Jumatatu, 3 Desemba 2018

Neno la Mungu | "Wale Waliofanywa Kuwa Watimilifu Ndio tu Wanaoweza Kuishi Maisha Yenye Maana"

Neno la Mungu | "Wale Waliofanywa Kuwa Watimilifu Ndio tu Wanaoweza Kuishi Maisha Yenye Maana"

Mwenyezi Mungu anasema, "Wale waliofanywa kuwa watimilifu hawawezi tu kuwa watiifu baada ya kushindwa, lakini wanaweza pia kuwa na maarifa na kubadilisha tabia yao. Wanamjua Mungu, wamepitia njia ya Mungu mwenye upendo, na wamejazwa na ukweli. Wanajua namna ya kupitia kazi ya Mungu, wanaweza kuteseka kwa ajili ya Mungu, na wanayo mapenzi yao wenyewe. … Kufanywa kuwa watimilifu kunarejelea wale ambao, baada ya kukamilika kwa kazi ya ushindi, wanaweza kufuatilia ukweli na kufaidika kutoka kwa Mungu.

Jumapili, 2 Desemba 2018

Tamko la Themanini na Sita

Tamko la Themanini na Sita

Watu husema kuwa Mimi ni Mungu mwenye huruma na wao husema kwamba Nitaoa wokovu kwa kila kitu Nilichokiumba—mambo haya yote yanasemwa kulingana na fikira za binadamu. Kunitaja Mimi kama Mungu mwenye huruma kunaelekezewa wazaliwa Wangu wa kwanza na kuletea Kwangu wokovu kunaelekezewa wazaliwa Wangu wa kwanza na watu Wangu. Kwa sababu Mimi ni Mungu mwenye hekima, ni wazi katika mawazo Yangu ni nani Ninaowapenda na ni nani Ninaowachukia.

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Katika Imani Yako kwa Mungu Unapaswa Kumtii Mungu"


Maneno ya Roho Mtakatifu | "Katika Imani Yako kwa Mungu Unapaswa Kumtii Mungu"


Mwenyezi Mungu anasema, "Jambo muhimu katika kumtii Mungu ni kuitambua nuru mpya, na kuweza kuikubali na kuiweka katika vitendo. Huu pekee ndio utii wa kweli. ... Kutoridhika na kuishi katikati ya neema za Mungu, kuwa na kiu ya ukweli, na kutafuta ukweli, na kunuia kuchumwa na Mungu—hii ndio maana ya kumtii Mungu katika hali ya utambuzi; hii ndiyo aina ya imani ambayo Mungu anataka."


Jumamosi, 1 Desemba 2018

Tamko la Tisini

Tamko la Tisini

Mwenyezi Mungu alisema, Wote walio vipofu lazima waondoke kutoka Kwangu na wasiwepo kwa muda zaidi hata kidogo, kwani wale ambao Nataka ni wale ambao wanaweza kunijua, wanaoweza kuniona na wanaoweza kupata vitu vyote kutoka Kwangu. Na wanaoweza kweli kupata vitu vyote kutoka Kwangu ni nani? Hakika kuna wachache sana wa mtu wa aina hii na hakika watapata baraka Zangu.

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Je, Umekuwa Hai Tena?"

Maneno ya Roho Mtakatifu | "Je, Umekuwa Hai Tena?"

Mwenyezi Mungu anasema, "Ikiwa watu wanatamani kuwa viumbe hai, na kuwa na ushuhuda wa Mungu, na kuthibitishwa na Mungu, wanapaswa kukubali wokovu wa Mungu, wanapaswa kuwa watiifu katika hukumu na kuadibu Kwake, na wanapaswa kukubali kwa furaha kushughulikiwa na kupogolewa na Mungu. Baada ya hapo ndipo wataweza kuweka katika matendo ukweli wote unaohitajika na Mungu, na baada ya hapo ndipo wataweza kupata wokovu wa Mungu, na kuwa viumbe hai kabisa.

Ijumaa, 30 Novemba 2018

Tamko la Tisini na Moja

Tamko la Tisini na Moja

Roho Wangu huongea na kutamka sauti Yangu daima—wangapi kati yenu wanaweza kunijua Mimi? Kwa nini lazima Nipate mwili na kuja kati yenu? Hili ni fumbo kubwa. Ninyi mnanifikiria kuhusu Mimi na kunitamani sana siku nzima, na mnanisifu, kunifurahia na kunila na kuninywa kila siku, na ilhali leo bado hamnijui Mimi. Ninyi ni wajinga na vipofu kweli! Jinsi gani mnavyonijua kidogo! Ni wangapi kati yenu wanaweza kufikiria kuhusu mapenzi Yangu? Yaani, ni wangapi kati yenu wanaoweza kunijua?

Matamshi ya Mungu | "Wale wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watakubaliwa na Mungu"

Matamshi ya Mungu | "Wale wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watakubaliwa na Mungu"

Mwenyezi Mungu anasema, "Kazi ya Roho Mtakatifu inabadilika kutoka siku hadi siku, ikipanda juu kwa kila hatua; ufunuo wa kesho unakuwa hata juu kuliko wa leo, hatua kwa hatua ukikwea hata juu zaidi. Hii ndiyo kazi anayotumia Mungu kumkamilisha mwanadamu. Iwapo mwanadamu hawezi kwenda sambamba, basi anaweza kuachwa wakati wowote. Kama mwanadamu hana moyo wa kutii, basi hawezi kufuata hadi mwisho. Enzi ya kale imepita; sasa ni enzi mpya. Na katika enzi mpya, kazi mpya lazima ifanywe.