Jumatano, 5 Desemba 2018

Neno la Mungu | "Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya"


Neno la Mungu | "Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya"

Mwenyezi Mungu anasema, "Kuonekana kwa Mungu hurejelea kuwasili Kwake duniani kufanya kazi Yake. Akiwa na utambulisho na tabia Yake, na katika mbinu Yake ya asili, Yeye hushuka miongoni mwa wanadamu kufanya kazi ya kuanzisha enzi mpya na kukamilisha enzi nyingine. Kuonekana kwa aina hii si aina fulani ya sherehe. Si ishara, picha, muujiza, au ono kuu, na hata zaidi si mchakato fulani wa kidini. Ni ukweli halisi ambao waweza kushikwa na kuonekana. 

Jumanne, 4 Desemba 2018

Tamko la Sabini na Tatu

Tamko la Sabini na Tatu

Mwenyezi Mungu alisema, Maneno Yangu yanatimizwa mara tu yanaposemwa; hayabadiliki kamwe na ni sahihi kabisa. Kumbuka hili! Kila neno na kirai kutoka katika kinywa Changu lazima yafikiriwe kwa uangalifu. Kuwa makini zaidi, usije ukapitia upotezaji na kupokea hukumu Yangu, ghadhabu Yangu na moto Wangu pekee. Kazi Yangu sasa inasonga kwa haraka sana, lakini ni safi na ni ya kutaka uangalifu mkubwa hadi kwa kiasi fulani—karibu haionekani kwa jicho tupu na haiwezi kuguswa na mikono ya mwanadamu.

Neno la Mungu | "Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu" (Sehemu ya Kwanza)

Neno la Mungu | "Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu" (Sehemu ya Kwanza)

Mwenyezi Mungu anasema, "Hatua tatu za kazi ndizo kiini cha usimamizi mzima wa Mungu, na ndani yazo zimeelezwa tabia ya Mungu na kile Alicho. Wale wasiojua kuhusu hatua tatu za kazi ya Mungu hawana uwezo wa kutambua jinsi Mungu anavyoonyesha tabia Yake, wala hawajui hekima ya kazi ya Mungu, na wanasalia kutojua njia nyingi Anazomwokoa mwanadamu, na mapenzi Yake kwa wanadamu wote. Hatua tatu za kazi ndizo maonyesho kamili ya kazi ya kumwokoa mwanadamu. Wale wasiofahamu hatua tatu za kazi watakosa kuelewa njia mbalimbali na kanuni za kazi ya Roho Mtakatifu;

Jumatatu, 3 Desemba 2018

Tamko la Sabini na Nne

Tamko la Sabini na Nne

Mwenyezi Mungu alisema, Wamebarikiwa wale ambao wamelisoma neno Langu na kuamini kwamba litatimizwa—Sitakutendea vibaya, lakini Nitafanya yale unayoamini yatimizwe kwako. Hii ni baraka Yangu ikija juu yako. Neno Langu linapiga siri zilizofichwa ndani ya kila mtu. Kila mtu ana majeraha ya mauti, na Mimi ni tabibu mzuri ambaye anayaponya—njoo tu katika uwepo Wangu. Kwa nini Nilisema kuwa katika siku zijazo hakutakuwa tena na huzuni na hakutakuwa na machozi? Ni kwa sababu ya hili.

Neno la Mungu | "Wale Waliofanywa Kuwa Watimilifu Ndio tu Wanaoweza Kuishi Maisha Yenye Maana"

Neno la Mungu | "Wale Waliofanywa Kuwa Watimilifu Ndio tu Wanaoweza Kuishi Maisha Yenye Maana"

Mwenyezi Mungu anasema, "Wale waliofanywa kuwa watimilifu hawawezi tu kuwa watiifu baada ya kushindwa, lakini wanaweza pia kuwa na maarifa na kubadilisha tabia yao. Wanamjua Mungu, wamepitia njia ya Mungu mwenye upendo, na wamejazwa na ukweli. Wanajua namna ya kupitia kazi ya Mungu, wanaweza kuteseka kwa ajili ya Mungu, na wanayo mapenzi yao wenyewe. … Kufanywa kuwa watimilifu kunarejelea wale ambao, baada ya kukamilika kwa kazi ya ushindi, wanaweza kufuatilia ukweli na kufaidika kutoka kwa Mungu.

Jumapili, 2 Desemba 2018

Tamko la Themanini na Sita

Tamko la Themanini na Sita

Watu husema kuwa Mimi ni Mungu mwenye huruma na wao husema kwamba Nitaoa wokovu kwa kila kitu Nilichokiumba—mambo haya yote yanasemwa kulingana na fikira za binadamu. Kunitaja Mimi kama Mungu mwenye huruma kunaelekezewa wazaliwa Wangu wa kwanza na kuletea Kwangu wokovu kunaelekezewa wazaliwa Wangu wa kwanza na watu Wangu. Kwa sababu Mimi ni Mungu mwenye hekima, ni wazi katika mawazo Yangu ni nani Ninaowapenda na ni nani Ninaowachukia.

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Katika Imani Yako kwa Mungu Unapaswa Kumtii Mungu"


Maneno ya Roho Mtakatifu | "Katika Imani Yako kwa Mungu Unapaswa Kumtii Mungu"


Mwenyezi Mungu anasema, "Jambo muhimu katika kumtii Mungu ni kuitambua nuru mpya, na kuweza kuikubali na kuiweka katika vitendo. Huu pekee ndio utii wa kweli. ... Kutoridhika na kuishi katikati ya neema za Mungu, kuwa na kiu ya ukweli, na kutafuta ukweli, na kunuia kuchumwa na Mungu—hii ndio maana ya kumtii Mungu katika hali ya utambuzi; hii ndiyo aina ya imani ambayo Mungu anataka."