaida ya binadamu hapa duniani, maisha ya kawaida ya binadamu ambayo hayajatenganishwa na Mungu na uongozi Wake. Mungu alimwambia binadamu kwanza namna ya kuunda madhabahu, namna ya kuyaunda madhabahu. Baada ya hapo, Alimwambia binadamu namna ya kutoa sadaka, na kuamuru namna ambavyo binadamu alifaa kuishi—kile alichofaa kutilia maanani katika maisha, kile alichofaa kutii, kile anachofaa na hafai kufanya. Kile Mungu alichoweka wazi kwa binadamu kilikuwa kinakubalika chote, na pamoja na tamaduni, taratibu, na kanuni hizi Aliwastanisha tabia ya watu, kuongoza maisha yao, kuongoza uanzishaji wao wa sheria za Mungu, kuwaongoza kuja mbele ya madhabahu ya Mungu, kuwaongoza katika kuishi maisha miongoni mwa mambo mengine yote ambayo Mungu alikuwa amemuumbia binadamu na yaliyomilikiwa na mpangilio na marudio ya mara kwa mara na ya kiasi. Kwanza Mungu alitumia taratibu na kanuni hizi rahisi kuweka vipimo kwa binadamu, ili hapa duniani binadamu aweze kuwa na maisha ya kawaida ya kumwabudu Mungu, aweze kuwa na maisha ya kawaida; hivi ndivyo yalivyo maudhui mahususi ya mwanzo wa mpango Wake wa usimamizi wa miaka elfu sita. Taratibu na sheria zinajumuisha maudhui mapana mno, yote ni maelezo ya mwongozo wa Mungu wa mwanadamu wakati wa Enzi ya Sheria, lazima yangekubaliwa na kuheshimiwa na watu waliokuwa wamekuja kabla ya Enzi ya Sheria, ni rekodi ya kazi iliyofanywa na Mungu katika Enzi ya Sheria, na ni ithibati ya kweli ya uongozi na mwongozo wa Mungu kwa wanadamu wote.

Wanadamu Hawatenganishwi Milele na Mafundisho na Matoleo ya Mungu

Katika taratibu hizi tunaona kwamba mwelekeo wa Mungu katika kazi Yake, katika usimamizi Wake, na kwa wanadamu ukiwa wa kumakinikia zaidi, wa ukweli, wa bidii, na wa kuwajibika. Anaifanya kazi ambayo lazima Afanye miongoni mwa wanadamu kulingana na hatua Zake, bila ya hitilafu hata kidogo, Akiongea maneno ambayo lazima aongee kwa wanadamu bila ya kosa au upungufu hata kidogo, Akimruhusu binadamu kuona kwamba hawezi kutenganishwa na uongozi wa Mungu, na Akimwonyesha namna ambavyo yale yote ambayo Mungu anafanya na kusema yalivyo muhimu kwa wanadamu. Licha ya kile ambacho binadamu alivyo katika enzi ijayo, kwa ufupi, wakati wa mwanzo kabisa—wakati wa Enzi ya Sheria—Mungu aliyafanya mambo haya rahisi. Kwa Mungu, dhana za watu kumhusu Mungu, ulimwengu na mwanadamu katika enzi hiyo zilikuwa za kidhahania na zisizoeleweka, na ingawaje walikuwa na fikra na nia fulani husika, zote zilikuwa hazina uwazi na si sahihi, na hivyo wanadamu walikuwa hawawezi kutenganishwa kutoka kwa mafundisho na matoleo ya Mungu kwao. Wanadamu wa mapema zaidi hawakujua chochote, na hivyo Mungu alilazimika kuanza kumfunza binadamu kutoka kwenye kanuni za juujuu na za kimsingi zaidi kwa minajili ya uwepo na taratibu zinazohitajika za kuishi, kutia moyoni mambo haya yote kwenye moyo wa binadamu kidogo kidogo, na kumpa binadamu uelewa wa Mungu kwa utaratibu, kutambua na kuelewa uongozi wa Mungu kwa utaratibu, na dhana ya kimsingi ya uhusiano kati ya binadamu na Mungu, kupitia kwa taratibu hizi na kupitia kwa sheria hizi, ambazo zilikuwa za maneno.. Baada ya kutimiza athari hii, ndipo tu Mungu aliweza, kidogo kidogo, kufanya kazi ambayo Angeweza kufanya baadaye, na hivyo taratibu hizi na kazi iliyofanywa na Mungu kwenye Enzi ya Sheria zikawa ndiyo msingi wa kazi Yake ya kuwaokoa wanadamu na hatua ya kwanza ya kazi katika mpango wa usimamizi wa Mungu. Ingawaje, kabla ya kazi ya Enzi ya Sheria, Mungu alikuwa ameongea naye Adamu, Hawa, na babu zao, amri na mafunzo hayo hayakuwa ya hatua kwa hatua sana au mahususi ili kutolewa moja baada ya nyingine kwa mwanadamu, na hayakuwa yameandikwa, wala hayakuwa taratibu. Hii ni kwa sababu, kwa wakati huo, mpango wa Mungu haukuwa umeenda mbali kiasi hicho; na Mungu alipokuwa amemwongoza binadamu hadi katika hatua hii tu ndipo Alipoweza kuongea taratibu hizi za Enzi ya Sheria, na kuanza kumfanya binadamu kuzitekeleza. Ulikuwa ni mchakato unaohitajika, na matokeo yasingeweza kuepukika. Tamaduni na taratibu hizi rahisi zinaonyesha binadamu hatua za usimamizi wa kazi ya Mungu na hekima ya Mungu inayofichuliwa katika mpango Wake wa usimamizi. Mungu anayajua maudhui yapi na mbinu zipi za kutumia ili kuanza, mbinu zipi za kutumia kuendelea na mbinu zipi za kutumia kumaliza ili aweze kupata kundi la watu lililo na ushuhuda Kwake Yeye, Aweze kupata kundi la watu walio na akili sawa na Yake. Anajua kile kilicho ndani ya binadamu, na kujua kile kinachokosa kwa binadamu, Anajua kile anachofaa kutoa, na namna Anavyofaa kumwongoza binadamu, na pia ndivyo Anavyojua kile binadamu anafaa na hafai kufanya. Binadamu ni kama kikaragosi: Ingawaje hakuwa na uelewa wowote wa mapenzi ya Mungu, alilazimika kuongozwa na kazi ya Mungu ya usimamizi, hatua kwa hatua hadi leo. Hakukuwa na kutodhihirika kokote katika moyo wa Mungu kuhusu kile Alichofaa kufanya; katika moyo Wake kulikuwa na mpango wazi na kamilifu kabisa, na Alitekeleza kazi hiyo ambayo Yeye mwenyewe alitaka kufanya kulingana na hatua Zake na mpango Wake, Akiendelea mbele kutoka katika hali ya juujuu hadi ile hali ya ndani kabisa. Ingawaje Hakuwa ameonyesha kazi ambayo Alifaa kufanya baadaye, kazi Yake ya baadaye bado iliendelea kutekelezwa na kuendelea mbele kulingana kabisa na mpango Wake, ambayo ni maonyesho ya kile Mungu anacho na alicho, na pia ni mamlaka ya Mungu. Licha ya ni awamu gani ya mpango Wake wa usimamizi ambayo Anafanya, tabia Yake na kiini chake kinamwakilisha Yeye mwenyewe—na hakuna kosa katika haya. Licha ya enzi, au awamu ya kazi, aina ya watu ambao Mungu anapenda, aina ya watu ambao Anachukia, tabia Yake, na kila kitu Alichonacho na kile ambacho Mungu ni hakitawahi kubadilika. Ingawaje taratibu na kanuni hizi ambazo Mungu alianzisha katika kazi ya Enzi ya Sheria zinaonekana rahisi na za juujuu kwa watu wa leo, na Ingawaje ni rahisi kuelewa na kutimiza, ndani ya hizo kunayo bado hekima ya Mungu, na kunayo bado tabia ya Mungu na kile Anacho na alicho. Kwani ndani ya taratibu hizi zinazoonekana rahisi, uwajibikaji na utunzaji wa Mungu kwa wanadamu unaonyeshwa, na kiini kizuri cha fikira zake, kumruhusu binadamu kutambua kwa kweli ukweli kwamba Mungu anatawala mambo yote na mambo yote yanadhibitiwa kwa mkono Wake. Haijalishi ni kiwango kipi cha maarifa ambacho wanadamu watajifunza au nadhari au mafumbo mangapi wanaelewa, kwa Mungu hakuna chochote kati ya hivi ambavyo vinaweza kusawazisha toleo Lake kwa, na uongozi wa mwanadamu; wanadamu milele hawatatenganishwa na mwongozo wa Mungu na kazi ya kibinafsi ya Mungu. Huu ndiyo uhusiano kati ya binadamu na Mungu usiotenganishwa. Licha ya kama Mungu anakupa amri, au taratibu, au Anakupa ukweli ili kuyaelewa mapenzi Yake, haijalishi ni nini Anachofanya, nia ya Mungu ni kumwongoza binadamu hadi katika siku nzuri ya kesho. Maneno yaliyotamkwa na Mungu na kazi Anayofanya ni ufunuo wa kipengele kimoja cha kiini Chake na vilevile ni ufunuo wa kipengele kimoja cha tabia Yake na hekima Yake, zote hizi ni hatua zisizozuilika katika mpango Wake wa usimamizi. Hili halifai kupuuzwa! Mapenzi ya Mungu yamo katika chochote Anachofanya; Mungu haogopi maoni yasiyo mahali pake wala haogopi dhana au fikira zozote za binadamu kuhusu Yeye. Yeye hufanya kazi Yake tu, na kuendeleza usimamizi Wake, kulingana na mpango Wake wa usimamizi, usiozuiliwa na mtu yeyote, suala lolote au kifaa chochote.
SAWA, ni hayo kwa leo. Tuonane wakati mwingine!
Juni 13, 2014
Tanbihi:
a. Maandishi asilia yanasoma “vitendo.”
b. Maandishi asilia yameacha “kichwa cha.”
c. Maandishi asilia yameacha “kupotezwa kwa.”
d. Maandishi asilia yameacha “ yaliyokuwa yameenda.”
e. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.
                                                                                     kutoka kwa Neno Laonekana Katika Mwili
Yaliyopendekezwa: Umeme wa Mashariki

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni