Jumapili, 10 Machi 2019

Neno la Mungu | Sura ya 100

Mwenyezi Mungu alisema, Ninawachukia wale wote ambao hawajajaaliwa na kuchaguliwa na Mimi. Kwa hiyo ni lazima Niwafukuze watu hawa kutoka katika nyumba Yangu mmoja baada ya mwingine, hivyo hekalu Langu litakuwa takatifu na bila doa, nyumba Yangu itakuwa mpya daima na haitakuwa nzee kamwe, jina Langu takatifu litaenezwa milele na watu Wangu watakatifu watakuwa wapendwa Wangu. Aina hii ya mandhari, aina hii ya nyumba, aina hii ya ufalme ni lengo Langu, makao Yangu nayo ni msingi wa uumbaji Wangu wa vitu vyote.

Jumamosi, 9 Machi 2019

Maneno ya Roho Mtakatifu | “Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu” (Sehemu ya Kwanza)

Maneno ya Roho Mtakatifu | “Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu” (Sehemu ya Kwanza)

Mwenyezi Mungu anasema, "Katika kila aina ya kazi ya Mungu kuna maono yanayofahamika na mwanadamu; maono yanayofuatwa na matarajio mwafaka ya Mungu kwa mwanadamu. Bila haya maono kama msingi, mwanadamu hawezi kuwa na uwezo wa utendaji na pia hangeweza kumfuata Mungu bila kuyumbayumba. Ikiwa mwanadamu hamjui Mungu au hayaelewi mapenzi ya Mungu, basi yote ayafanyayo ni bure na yasiyoweza kukubalika na Mungu. 

Ijumaa, 8 Machi 2019

neno la Mungu | Fumbo la Kupata Mwili (4)

Mwenyezi Mungu alisema, Mnapaswa kujua kuhusu hadithi ya ndani na uumbaji wa Biblia. Ufahamu huu haushikiliwi na wale ambao hawajakubali kazi mpya ya Mungu. Wao hawajui. Waelezee mambo haya ya kiini, na hawatakuwa pamoja nawe wenye kushikilia sana elimu ya vitabuni na sheria kuhusu Biblia. Wao huchunguza kwa uthabiti kile ambacho kimetabiriwa: Kauli hii imeshatimia? Kauli ile imeshatimia? Kukubali kwao injili ni kwa mujibu wa Biblia; wao huhubiri injili kulingana na Biblia. 

Alhamisi, 7 Machi 2019

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Ahadi kwa Wale Ambao Wamekamilishwa”

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Ahadi kwa Wale Ambao Wamekamilishwa”


Mwenyezi Mungu anasema, “Wale watakaokamilishwa na Mungu ni wale watakaopokea baraka za Mungu na urithi Wake. Yaani, wanasikia na kuelewa kile Mungu Alicho nacho na Alicho, ili kiwe kile ambacho walicho nacho ndani yao; wanayo maneno yote ya Mungu ndani yao; haijalishi ni vipi nafsi ya Mungu ilivyo, mnaweza kusikia na kuelewa kila kitu Anachokuambia vile kilivyo, na hivyo kuishi kwa kudhihirisha ukweli. Huyu ndiye aina ya binadamu aliyekamilishwa na Mungu na aliyepatwa na Mungu.”

Jumatano, 6 Machi 2019

Hudumu kama Waisraeli Walivyofanya

Hudumu kama Waisraeli Walivyofanya

Mwenyezi Mungu alisema, Siku hizi watu wengi hawatilii maanani mafunzo yapi yanayopaswa kusomwa wakati wa upatano na wengine. Nimegundua kuwa wengi wenu hawawezi kujifunza mafunzo hata kidogo wakati wa ushirikiano na wengine. Wengi wenu mnashikilia maoni yenu mwenyewe, na wakati mnafanya kazi kanisani, unatoa maoni yako na yeye anatoa yake, moja uhusiano na mingine, bila kushirikiana kabisa.

Jumanne, 5 Machi 2019

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa “Maonyo Matatu” | How to Be a Loyal Servant of God

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa “Maonyo Matatu” | How to Be a Loyal Servant of God


Mwenyezi Mungu anasema, “Kama muumini wa Mungu, hufai kuwa watiifu kwa yeyote mwingine isipokuwa Yeye katika mambo yote na mjilinganishe na moyo Wake katika mambo yote. Hata hivyo, ingawa wote huelewa mafundisho haya, ukweli huu wa kimsingi ulio wazi kabisa kwa binadamu hauwezi kuonekana kuwa kujumuishwa kwao kikamilifu, kutokana na ugumu wao, kama vile hali yao ya kutojua, upuzi, au ufisadi.

Jumatatu, 4 Machi 2019

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Kutanafusi kwa Mwenye Uweza”

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Kutanafusi kwa Mwenye Uweza”

Mwenyezi Mungu anasema, “Wanadamu, walioacha ruzuku ya uzima kutoka kwa mwenye Uweza, hawajui kwa nini wanaishi, na bado wanaogopa kifo. Hukuna usaidizi, hakuna msaada, lakini bado wanadamu wanasita kufumba macho yao, wakiyakabili yote bila woga, wanaendeleza kwa muda mrefu kuishi kwa aibu ulimwenguni humu katika miili isiyokuwa na utambuzi wa nafsi. Unaishi hivyo, pasipo matumaini; anaishi hivyo, pasipo kuwa na lengo.